Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nchi yetu kadiri siku zinavyoenda mbele, imeshuhudia zikitungwa sheria nyingi za kuirudisha nchi nyuma, yaani sheria nyingi zimekuwa za kuwatesa na kuwaonea wananchi. Ni sheria za kuhalalisha uovu dhidi ya wananchi:
1.
Tulikuwa na sheria ya vyama vya siasa, lakini baadaye ikabadilishwa hiyo sheria ili kuvibana na kuvitisha vyama vya siasa.
1. Tulikuwa na sheria inayomlinda Rais hata akifanya uovu gani asishtakiwe. Watu walikuwa wakilalamikia sheria hiyo. Wakati watu wakitaka sheria hiyo ya kinga kwa Rais kutokushtakiwa akifanya uhalifu, iondolewe, wakatunga sheria ya kuongeza watu ambao hata wafanye uovu wa namna gani dhidi ya wananchi, hawawezi kushtakiwa. Zaidi ya Rais, wakaongezwa Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu!!
2. Wakati watu wakilalamikia utendaji wa hovyo wa vyombo vya usalama, hasa polisi na TISS, wakatunga sheria kuwa sasa TISS waruhusiwe kuwakamata watu wanaowataka kwa njia za kificho, wanaweza kuwashikilia, na hata wakiwafanyia uovu wowote ule, na hata ikithibitika hao watu waliofanyiwa uovu hawakuwa na hatia yoyote, hao maofisa wa TISS, kamwe hawawezi kushtakiwa kwa huo uovu walioufanya.
3. Hivi karibuni tumeshuhudia tena, serikali ikitunga kanuni za uchaguzi ambazo zinatamka wazi kuwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi, hata wakitenda jinai wakati wa zoezi la uchaguzi, kamwe hawawezi kushtakiwa!!
Swali la kujiuliza wewe mwananchi: Hivi hii serikali ipo kwaajili ya kulinda uovu wa wakuu wa Serikali? Hivi hii Serikali ina maana ipo kwaajili ya kutenda uovu dhidi ya wananchi ndiyo maana wakati wote inaunda sheria za kulinda uovu na waovu?
FIkiria kuwa hizo sheria za kulinda waovu wa serikali, kabla ya kuwa sheria, mswada uliandaliwa na Serikali. Hivi Serikali iliyoandaa miswada ya kulinda uovu, ni serikali kweli, au genge la maharamia dhidi ya wananchi lilipo ndani ya Serikali? Baada ya mswada kuandaliwa, ulipelekwa bungeni, halafu na hao wabunge wakapitisha, hivi hao ni wabunge wa wananchi au genge linalotumika na wahalifu kuhalalisha uhalifu wao? Baada ya Bunge, miswada hiyo ilipelekwa kwa Rais, na Rais akaridhia na kusaini. Hivi huyu Rais ni Rais kwaajili ya watu gani? Ni Rais kwaajili ya wananchi au makundi ya kihalifu ndani ya Serikali? Rais unasaini vipi mswada unaolenga kufuta haki za watu unaowaongoza?
Fikiria Rais anayehalalisha TISS kuwakamata watu kwa kificho, kuwafanya lolote hao watu, halafu hao maafisa wa TISS hata ikidhihirika wamemfanyia mtu uovu, hairihusiwi kuwashtaki!! Matokeo yake, ndiyo haya tunayoyaona.
Kwa mazingira ya sasa, na sheria hizo mbaya za kulinda waovu dhidi ya wananchi, wacha wananchi wawalinde, maana waliotakiwa kuwalinda wamegeuka na kuwa dhidi yao.