Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tafuta post za mtu anajiita baosita,alitoa tiba yake humu na mimi nimepona..vitunguu swaumu ndo tiba
mungu ni mwema sana, we ulikuwa na tatizo gani mkuu, ni amoeba?
ndio..dawa ya yule jamaa kiboko
siwezi kusema maabara zote ni mbovu lakini things done by lab tech muda mwingine huwa nachanganyikiwa. Tuliwahi letewa majibu ya ccta(mtawa) yuko positive. Kufanya sie wenyewe ni negative na kurudia mara ya pili maabara hiyo hiyo majibu yakawa negative. Naomba uniambie apart from abdominal pain ulishawahi kuharisha? ....Damu? Kukosa hamu ya kula? Kuhisi tumbo limejaa? Kunya mnyoo? Kuhisi kichefuchefu? Kukohoa au kubanwa kifua kama mtu wa asthma? Unakula chakula kiasi gani kwa siku? Kina mchanganyiko? Unakunywa maji mara ngapi kwa siku? Kiasi gani?
Nina tatizo km lako sema nini na mgongo sasa unauma,nahangaika sana,napata choo kinamakamasi,Mara ingine sipati ama napata kidogo,Mara ingine najihisi km nnavidonda njia ya haja,Wakuu,
Yamenikuta mwenzenu tafadhali naomba msaada wa kitabibu.
Ni miezi miwili mfululizo sasa nakunywa dawa za amoeba lakini tatizo lipo palepale. Naendelea kuteseka na maumivu ya tumbo yanayoambatana na gas nyingi na homa na miguu kupata moto nyakati za usiku. Nimekuwa nikijisikia kama nahitaji kwenda haja lakini nikienda naishia kujikamua sana na kupata choo chenye makamasi. Kila nikipima kwenye maabara za hospitali mbalimbali na maabara zinazotoa huduma za vipimo tu, naambiwa aidha nina amoeba au nina ascaris. Baada ya vipimo, hutumia dawa na wakati mwingine dozi mbili kabisa lakini mwisho wa siku, nakaa siku kama moja tu maumivu yanarudi palepale.
Kwa upande wa amoeba, nimetumia dawa karibu zote zinazotajwa na madaktari kuwa ni nzuri including tinidazol, senitidazol, furazol, flagile, (sina uhakika na spelling), n.k. na kwa upande wa minyoo, nimetumia sana dawa aina za albendazol, zentel, combustin, n.k. Ajabu ni kwamba wakati natumia maumivu yanapungua almost yote isipokuwa tu kinachoumiza ni kichefuchefu na mwili kuchoka kutokana na kunywa dawa kali.
Nimejaribu kutumia hata alternative medication ikiwa ni pamoja na kunywa juice ya kitunguu swaumu kama ilivyosgauriwa na mdau mmoja humu JF, lakini hali ipo pale pale. Miaka ya zamani niliugua alcers (vidonda vya tumbo) lakini nilipata tiba fulani mpaka nilipona na nimekuwa nikipima mara kadhaa lakini naambiwa sina vidonda vya tumbo.
Baadhi ya madaktari wamekuwa wakisema kwamba kwa dawa nazokunywa hawaamini kama amoeba huwa haiponi au minyoo haifi. Wanachoamini wao ni kwamba mazingira ninayoishi ndiyo yanayosababisha nipate infections mara kwa mara. Madaktari hao walinishauri mambo kadhaa ya usafi ya kuzingatia. Kutokana na mateso nayopata, nimejitahidi sana kuzingatia masharti hayo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kula vyakula mahotelini, kunywa maji yaliyochemshwa, kujiepusha na maji kuingia kinywani wakati wa kuoga, kutokula matunda na vitu kama kachumbali, n k. Pamoja na hatua hiyo, bado hali ya maumivu ipo na nikipima naambiwa aidha nina amoeba ikiwa kwenye early stage au nina minyoo aina ya ascaris. Kwa upande wa Dar nimetibiwa hospital za Agakhan, Mikocheni, Legency na vituo mvalimbali vya afya. Nikiwa Mwanza nimetibiwa sana Bugando na Sekoture. Mbeya nimetibiwa mara mbili hospitali ya rufaa na hospitali moja ipo eneo la Uyole bahati mbaya sikumbuki jina.
Ndugu zangu na hasa wadau wa jukwaa hili JF Doctor, naomba msaada wenu. Nachotaka kujua ni:-
(1) Je, kuna dawa gani nyingine ya amoeba nayoweza kujaribu ambayo ni ya uhakika katika kutibu amoeba ukiachana na hizo nilizotaja kwa uchache? Au ni tiba gani mbadala ya uhakika nayoweza kupata ili kuondoa kabisa ugonjwa huu?
(2) Kuna dawa za kienyeji baadhi zinatoka Zanzibar zinauzwa pale Kariakoo karibu na stendi ya daladala za Mwenge. Baadhi zimeandikwa kwamba zinatibu aina zote za minyoo including amoeba. Je, ni kweli kwamba amoeba ni minyoo? Kama ni minyoo, je hakuna uwezekano wa diagnosis ya kimaabara kuchanganya interpretation ya amoeba na minyoo ya ascaris? Nauliza hivi kwa sababu isije ikawa wakati mwingine natumia dozi kubwa za amoeba wakati tatizo ni minyoo ya ascaris au kinyume chake?
Wadau naomba msaada wenu wa kitabibu, asante.
Kwa siku ngapi mkuuMkuu kupona kabisa amoeba tumia kwa pamoja dawa zifuatazo. 1. Dawa/ dozi za minyoo - zentel 2.antibiotic - doxycycillin, 3.dozi ya amoeba flagyl 4. Dozi ya amoeba azithromycin. 5.dawa ya minyoo inaitwa yomesan inapatikana shamshudin phamarcy, teremka akiba d,i.t nenda moja kwa moja morogoro road km unaenda posta uliza apolo dispensary uliza hiyo phamacy.. Unaweza pia kutumia panadol na vitamin b. Kumbuka tumia dawa hizi kwa pamoja