Kwanini Shilingi ya Kenya ina thamani kuliko Shilingi ya Tanzania?

wazanaki

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2020
Posts
1,092
Reaction score
808
Wakuu turejee.

Huwa najiuliza. Wanaohusika ku adjust (kupandisha na kushusha) thamani ya pesa kwenye mataifa ya kidunia ni nani (najua hii process haifanyei na mungu inafanywa na binadamu)

Pia nilikua najiuliza, Kenya mbona sometimes uchumi wake unayumba lakini thamani yake ya pesa inanaki palepale licha ya kwamba tanzania kuna mali za kutosha na nguvu kazi. Na sisi ndo tunalisha almost east africa nzima. Kama sisi ndo tunategemewa kwa nn sisi ndo pesa yetu isiwe na value kuliko pesa ya nchi yoyote inayo tuzunguka east afrika. Tunafeli wapi.

Pia tunajua nchi kama Kenya thamani yake ya pesa ni kubwa kuliko yetu inakua na advantage kubwa sana kutulalia. Kwa maana ya kwamba. Kwa kazi ile ile atakayofanya Mkenya na Mtanzania.

Mkenya ata gain more akitumia pesa yake. Kwa maana ya kwamba mkenya akija na pesa yaje Tanzania anaweza akanunua magunia ya chakula mengi zaidi kuliko wewe ukienda kenya na tsh. Kwa hiyo hii inampa mkenya advantage ya kutofanya kazi nyingi kama mtz.

Hii ni opinion yangu. Kama una i-challenge. Naomba uje kwenye mada.
 
Kwanza nikutoe tongotongo. Currency ya nchi kuwa juu haimanishi kuwa na uchumi uko juu Sawa, currency kuwa juu au chini inaathiriwa na monetary na fiscal policy ya nchi husika kulingana na nini inachotaka nchi husika. Pia kumbuka ksh ipo karibu Sawa na yen ya Japan.
 
Ok. Nani anasimamia process nzima ya currency adjustment( kupanda au kushuka) ili makosa yasitokee
 
Ukitaka kujua tulifikaje hapa inabidi uanzie kwenye vita ya kagera na after effects zake then uje kwenye masharti ya ifm na wb kwa Nyerere kutaka serikali ishushe thamani ya shilingi yake ili ipate misaada..since then tumeweza ku maintain the gape difference bt not catch up to them.
 
Yes..economics..achana na kusoma uchumi mkuu..unatakiwa kusoma hata ukiwa ushamaliza kusoma..yaan som ujue dunia inaendaje[emoji3062]
Na hiki ndo wengi hawakifanyi. Afu ukianza ku argue anakurudisha kwenye point za kwenye notes za darasani.
 
Hahahaa lima tu mahindi mkuu..wasalimie mfaranyaki...mie natesekea Tinde huku
Mahindi bei ipo juu kuliko dar watu wamekata mitaji hadi wengine tunauguza depression mixer presha
Unanunua gunia la mahindi 45000 , ulisafirishe. Hadi manzese dar halafu unakuta gunia hilo bei ya soko ni 35000
Ukiwa na gunia 300 plus , kuzimia na. Kuanguka inakuwa ni option rahisi, kuliko kukomaaa ukagongwe na magari kwa mawazo
Wasalimie isaka hapo
 
Mimi huwa naona ni digits tu ndio huwa tunatofautiana,ila sio Uchumi kukua.kwa mfano,
Shilingi 10000 ya Tanzania ni Sawa na Ksh 450 lakini hapo haimaanishi hiyo 450 ni rahisi kupatikana ukiwa kenya.ni kwamba malipo yaleyale ya tsh 10000 kwa tanzania na kwa kenya ni 450.yani mzazi fukara wa kenya hawezi kumpa mwanae 450 akatumie shuleni ni hela kubwa pia kwao.
 
Kuna fedha za nchi nyingne unaweza beba kwenye wallet hata noti ambazo ukizibadili kwa bei ya hapa nchini unakua na 6-7millions
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…