Iron Man Triple 3
Member
- Jun 19, 2019
- 20
- 26
Aman iwe juu yenu
Naomba kuuliza ni kwanini wasanii wengi hupenda sana kwenda kufanya show zao kahama na mwanza ambayo ni mikoa masikin kwa majubi wa takwimu za taifa
Je kahama kwa masikin kuna nini mbona show nyingi hufanyika sana pale na tena show za bei kubwa kubwa
Tena show nyingi hufanyika za one man show
Alianza alikiba akajaza uwanja kaja diamond kajaza uwanja nandy naye alijaza uwnja chege na wasanii wengi pia hujaza uwaja
Tukija kwa jiji kubwa na la pili kwa ukubwa nchi nzima ambalo kwa mujibu wa takwimu za taifa ni jiji masikin sana. Napo show hufanyika za kibabe sana tena za kila mwaka
Mwanza kunaweza fanyika show hata tano kwa siku na kila show ikajaza watu
Moja inaweza kuwa isamilo ikajaza na nyingine inaweza kuwa jembe ikajaza na nyingine inaweza kuwa villa ikajaza na nyingine inaweza gold crest ikajaza pia
Je sasa kwanini sehemu hizi masikin hutema sana pesa kushinda sehemu tajili nchini
Nawasilisha
Mayala B
Mkuu pengine huijui vizuri Kahama! Kwanza tambua kuwa Kahama ni wilaya ya pili nchini katika kuchangia pato la taifa baada ya Ilala. Kahama inamiliki migodi miwili mikubwa nchini ambayo huwalipi basic nzuri wafanyakazi wake, Acacia-Buzwagi na Acacia-Bulyanhulu ambao ndiyo mgodi mkubwa wa underground kuliko yote East and Central Africa, kuna migodi mingi sana midogo midogo ambayo inachangia kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa pesa, kuna posho mills za kutosha ambazo huwauzia mchele wapemba, Kahama ina ardhi nzuri kwa kilimo kwahiyo watu wengi wanajipatia fedha lukuki kupitia kilimo pia kahama ni sehemu ambayo ina muingiliano mkubwa wa watu wa east africa, mfano mtu anayeenda kongo ya bukavu, Rwanda, Burundi na Uganda lazima alale Kahama.