Kwanini siasa hasa Afrika na mahsusi Tanzania ni kimbilio la watu waliofeli karibu katika kila kitu?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Ukiangalia wanasiasa wetu nchini, wengi, ima ni wababaishaji au watu waliofeli katika karibu kila jambo. Je ni kwa sababu siasa huwa haina miiko kama vile viwango vya elimu, uadilifu, uzoefu na mengine kama haya?

Je ni kwa sababu siasa ni haramu iliyohalalishwa ili wachache kuwatawala, kuwaibia na kuwaumiza wengine?

Je ni kwa sababu ni rahisi watu kuficha madhaifu yao kwenye siasa?

Je ni kwa sababu ndiko kuna ulaji wa dezo ambapo mtu anaweza kuingia kapuku leo kesho akaamka tajiri?

Je ni kwa sababu wanasiasa wetu huwa hawaambiani ukweli, kujichunguza, na kuchunguzana?

Je ni kwa sababu watu wetu walio wengi wamekata tamaa na kuwaachia wanasiasa kila kitu?

Je ni kwa sababu siasa ni kitu rahisi kufanywa hata na mjinga yeyote kwa vile ahitaji busara wala elimu?
Je ni kwanini?

 

Attachments

  • 1735848800862.png
    1 MB · Views: 3
  • 1735848964196.png
    63 KB · Views: 3
  • 1735849177123.png
    388.7 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…