Kwanini Shule zetu za kata zinakufa? Nini kifanyike kuziinua?

Kwanini Shule zetu za kata zinakufa? Nini kifanyike kuziinua?

Joined
Dec 26, 2021
Posts
33
Reaction score
24
Kwa nini shule zetu za kata zinakufa? Na nini kifanyike tuzi-inue shule zetu za kata?

Kwa hali ya sasa, shule zetu za kata zipo kwa ajili ya kundi maskini au kundi la wasiojiweza.

Sidhani kama hii ndiyo ilikuwa nia ya kuanzisha shule hizi. Naamini kabisa shule hizi zilianzishwa kwa malengo ya kutoa elimu bora kwa Watanzania wote na kwa gharama nafuu.

Lakini kwa sasa, kinachofanyika ni nje ya malengo au kusudi lililokusudiwa. Maana shule hizi za kata zimekuwa shule za maskini.

Nini kifanyike tupate tuziimarisha na kuzikuza shule hizi?

Cha kwanza, serikali itafute namna ya kutunga sheria za kuwalazimu watumishi wa serikali wote. Mojawapo ya kigezo upate kuwa mtumishi wa serikali ni kusomesha mtoto wako shule za serikali.

Maana hawa watumishi wa serikali, miongoni mwao ndio watunga sera na mitaala ya elimu nchini. Kwa sasa hao hao watunga mitaala na sera za elimu, watoto hawasomi shule hizi.

Hii sheria ikitungwa, itasaidia kufanya marekebisho kwenye sekta ya elimu ambayo yatafanyika kwa uharaka na kupewa kipaumbele.

Tukifuatilia hata sasa, unaweza kuta watoto wa waziri wa elimu wa sasa huenda hawasomi Tanzania au kwenye shule zetu za kata.

Sasa si aibu sasa, kama mtunga sera na msimamizi wa sera, yeye hana watoto ambao wanashiriki kwenye utekelezaji wa sera hizo. Inatia shaka kuona mheshimiwa waziri husika hana imani na elimu inayotolewa na serikali.

Ni lazima serikali ikubali kuwekeza kwenye elimu, ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa. Serikali inapaswa kuwekeza kwenye kubadilisha aina ya elimu, ianze kutoa elimu ya kumfikirisha mwanafunzi na sio kumkalilisha.

Uwekezaji huo utakuwa wa kifedha, rasilimali watu, usimikaji wa sheria na sera mpya za elimu nchini.
 
Nchi hii kila mtu anataka iwe anavyotaka yeye na anavyojisikia yeye iwe.

Maisha hayafanani Wala hayalingani.

Muhimu Ni kujua unataka Nini na kutaka kitu gani kwenye Maisha.

Wenzio wanataka Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
 
Ujamaa ushakufa siku nyingi ndugu yangu!
Tafuta pesa, somesha watoto wako shule za maana.
Haya unayoyataka hayawezekani tena katika karne hii.
 
Kabla sijamaliza kusoma uzi wako nambie kwanza kama kuna kiongozi yeyote mwandamizi wa serikali na CCM anayesomesha kijana wake kwenye shulebl yeyote ya kata. HAKUNA
 
Tuchangie tuziimarishe.

Vinginevyo peleka mwanao Private schools
 
UJAMAA USHAKUFA SIKU NYINGI NDUGU YANGU!

TAFUTA PESA, SOMESHA WATOTO WAKO SHULE ZA MAANA.

HAYA UNAYOYATAKA HAYAWEZ4KANI TENA KATIKA KARNE HII.
ni kweli kabisa ndugu hata Waziri wa Elimu mwenyewe hapeleki mtoto wake KAYUMBA... chukua hatua.
 
Tatizo ni moja tu, HAZINA WALIMU WA KUTOSHA.
Kuna shule ipo chanika inaitwa nguvu mpya form one pekee ni zaidi ya 600 walimu wa hesabu shule nzima wapo wawili ha haha ha ha afu walimu wanastaafu wengne wanakufa na ajira hazitolewi.
 
