Kwanini siponi Amoeba? Je, kuna uhusiano gani kati ya Amoeba na Minyoo ya Ascaris?

Kwanini siponi Amoeba? Je, kuna uhusiano gani kati ya Amoeba na Minyoo ya Ascaris?

tafuta post za mtu anajiita baosita,alitoa tiba yake humu na mimi nimepona..vitunguu swaumu ndo tiba
 
ndio..dawa ya yule jamaa kiboko

asante kwa ushuhuda, mkuu, wacha na sisi tuitumie. umetumia mara moja tu au unarudia rudia mara kadhaa. mi nilitumia mara tatu sijapona na inavochefua nikaona ntasababisha magonjwa mengine bure
 
Dumelambegu

Ulipona hii Amoeba, manake hujatupa mrejesho ni tiba gani ilikusaidia.
 
Last edited by a moderator:
siwezi kusema maabara zote ni mbovu lakini things done by lab tech muda mwingine huwa nachanganyikiwa. Tuliwahi letewa majibu ya ccta(mtawa) yuko positive. Kufanya sie wenyewe ni negative na kurudia mara ya pili maabara hiyo hiyo majibu yakawa negative. Naomba uniambie apart from abdominal pain ulishawahi kuharisha? ....Damu? Kukosa hamu ya kula? Kuhisi tumbo limejaa? Kunya mnyoo? Kuhisi kichefuchefu? Kukohoa au kubanwa kifua kama mtu wa asthma? Unakula chakula kiasi gani kwa siku? Kina mchanganyiko? Unakunywa maji mara ngapi kwa siku? Kiasi gani?

mkuu hizo dalili ulizotaja ninazo na nimeenda kupima hospital mpaka kiasi cha kupigwa x-rays naambiwa sina matatizo ya moyo wala kifua. Nikapewa dawa za kusafisha mapafu lakini bado tatizo ni lile lile. pia kwa miaka 3 mfululizo nimekuwa mtu ambaye sina hamu ya kula kabisa. kasoro siharishi
 
Nimepata elimu ya kutosha kwa maelezo ya wataalamu humu na shuhuda za wagonjwa wa amoeba Asanten saana,mbarikiwe wana jf nami nina shida hii mpaka nmeshindwa kusoma.nitaanza kufanyia kazi ushauri wa dawa,tiba mbadala hizo na mengine yote...viva jf
 
Dumelambegu ulitumia Dawa gani kutibu vdonda vya tumbo?
Nisaidie aisee
 
Naam nimewasikiliza ote wadau ushauri vado nimzuri tu samahani kwa kiswahili changu mana mimi simswahili, tatizo ilo bado linanisumbua ata mm kwaio dawa upatw mganga wakienyeji akupe majimajani flani upige mwino mana unapo chelewa ata mapafu yataharibika
 
Saidieni wagonjwa ndg zangu madaktari ikiwezekana wasikiana na mgonjwa huyu umuite mzungunze Ana kwa ana.


Wengi tunaumwa mno
 
Wakuu,

Yamenikuta mwenzenu tafadhali naomba msaada wa kitabibu.

Ni miezi miwili mfululizo sasa nakunywa dawa za amoeba lakini tatizo lipo palepale. Naendelea kuteseka na maumivu ya tumbo yanayoambatana na gas nyingi na homa na miguu kupata moto nyakati za usiku. Nimekuwa nikijisikia kama nahitaji kwenda haja lakini nikienda naishia kujikamua sana na kupata choo chenye makamasi. Kila nikipima kwenye maabara za hospitali mbalimbali na maabara zinazotoa huduma za vipimo tu, naambiwa aidha nina amoeba au nina ascaris. Baada ya vipimo, hutumia dawa na wakati mwingine dozi mbili kabisa lakini mwisho wa siku, nakaa siku kama moja tu maumivu yanarudi palepale.

