Kwanini shule za kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa?

Kwanini shule za kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa?

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2024 yanaonesha tena kwamba shule za Kanisa Katoliki zimeendelea kuongoza kwa viwango vya juu vya ufaulu. Kwa mfano, kati ya watahiniwa 19,182 waliotoka kwenye shule za Kanisa, asilimia 97.72 walipata daraja la kwanza hadi la tatu, huku asilimia 0.04 pekee wakipata daraja la sifuri.

Kwa upande mwingine, shule za Kiislamu hazijajitokeza kwa wingi katika nafasi za juu za ufaulu. Hali hii imekuwa ikiendelea kwa miaka mingi, na inazua maswali: Kwa nini shule za Kiislamu hazifanyi vizuri katika mitihani ya taifa? Je, tatizo ni mfumo wa elimu, usimamizi, au kuna mambo mengine yanayochangia hali hii?

TATIZO LIKO WAPI?

Uchambuzi wa hali ya shule za Kiislamu unaonesha changamoto mbalimbali zinazoweza kuwa sababu ya matokeo yasiyoridhisha.

1. Changamoto ya Usimamizi

Shule nyingi za Kiislamu huanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya kidini pamoja na elimu ya kawaida. Hata hivyo, usimamizi wa shule hizi mara nyingi haupo kwenye mfumo thabiti kama ule wa shule za Kanisa, ambazo zinakuwa chini ya taasisi zilizo na uzoefu wa miaka mingi katika uendeshaji wa taasisi za elimu.

Shule nyingi za Kanisa zinamilikiwa na majimbo ya Kanisa Katoliki, ambayo yana mtandao mpana wa usimamizi, huku bodi za shule zikiwa na utaratibu wa kufuatilia mwenendo wa kila taasisi. Kwa upande wa shule za Kiislamu, mara nyingi usimamizi wake hutegemea watu binafsi au taasisi zisizo na mfumo madhubuti wa ufuatiliaji wa maendeleo ya shule na walimu.

2. Mchanganyiko wa Mtaala

Shule za Kiislamu zina jukumu la kufundisha masomo ya dini pamoja na masomo ya mtaala wa serikali. Wanafunzi hutumia muda mwingi kwenye masomo ya dini, jambo ambalo linaweza kupunguza muda wao wa kujifunza masomo ya kawaida.

Kwa mfano, shule za Kanisa zinazingatia mfumo wa mtaala wa serikali kwa ukamilifu, huku masomo ya dini yakiwa sehemu ya malezi badala ya kuwa sehemu kubwa ya ratiba ya shule. Kwa upande wa shule za Kiislamu, mgawanyo wa muda kati ya masomo ya dini na masomo ya kawaida unaweza kuathiri maandalizi ya wanafunzi kwa mitihani ya taifa.

3. Ukosefu wa Walimu Bora

Moja ya sababu kubwa zinazochangia ufaulu wa shule za Kanisa ni uwekezaji mkubwa katika walimu wenye sifa na uzoefu. Shule hizi huwalipa walimu vizuri, huwapa mafunzo ya mara kwa mara, na kuhakikisha mazingira mazuri ya kufundisha.

Kwa upande wa shule nyingi za Kiislamu, changamoto ya bajeti inasababisha walimu wengi wasilipwe vizuri au kutokuwa na mafunzo ya mara kwa mara ya kuongeza ufanisi wa ufundishaji. Hii inapelekea shule kukosa walimu wenye weledi wa kutosha kuandaa wanafunzi kwa ushindani wa kitaifa.

4. Miundombinu Duni

Shule za Kanisa zinahakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia, ikiwa ni pamoja na maabara bora, maktaba za kisasa, na vifaa vya kujifunzia vya kutosha. Kwa upande wa shule nyingi za Kiislamu, ukosefu wa rasilimali hizi ni changamoto kubwa, jambo ambalo linaweza kuathiri viwango vya ufaulu.

5. Motisha kwa Wanafunzi

Katika shule za Kanisa, kuna utamaduni wa kushindanisha wanafunzi na kuwatia motisha kupitia zawadi na mfumo wa kutambua juhudi zao. Wanafunzi wanahamasishwa kushiriki katika mashindano ya kitaaluma na kupewa mwongozo wa karibu na walimu wao.

Kwa upande wa shule za Kiislamu, motisha kama hizi hazionekani kupewa kipaumbele kwa kiwango kikubwa. Hali hii inawafanya wanafunzi wengi wasikazane katika masomo ya kawaida kwa bidii ile ile inayoshuhudiwa katika shule za Kanisa.

NINI KIFANYIKE KUBORESHA UFAULU WA SHULE ZA KIISLAMU?

Ili shule za Kiislamu zifanye vizuri zaidi katika mitihani ya taifa na kushindana na shule za Kanisa, yafuatayo yanapaswa kufanyiwa kazi:

1. Kuimarisha Usimamizi
Shule za Kiislamu zinahitaji kuwa na mfumo thabiti wa usimamizi, kwa mfano, kuanzisha bodi za uendeshaji zitakazowajibika kufuatilia maendeleo ya shule na kuhakikisha viwango bora vya elimu vinazingatiwa.


