Kwa Nini shule zetu za kata zinakufa? Na Nini kifanyike tuzi-inue shule zetu za kata?
Kwa hali ya Sasa, shule zetu za kata zipo Kwa ajili ya kundi maskini au kundi la wasiojiweza.
Sidhani kama hii ndio ilikuwa nia ya kuanzisha shule hizi. Naamini kabisa shule hizi zilianzishwa Kwa malengo ya kutoa elimu Bora kwa watanzania wote na kwa gharama nafuu.
Lakini Kwa Sasa, kinachofanyika ni nje ya malengo ya au kusudi lililokusudiwa. Maana shule hizi za kata zimekuwa shule za maskini.
Nini kifanyike tupate tuziimarasha na kuzikuza shule hizi?
Cha kwanza, serikali itafute namna ya kutunga Sheria za kuwalazimu watumishi wa serikali wote. Moja wa kigezo upate kuwa mtumishi wa serikali ni usomeshe mtoto wako shule za serikali.
Maana Hawa watumishi was serikali, miongoni mwao ndio watunga sera na mitaala ya elimu nchini. Kwa Sasa hao hao watunga mitaala na sera za elimu watoto hawasomi shule hizi.
Hii Sheria ikitungwa, itasaidia kufanya marekebisho kwenye sekta ya elimu ambayo yatafanyika kwa uharaka na kupewa kipaumbele.
Tukifuatilia hata Sasa, unaweza Kuta watoto wa waziri wa elimu wa saa huenda hawasomi Tanzania au kwenye shule zetu za kata.
Sasa Si aibu Sasa, kama mtunga sera na msimamizi wa sera, yeye Hana watoto ambao wanashiriki kwenye utekelezwaji wa sera hizo. inatia shaka kuona mheshimiwa waziri husika Hana Imani na elimu inayotolewa na serikali.
Ni lazima serikali ikubali kuwekeza kwenye elimu, ndio msingi wa maendeleo ya Taifa. Serikali inapaswa kuwekeza kwenye kubadilisha aina ya elimu, ianze kutoa elimu ya kumfikirisha mwanafunzi na sio kumkalilisha.
Uwekezaji huo utakuwa wa kifedha, rasilimali watu, usimikaji wa Sheria na sera mpya za elimu nchini.