Kwanini siasa za Tanzania zimeegamia kujadili yaliyopita

Kwanini siasa za Tanzania zimeegamia kujadili yaliyopita

JPM alifanya makosa makubwa na yalifichwa sasa makosa hayo yameanza kuwekwa wazi na bado sana mtaona na mtashangaa.
Habari wakuu,

Sio lengo langu kufundisha mamlaka husika namna ya utendaji wa majukumu yao wala kuelekeza nini cha kufanya lakini mimi pia sio mwanasiasa, mahusiano yangu na serikali yapo upande wa ulipaji kodi pekee nawapa chao nabaki na changu.

Mapema leo nimeona nami nitoe maoni yangu kuhusu kinachoendelea katika medani za kisiasa na serikali kwa ujumla, kwanini muda mwingi mnamzungumzia JPM tatizo nini? Kwanini msitumie huo muda na nguvu kumpa ushirikiano aliepo madarakani ili kuua mijadala ya kulinganisha uongozi kwamba huyu mbaya huyu mzuri.

Najua JPM alikuwa mtu mbaya kwa makundi fulani ya watu na mkombozi kwa baadhi,nimejaribu kufanya utafiti ninyi watumishi wa umma mnapenda majungu ndio mmekua chanzo cha hizi kelele za kulinganishana,sote tunajua jamaa aliziba mianya ya pesa za chap chap kwaupande mwingine net amount due hazipo vizuri lazima jamaa angeonekana mbaya tu...Wacha jamaa apumzike kibaya kwako kizuri kwa wengine na kizuri kwako kibaya kwa wengine.

Viva Tanzania mama anaupiga mwingi nchi inasonga,vituo vya afya kila mahali.

Ni AIBU kubwa kupambana na MAREHEMU huku ukijua nawe ni marehemu TARAJARI.

Ubadhilifu wa dhahili umeshamiri kwasababu wanaamini mnoko hayupo! Ukiibia Serikali unaonekana mjanja jamii inakusifu.

Viongozi SASA wameamua kujijenga haraka haraka kufidia hasara Kwa kipindi kilichopita.

Miradi binafsi inakuwa Kwa Kasi

Sababu hawana sera zao kuisaidia nchi. Sera ni divide and rule kuwatenganisha Watz ili kuwatawala na kutumbua pesa zao kirahisi.

Hao wanaompenda nao waje wamsifie au kumtetea, wale waliokuwa wanaona ni ibilisi ngoja wampe ukweli wake.

Hata dhalimu aliiba serekalini, alipokuwa akitendea wengine ukatili na kupora haki ya watu kupata viongozi wawatakao, hakujua kuwa iko siku atakuwa marehemu?

Tena wizi mkubwa ulifanyika kipindi cha dikteta

Wanaotaka kuimba nyimbo za kumsifu,na waendelee.Na wanaoona bado wana dukuduku na marehemu nao waendelee kumsimanga.Msiingiliane wala kuoneana gere katika utendaji wenu.
 
Hakuna ukweli hapo,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni jamaa kafanya mengi mazuri.Kama mtu alikufa kama wanavyodai ni uzembe wake mwenyewe V8 ipo speed 180 full light kitamba chekundu hewani unaleta mzaa barabarani utagongwa tu hakuna namna

Hakufanya mazuri bali alitekeleza wajibu wake kiasi fulani, ufahamu kuwa alikuwa analipwa mshahara na sio kujitolea.
 
Ukiona mtu yeyote alimpenda Magufuli au anamtetea basi ujuwe ni mnyonya damu muabudu mizimu na mtu asiyestaarabika wala hajui dunia ya wastaarabu watu wanaishi vipi.
Exactly.
 
Back
Top Bottom