Kwanini show nyingi za wasanii wa muziki hufanyika sana Mwanza na Kahama?



Mkuu pengine huijui vizuri Kahama! Kwanza tambua kuwa Kahama ni wilaya ya pili nchini katika kuchangia pato la taifa baada ya Ilala. Kahama inamiliki migodi miwili mikubwa nchini ambayo huwalipi basic nzuri wafanyakazi wake, Acacia-Buzwagi na Acacia-Bulyanhulu ambao ndiyo mgodi mkubwa wa underground kuliko yote East and Central Africa, kuna migodi mingi sana midogo midogo ambayo inachangia kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa pesa, kuna posho mills za kutosha ambazo huwauzia mchele wapemba, Kahama ina ardhi nzuri kwa kilimo kwahiyo watu wengi wanajipatia fedha lukuki kupitia kilimo pia kahama ni sehemu ambayo ina muingiliano mkubwa wa watu wa east africa, mfano mtu anayeenda kongo ya bukavu, Rwanda, Burundi na Uganda lazima alale Kahama.
 
Vp mkuu mzunguko wa pesa uko vzr au umekaaje kaaje mkuu(yaani kwa ujumla)?
Mwanza hali ya pesa/fedha iko vizuri, na mzunguko uko vizuri pia mahitaji muhimu sio ya gharama labda mwenyewe tu upende kujiinua!!!
Karibu Mwanza
 



Kuna UKIMWI kuzidi njombe na makete?
 
Mwanza hali ya pesa/fedha iko vizuri, na mzunguko uko vizuri pia mahitaji muhimu sio ya gharama labda mwenyewe tu upende kujiinua!!!
Karibu Mwanza
Asante sana mkuu, nilishawahi kuishi kipindi flani hivi,niliona gharama za maisha zilikua za kawaida na pia wenyeji wa Mwz hawana noma na mtu kabisaa.

Ila kipindi hiki cha mzee baba ndo nilikua sina uhakika na mzunguko wa pesa kwa upande wa biashara mkuu.
 
Pako vizuri kabisa,karibu sana
 
Mwanza wasukuma bado washamba sana kuna wasanii wao huku wanaimba kisukuma yani wanapiga hela mbaya
 
Me nimezaliwa mwanza Mabatin,Ila kinacho fanya mwanza ijaze kwenye show za wasanii ni kutokana na uwepo wa vijana weng wanao toka vijiji vya mikoa ya jiran,kigoma,shinyanga,tabora n,k,Hawa vijana weng huja na ushamba flan, Na kutokana na upataji wa pesa ulivo rahis hapa mwanza vijana hawa hujikuta wana shobokea vitu kama hivyo,hata kahama ni hivo hvo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…