Tatizo ni moja tu, HAZINA WALIMU WA KUTOSHA.
Kuna shule ipo chanika inaitwa nguvu mpya form one pekee ni zaidi ya 600 walimu wa hesabu shule nzima wapo wawili ha haha ha ha afu walimu wanastaafu wengne wanakufa na ajira hazitolewi.
Hiyo shule niliomba kujitolea hadi barua wakaniambia niandike tena masomo ya sayansi hawajaniita..sasa wa kumlaumu nan?
 
Kwa Nini shule zetu za kata zinakufa? Na Nini kifanyike tuzi-inue shule zetu za kata?

Kwa hali ya Sasa, shule zetu za kata zipo Kwa ajili ya kundi maskini au kundi la wasiojiweza.
...
Elimu msingi! Kusoma, kuandika na Kuhesabu' hili ndilo dhumuni pekee la elimu msingi mengine mbwembwe,. Ubora juu yako mzazi
 
Tatizo ni walimu na vifaa vya kufundishia lakini mleta mada solution yake ni kulazimisha watumishi wa serikali kusomesha watoto wao hapo ili kugawana umaskini , akili za maharage mabovu hizi
 
Nchi imeparanganyika.hakuna ajila za waalimu wala watumishi wa afya.
 
Tatizo ni moja tu, HAZINA WALIMU WA KUTOSHA.
Kuna shule ipo chanika inaitwa nguvu mpya form one pekee ni zaidi ya 600 walimu wa hesabu shule nzima wapo wawili ha haha ha ha afu walimu wanastaafu wengne wanakufa na ajira hazitolewi.
Unategemea mtoto wa Nguvu Mpya Secondary School apambane katika soko la ajira na mtoto wa Feza.
 
Kwa Nini shule zetu za kata zinakufa? Na Nini kifanyike tuzi-inue shule zetu za kata?

Kwa hali ya Sasa, shule zetu za kata zipo Kwa ajili ya kundi maskini au kundi la wasiojiweza.

Sidhani kama hii ndio ilikuwa nia ya kuanzisha shule hizi. Naamini kabisa shule hizi zilianzishwa Kwa malengo ya kutoa elimu Bora kwa watanzania wote na kwa gharama nafuu.

Lakini Kwa Sasa, kinachofanyika ni nje ya malengo ya au kusudi lililokusudiwa. Maana shule hizi za kata zimekuwa shule za maskini.

Nini kifanyike tupate tuziimarasha na kuzikuza shule hizi?

Cha kwanza, serikali itafute namna ya kutunga Sheria za kuwalazimu watumishi wa serikali wote. Moja wa kigezo upate kuwa mtumishi wa serikali ni usomeshe mtoto wako shule za serikali.

Maana Hawa watumishi was serikali, miongoni mwao ndio watunga sera na mitaala ya elimu nchini. Kwa Sasa hao hao watunga mitaala na sera za elimu watoto hawasomi shule hizi.

Hii Sheria ikitungwa, itasaidia kufanya marekebisho kwenye sekta ya elimu ambayo yatafanyika kwa uharaka na kupewa kipaumbele.

Tukifuatilia hata Sasa, unaweza Kuta watoto wa waziri wa elimu wa saa huenda hawasomi Tanzania au kwenye shule zetu za kata.

Sasa Si aibu Sasa, kama mtunga sera na msimamizi wa sera, yeye Hana watoto ambao wanashiriki kwenye utekelezwaji wa sera hizo. inatia shaka kuona mheshimiwa waziri husika Hana Imani na elimu inayotolewa na serikali.

Ni lazima serikali ikubali kuwekeza kwenye elimu, ndio msingi wa maendeleo ya Taifa. Serikali inapaswa kuwekeza kwenye kubadilisha aina ya elimu, ianze kutoa elimu ya kumfikirisha mwanafunzi na sio kumkalilisha.

Uwekezaji huo utakuwa wa kifedha, rasilimali watu, usimikaji wa Sheria na sera mpya za elimu nchini.
hamtaki kusoma? upo mkoa gani ambako shule zenu zinakufa?
 
Back
Top Bottom