Kwanini sisi wanaume huwa tunawaacha wanawake wanaotupenda kwa dhati bila kutumia nguvu nyingi?

Kwanini sisi wanaume huwa tunawaacha wanawake wanaotupenda kwa dhati bila kutumia nguvu nyingi?

qarem

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2018
Posts
626
Reaction score
825
Eeeh bwana eeh wasalaaam.

Hebu wajuba njooni tutoe sababu za msingi zinazofanya tunawakimbia akina dada wanatupenda wao wenyewe bila kutumia nguvu nyingi.

Mimi binafsi nimekutana na kesi nyingi sana huwa nakinahiwa kabisa na ile hamu ya kuwa na mdada alienipenda bila mimi either kumtongoza or ile inaitwa sukuma mleviii kitu imo.

Katika kumbukumbu za hivi karibuni kuna mdada alikua akinipenda mno kutoka kanda ya ziwa tokea tulipokutana 823 kj msange tabora mujibu wa sheria.

Hivyo hivi karibuni kwakua still tulikua na mawasiliano alikuja kufunguka yeye mwenyewe,nilimkubalia ila sikua na ileee hamu haswaaa kama vile nikimtongoza mwenyewe mdada.

Basi bwana penzi lile halikufika hata week mimi nilimpotezea yule mdada wa watu mpaka leo nikikumbuka namuonea huruma,alikua akinipenda sana halafu mimi kwakua nilikua simkubali nilikua namchukulia poa,mpaka nilipokuja kutowasiliana nae tena mpaka leo hii.

Hebu tutoeni sababu za msingi ni kwanini inatokeaga hivii,mimi binafsi sipendi tu mdada ajirahisishe sana ndo mana huwa napoteza appetites.

Karibuni uzi uko tayari

NB: Mtanisamehe sipo vizuri katika ku narrate visa/habarii kikubwa content imeonekana inahitaji nini.
 
Hakuna mwanamke anaempenda mwanaume kwa dhati,ukiona mwanamke anakwambia anakupenda jua
1.kwako Kuna maslahi Fulani ndiyo anayapenda sio wewe.
2.ameshapiga tochi mbele kwamba mwishowe Kuna kitu atakuja faidika kwako,kinyume na hapo,hakuna mwanamke anaempenda mwanamme.
Hutaki unaacha au chunguza kwa makini.
 
Iliwahi kunitokea hata mimi. Kuna mdada alinipenda ile kinoma sema mimi sikuwa hata na ile chembe ya kumpenda yeye na nilimueleza ninavyojisikia kwake ila alilazimisha. Alitia huruma sana ikabidi nimkubalie kichwa upande nimsogezee siku. Ile tuna week ya pili tu akaanza kung'ang'ana kutaka nikajitambulishe kwao na yeye kwetu, ukicheki sikuwa tayari kuoa. Sikufikiria mara mbili kumwambia 'kwanzia sasa tumeachana'.
 
Acha utani mkuu.

Kwa hiyo hata huyu shemeji yenu wa hapa JF kila siku ananiambia halali bila kuniona na kuniskia ananichora?
 
Iliwahi kunitokea hata mimi. Kuna mdada alinipenda ile kinoma sema mimi sikuwa hata na ile chembe ya kumpenda yeye na nilimueleza ninavyojisikia kwake ila alilazimisha. Alitia huruma sana ikabidi nimkubalie kichwa upande nimsogezee siku. Ile tuna week ya pili tu akaanza kung'ang'ana kutaka nikajitambulishe kwao na yeye kwetu, ukicheki sikuwa tayari kuoa. Sikufikiria mara mbili kumwambia 'kwanzia sasa tumeachana'.
Ila Mkuu tunachokifanya sio poa ni unyanyasaji wa kijinsia!!
 
Mbona boss Mimi sikua na chochotee..! Sometimes upendo upo tatizo linakuja hatujui tunataka nini katika mapenz
Hakuna mwanamke anaempenda mwanaume kwa dhati,ukiona mwanamke anakwambia anakupenda jua
1.kwako Kuna maslahi Fulani ndiyo anayapenda sio wewe.
2.ameshapiga tochi mbele kwamba mwishowe Kuna kitu atakuja faidika kwako,kinyume na hapo,hakuna mwanamke anaempenda mwanamme.
Hutaki unaacha au chunguza kwa makini.
 
Namchokaga fasta demu anaeonesha kunijali sana
Hao mademu wanakujali kwenye mambo gani?

Maana wanaume wanatujali kwenye usaidizi.

Mwanamke akusaidie kukujali kwenye biashara umchoke?.

Mwanamke akujali kwenye kukupigia nguo pasi au kukuandalia chakula kizuri umchoke?.

Mwanamke akujali kuwakaribisha ndugu vizuri au wageni wajapo nyumbani nako umchoke?
 
Ila Mkuu tunachokifanya sio poa ni unyanyasaji wa kijinsia!!
Sifikiri kama ni unyanyasaji. Kumpenda mtu sio kosa ila shida ni pale huyo unaempenda anakufeel kama wewe unavyo mfeel? Kingine ukiangalia wengine wanafanya hivyo ili kuonyeshana mtaani au anamalengo mengine ambayo sio rahisi kuyajua kwa haraka.
 
Back
Top Bottom