2. Kuboreshwa kwa Mtaala
Badala ya kugawanya muda kati ya masomo ya dini na masomo ya kawaida kwa namna inayoweza kuathiri ufaulu, shule zinapaswa kuhakikisha kuwa ratiba ya masomo inatilia mkazo maandalizi ya mitihani ya taifa huku masomo ya dini yakipangwa kwa namna isiyozuia maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.


3. Uwekezaji Katika Walimu
Shule za Kiislamu zinapaswa kuweka kipaumbele katika kuajiri na kuwahifadhi walimu wenye sifa bora kwa kuhakikisha wanapewa mishahara mizuri na mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha mbinu zao za ufundishaji.


4. Kuboresha Miundombinu
Kama ambavyo shule za Kanisa zinawekeza katika maabara, maktaba na vifaa vya kujifunzia, shule za Kiislamu zinapaswa kufanya vivyo hivyo ili kuwapa wanafunzi mazingira bora ya kujifunzia.


5. Motisha kwa Wanafunzi
Ni muhimu kwa shule za Kiislamu kuanzisha utaratibu wa kuwatia moyo wanafunzi kupitia tuzo kwa wale wanaofanya vizuri, programu za mashindano ya kitaaluma, na kuweka mifumo ya kuhamasisha bidii darasani.

HITIMISHO

Matokeo ya mwaka 2024 yanaendelea kuonyesha kuwa shule za Kanisa zinafanya vizuri zaidi katika mitihani ya taifa kwa sababu ya mifumo yao imara ya usimamizi, uwekezaji katika walimu, miundombinu bora, na mtazamo wa elimu kama sehemu ya maendeleo ya jamii.

Kwa upande wa shule za Kiislamu, kuna changamoto zinazohitaji kushughulikiwa ili kufanikisha matokeo bora. Ikiwa usimamizi utaimarishwa, walimu bora wataajiriwa, miundombinu itaboreshwa, na wanafunzi watapewa motisha ya kutosha, kuna uwezekano mkubwa wa kuona shule hizi zikifanya vizuri na kushindana kwa karibu na shule zinazoongoza nchini.
Wakatoliki si unajua wana Mou na serikali?
 
Kwenye nyuzi hizi makobaaz wengi huwa vipofu ghafla maana ukweli unauma, na hata wakijibu huwa pumba nyingi sana maana huwa hawataki kukiri ukweli huwa wanazunguuka. Muanzilishi wa dini hajui kusoma wala kuandika halafu utegemee taasisi za dini ya muanzilishi zifanye vizuri thubutuu mlinganyo unakataa.
Yesu alisoma chuo kikuu gani duniani? Au taja shule aliosoma std 1 tu
 
Kama hakusoma shule alijua vipi
Vizuri unakiri kabisa kuwa Yesu alienda shule na ukumbuke hiyo ilikuwa miaka mingi sana kabla ya mtume wako mudi kuwepo duniani sasa jiulize ilikuwaje mtume wako mudi aliyezaliwa miaka mingi sana baadae asijue kusoma wala kuandika yaani alikuwa mbumbumbu kiasi gani asijue hayo! na bado kaleta dini ya mchongo na wewe hushtuki tu unamuamini shtuka wewe kabla hujafa ukaenda kuzimu.
 
Hizo shule shida kubwa ni management

Yaani mkuu wa shule kachaguliwa na Bakwata ambapo huko Bakwata kuna mjomba wake ndiyo kamleta hapo

Halafu mkuu wa shule anaanza sasa kuleta maostazi ndugu zake katika imaan ndiyo wafundishe!
Wengine nj form 6 tu ila anawapa mashavu waje wafundishe watoto wa dada zake .

Pili hawana moral ethics kazini, unakuta teacher jumatatu mpaka ijumaa kapiga tu kanzu na makobazi na fimbo mkononi anasimamisha kipindi ili aende akaswali dua aje aendelee..

Mimi nilisomaga shule ya jamhuri Dodoma ile inamilikiwa na bakwata ya siku nyingi sana tangu 1982 huko ila hata kufaulu pale advance ilikuwa ni juhudi zetu tu, hakuna maboresho yoyote yale mpaka leo siwezi kukubali mwanangu aende pale au shule yoyote ya kiislamu.

Kwenye interview zao za ualimu kama huitwi juma. Mahamud au darwesh tu basi huna kazi hapo.

Malipo wanalipwa kiduchu sana na kwa mafungu mafungu mpaka labda wanafunzi walipe ada .

Mkuu wa shule mwenyewe unakjta kachoka mwenyewe vipi walimu wake si wamechakaa kabisa?
 
