Ni fikra na mawazo mabovu kudhani waislamu wanafeli kwasababu ya uislamu wao. Sababu kubwa ya shule za kikiristo kifaulisha sana ni mchujo wa wanafunzi unaofanywa ili kupata the best kama unavyoweza kuona Kwa shule kama St. Francis Mbeya, na shule nyengine nyingi.
Waislamu Kwa kutambua maana na lengo la elimu, ambalo ni kubadilisha jamii kuwa jamii Bora na yenye manufaa Kwa watu, kamwe hawawezi kumkataa mwanafunzi eti Kwa sababu hawezi kuperform Kwa namna flani. Ukiona kijana kafukuzwa shule ya kiislamu basi ni kwasababu za kimaadili Tena zilizovuka mipaka.
Lengo la elimu ni kufanya jamii yetu kuwa Bora, lakin ingawa watu wanajisifu kwa kufaulisha sana Tena Kwa one za saba, lakini kama nchi Bado tunazidi kuwa masikini, Bado tunategemea nchi za Ulaya, Amaerika, na Asia kuendesha maisha yetu. Tumeshindwq hata kutengeneza vijiko vya kulia wali. Wapo wapi wasomi wetu tunaotamba nao.
Labda tungejiuliza ni Kwa namna tunaweza kuzibadilisha hizi higher performances na kuwa manufaa kwa jamii. Yapo wapi manufaa ya elimu yetu hali ya kuwa tumeshindwa hata ku-control uchafu. Ukitembea katika baadhi ya miji yetu utaona mitaro ya Maji ya mvua inatiririsha kinyesi cha binadamu, wapo wapi walijitapa Kwa ufaulu basi wayaweke mazungira yetu safi.
Wengi wa wasomi wa kiafrika, maprofesa kwa madaktari wanaishia kuwa mafisadi, yapo wapi manufaa ya elimu ambayo mnanisifia nayo enyi wakristo wa Tanzania. Tena mara nyingi wengi wa viongozi wa kiislamu, walioifahamu dini na dunia yao, wapo katika kutenda haki na ni waadilifu wa kweli.