Kwa upande wa amoeba, nimetumia dawa karibu zote zinazotajwa na madaktari kuwa ni nzuri including tinidazol, senitidazol, furazol, flagile, (sina uhakika na spelling), n.k. na kwa upande wa minyoo, nimetumia sana dawa aina za albendazol, zentel, combustin, n.k. Ajabu ni kwamba wakati natumia maumivu yanapungua almost yote isipokuwa tu kinachoumiza ni kichefuchefu na mwili kuchoka kutokana na kunywa dawa kali.

Nimejaribu kutumia hata alternative medication ikiwa ni pamoja na kunywa juice ya kitunguu swaumu kama ilivyosgauriwa na mdau mmoja humu JF, lakini hali ipo pale pale. Miaka ya zamani niliugua alcers (vidonda vya tumbo) lakini nilipata tiba fulani mpaka nilipona na nimekuwa nikipima mara kadhaa lakini naambiwa sina vidonda vya tumbo.

Baadhi ya madaktari wamekuwa wakisema kwamba kwa dawa nazokunywa hawaamini kama amoeba huwa haiponi au minyoo haifi. Wanachoamini wao ni kwamba mazingira ninayoishi ndiyo yanayosababisha nipate infections mara kwa mara. Madaktari hao walinishauri mambo kadhaa ya usafi ya kuzingatia. Kutokana na mateso nayopata, nimejitahidi sana kuzingatia masharti hayo, ikiwa ni pamoja na kuepuka kula vyakula mahotelini, kunywa maji yaliyochemshwa, kujiepusha na maji kuingia kinywani wakati wa kuoga, kutokula matunda na vitu kama kachumbali, n k. Pamoja na hatua hiyo, bado hali ya maumivu ipo na nikipima naambiwa aidha nina amoeba ikiwa kwenye early stage au nina minyoo aina ya ascaris. Kwa upande wa Dar nimetibiwa hospital za Agakhan, Mikocheni, Legency na vituo mvalimbali vya afya. Nikiwa Mwanza nimetibiwa sana Bugando na Sekoture. Mbeya nimetibiwa mara mbili hospitali ya rufaa na hospitali moja ipo eneo la Uyole bahati mbaya sikumbuki jina.

Ndugu zangu na hasa wadau wa jukwaa hili JF Doctor, naomba msaada wenu. Nachotaka kujua ni:-

(1) Je, kuna dawa gani nyingine ya amoeba nayoweza kujaribu ambayo ni ya uhakika katika kutibu amoeba ukiachana na hizo nilizotaja kwa uchache? Au ni tiba gani mbadala ya uhakika nayoweza kupata ili kuondoa kabisa ugonjwa huu?

(2) Kuna dawa za kienyeji baadhi zinatoka Zanzibar zinauzwa pale Kariakoo karibu na stendi ya daladala za Mwenge. Baadhi zimeandikwa kwamba zinatibu aina zote za minyoo including amoeba. Je, ni kweli kwamba amoeba ni minyoo? Kama ni minyoo, je hakuna uwezekano wa diagnosis ya kimaabara kuchanganya interpretation ya amoeba na minyoo ya ascaris? Nauliza hivi kwa sababu isije ikawa wakati mwingine natumia dozi kubwa za amoeba wakati tatizo ni minyoo ya ascaris au kinyume chake?

Wadau naomba msaada wenu wa kitabibu, asante.
Nina tatizo km lako sema nini na mgongo sasa unauma,nahangaika sana,napata choo kinamakamasi,Mara ingine sipati ama napata kidogo,Mara ingine najihisi km nnavidonda njia ya haja,
Bado napambana,nimeamua kutafuta mitishamba,
 
Mkuu kupona kabisa amoeba tumia kwa pamoja dawa zifuatazo. 1. Dawa/ dozi za minyoo - zentel 2.antibiotic - doxycycillin, 3.dozi ya amoeba flagyl 4. Dozi ya amoeba azithromycin. 5.dawa ya minyoo inaitwa yomesan inapatikana shamshudin phamarcy, teremka akiba d,i.t nenda moja kwa moja morogoro road km unaenda posta uliza apolo dispensary uliza hiyo phamacy.. Unaweza pia kutumia panadol na vitamin b. Kumbuka tumia dawa hizi kwa pamoja
Kwa siku ngapi mkuu
 
Back
Top Bottom