Watu wenye maarifa hawezi kusifia ufaulu wa Shule za Wakatoliki...hawastali kusifiwa!!!
Nasema hivyo kwa sababu wana utaratibu wa kuchuja sana wanafunzi wanaoingia shule zao....hata shule nyingine zikifanya kama wao lazima matokeo yawe mazuri ......
Mzazi anaweza kuambiwa kabisa kama mtoto wako hata fikisha maks flani itabidi umhamishe.....

Kwa mtu mwenye maarifa akiona hali kama hiyo ataona kabisa kuwa, hawana sababu ya kujisifia.... kama wangepika wanafunzi wakawaida wakawa wazuri na kufaulu vizuri; ndio tungewaelewa na KUWAPA MAUA YAO au wanataka wanafunzi wenye uwezo wa kawaida (ambao ndio wengi) na wale wenye uwezo mdogo wao wakasome wapi???
Well said,. Wanaamisha Kwa lazima Ili kubalance matokeo ya mwisho. Yani wanabakisha cream pekee
 
Watu wenye maarifa hawezi kusifia ufaulu wa Shule za Wakatoliki...hawastali kusifiwa!!!
Nasema hivyo kwa sababu wana utaratibu wa kuchuja sana wanafunzi wanaoingia shule zao....hata shule nyingine zikifanya kama wao lazima matokeo yawe mazuri ......
Mzazi anaweza kuambiwa kabisa kama mtoto wako hata fikisha maks flani itabidi umhamishe.....

Kwa mtu mwenye maarifa akiona hali kama hiyo ataona kabisa kuwa, hawana sababu ya kujisifia.... kama wangepika wanafunzi wakawaida wakawa wazuri na kufaulu vizuri; ndio tungewaelewa na KUWAPA MAUA YAO au wanataka wanafunzi wenye uwezo wa kawaida (ambao ndio wengi) na wale wenye uwezo mdogo wao wakasome wapi???
Popote wanapotaka kufankiwa kwa viwango vya juu basi mchujo lazima ndiyo maana hata university utaambiwa kuna GPA fulani inabidi mwanafunzi awe nayo ili aweze endelea na masomo kutoka mwaka hata mwaka ni mchujo huo. Ndiyo maana kwenye makampuni au taasisi zinazozingatia best practice za HRM lazima kuna performance appraisal na kuna rating unapewa kila mwaka ukipata rating ya chini unawekwa kwenye performance improvement plan ya muda fulani hujaimprove unaondolewa kazini, mchujo huo.
Kwa hiyo shule za wakatoliki kwa mwanafunzi asiyependa ushindani aliyezoea kubweteka lazima mchujo umuondoe. Kwa hiyo wakatoliki wanazingatia best academic practices.
Hata kwenye academy za soka wana mchujo kamsome wyne rooney, c.ronaldo kwenye akademy walizojifunza soka walianza wangapi na wangapi waliishia njiani na wangapi walifika mwisho na kufanikiwa kupata club za maana za kucheza soka.
Kwenye dunia ya ushindani hakuna huruma eti wenye uwezo mdogo wakasome wapi? ingekuwa hivyo basi waalimu wa vyuo vikuu wangekuwa wanachukuliwa wowote tu wale wasingekuwa wanaangalia ufaulu.
 
Sijui kama unajua ulichokiandika au una andika tu kama mashabiki wa Yanga na Simba
Mfano GPA zipo university ni kweli ila zinawekwa Labda kozi ya sheria (Law) mwanafunzi aanzie pass ya 3 +
Inamaana mwanafunzi akiwa na GPA 3 anaruhusiwa kusoma sheria; sasa kinapo ibuka chuo na kusema chenyewe kinataka wanafunzi wenye 4.5 halafu useme ni mchujo wa kawaida ....utakuwa huna maarifa!
Kwa hiyo kwa akili yako unaona kuchukua wanafunzi wenye A++ na kuwaacha wengine halafu mwisho wa siku mje hapa kujisifia kuwa mmefaulisha ni sawa?
Nisijue nilichokiandika? kweli una tatizo kwenye uelewa wako na kufikiri kwako kuna walakini mkubwa sana ndiyo maana huutaki ushindani wa viwango vya juu na unauogopa kabisaa. Wewe ni aina ya mtu unayetaka huruma huruma badala ya kupambana full kudai kamserereko. Yaani unataka kupangia kila taasisi ya elimu iwe sadakalawe aingie tu kila mwenye ufaulu unaoutaka wewe. Kwa akili yako ulitaka course kama computer engineering wachukuliwe tu hata wenye ufaulu wa chini? Nakumbuka miaka kadhaa kozi kama hiyo ya computer engineering pale UDSM ilikuwa wanaingia wanafunzi chini ya 40 Tanzania nzima hii ni kumaanisha vipanga tu tena wale cream ndo walikuwa wanafaulu kusoma hiyo kozi na katika hao wanaomaliza unakuta labda 10+ wameshindwa kufikia ufaulu uliowekwa yaani wamechujwa.
 
Back
Top Bottom