Ndugu yangu Nyalotsi usijali kabisa kwa kuniuliza maswali mengi hata kama yanajirudia. Kimsingi, nipo hapa kupata suluhisho la tatizo lililonisibu muda mrefu sana. Kila maelezo utakayohitaji kwangu utayapata kadri ninavyofahamu. Sasa ningependa kujibu maswali yako kama ifuatavyo:-
Muda mrefu umepita tangu nilipoharisha kwa maana halisi ya kuharisha. Mara kwa mara nimekuwa nikipata choo cha kawaida yaani siyo kigumu wala laini sana. Ni mara chache sana napata choo kigumu kiasi cha kuumia.
Kuna wakati nilifanyiwa culture na walibaini typhoid na aina ya dawa ambayo ingefaa. Nilipata tiba na ilinisaidia. Baada ya wiki kama moja hivi niliendelea kujisikia vibaya. Nilipopima niliambiwa nina amoeba.
Umri wangu ni miaka 45.
Afya yangu kwa ujumla kimwonekano ni nzuri. Kwa kuniona, ni vigumu kubaini kama ndiye mwenye hayo matatizo. Nina haiba nzuri tu labda ni kwa sababu nakula chakula kama kawaida ingawa nateseka na maumivu ya tumbo. Kumbuka pia, nimepima mara kadhaa vidonda vya tumbo na kuambiwa sina kabisa.
Kuhusu kuona minyoo, kwa kweli sijawahi kuona. Choo ninachotumia siyo cha shimo. Hivyo, nimekuwa nikikiona choo mara kwa mara na mara zote sijawahi kuona minyoo.
Kuhusu colonoscopy ningependa kujua undani wa kipimo hicho na ni wapi kinapoweza kufanyika nifanye.
Otherwise, nikushukuru kwa kutenga muda wako wa kufuatilia tatizo langu.