Kwanini Somo la Hisabati bado ni changamoto?

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Wanafunzi wa Darasa la Saba wamemaliza Mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi, lkn ktk tathimini ya haraka haraka wanafunzi wengi wanalalamika kuwa mtihani wa somo la Hisabati ulikuwa mgumu sana.

Swali ambalo nimejiuliza:

1. Kuna tatizo gani ktk somo la Hisabati kwa Elimu ya Tanzania?

2. Ni somo la Hisabati ndio Gumu au Wanao tunga mitihani ya somo la Hesabati ndio wanafanya somo lionekane kuwa gumu?
nadhani kuna haja kwa mamlaka ya Elimu kutazama kwa makini ili ibainike.

Tusitunge mitihani kama vile tunawakomoa wanafunzi. tuwapime kwa viwango vyao na kwa kulingana na upeo wao wa akili tusiwape mitihani ambayo iko juu ya uwezo wao.

Kwani kuna ulazima wa kutunga maswali "complicated"? kwa maoni yangu sioni kama kuna ulazima.
 
Hivi mmewahi kujiuliza kwamba mtu aliyepata division 4 ya point 28 somo la BASIC MATHS alipata F akaenda kusoma ualimu wa GRADE A anapata training ya kufundisha masomo yoote ya PRIMARY SCHOOL anakuja kuwa mwalimu wa hesabu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

Nadhani sera ya elimu iangalie hapo kwanza waalimu wa hesabu kwa level zoote hasa shule za misingi wawe wamefaulu hesabu au kuwe na utaratibu wa ku train waalimu wa shule za misingi kufundisha masomo walioyabobea kama sekondari ilivyo.

Mwanafunzi yyt humudu somo katika hatua za MSINGI kabla ya kufika sekondari.

Nashauri sera iangaliwe upya.
 
Sahihi.

Lakini pia vipi kuhusu utungaji wa mtihani wenyewe wa Hasabati?

Je, unazingatia viwango na uwezo wa watoto wa darasa la saba?

Sio kwamba mtihani unao tungwa ni mgumu sana!
 
Nadhani waziri wa Elipo Prof Ndalichako pamoja na wataalamu wa elimu wanapaswa wafanye utafiti.

lkn pia NECTA wanapaswa watunge mtihani kwa lengo la kupima uwezo wa watoto sio kukomoa.

Ukilimganisha Mtihani wa Hesabu kwa shule za kenya na Uganda, Mtihani wa Tanzania very complicated, hii imekuwa kasumba kwa watungaji wetu wa mtihani.
 
Kwa ujumla wanafunzi wa sasa wengi hawapendi hesabu na masomo ya sayansi...
Wanafunzi hawapendi hesabu sababu waalimu wa sasa maarifa (skills) za ufundishaji hazimvutii mwanafunzi kupenda hisabati

Na somo lenyewe huwezi kuanza kulipenda na kulimudu katika hatua za mbele. Lazima uwe na msingi imara
 
Mimi nilimkubali Mwalimu Nyerere kuanzisha UPE.

Walichukua wanafunzi wakali wa hesabu shule ya msingi wakawa walimu baadae zimekuja hizi sekondari za mwendokasi watu wakaanza kashfa nzito sana dhidi ya walimu hawa wa UPE.

Mimi hadi leo nakumbuka mwalimu wangu alinifundisha simultaneous equation nikiwa darasa la saba tena kijijini sana.Nilivyoenda kidato cha kwanza nikayakuta wenzangu wakawa wanaamini niliwahi kusoma sekondari.Wakati hata tuition tu ya pre form one sikuwahi kusoma
Hivi mmewahi kujiuliza kwamba mtu aliyepata division 4 ya point 28 somo la BASIC MATHS alipata F akaenda kusoma ualimu wa GRADE...
 
Wanafunzi wa Darasa la Saba wamemaliza Mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi, lkn ktk tathimini ya haraka haraka wanafunzi wengi wanalalamika kuwa mtihani wa somo la Hisabati ulikuwa mgumu sana.

Swali ambalo nimejiuliza:

1. Kuna tatizo gani ktk somo la Hisabati kwa Elimu ya Tanzania?

2. Ni somo la Hisabati ndio Gumu au Wanao tunga mitihani ya somo la Hesabati ndio wanafanya somo lionekane kuwa gumu?
nadhani kuna haja kwa mamlaka ya Elimu kutazama kwa makini ili ibainike.

Tusitunge mitihani kama vile tunawakomoa wanafunzi. tuwapime kwa viwango vyao na kwa kulingana na upeo wao wa akili tusiwape mitihani ambayo iko juu ya uwezo wao.

Kwani kuna ulazima wa kutunga maswali "complicated"? kwa maoni yangu sioni kama kuna ulazima.
Kiongozi math yaonekana ngum pia ni sababu walim weng wako shallow kweny ufundshaj
 
Hivi mmewahi kujiuliza kwamba mtu aliyepata division 4 ya point 28 somo la BASIC MATHS alipata F akaenda kusoma ualimu wa GRADE A anapata training ya kufundisha masomo yoote ya PRIMARY SCHOOL anakuja kuwa mwalimu wa hesabu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

Nadhani sera ya elimu iangalie hapo kwanza waalimu wa hesabu kwa level zoote hasa shule za misingi wawe wamefaulu hesabu au kuwe na utaratibu wa ku train waalimu wa shule za misingi kufundisha masomo walioyabobea kama sekondari ilivyo.

Mwanafunzi yyt humudu somo katika hatua za MSINGI kabla ya kufika sekondari.

Nashauri sera iangaliwe upya.
Fact mkuu maana sio hesab TU all science subject bado wanaend Soma wat walopata lower class
 
Hivi mmewahi kujiuliza kwamba mtu aliyepata division 4 ya point 28 somo la BASIC MATHS alipata F akaenda kusoma ualimu wa GRADE A anapata training ya kufundisha masomo yoote ya PRIMARY SCHOOL anakuja kuwa mwalimu wa hesabu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.

Nadhani sera ya elimu iangalie hapo kwanza waalimu wa hesabu kwa level zoote hasa shule za misingi wawe wamefaulu hesabu au kuwe na utaratibu wa ku train waalimu wa shule za misingi kufundisha masomo walioyabobea kama sekondari ilivyo.

Mwanafunzi yyt humudu somo katika hatua za MSINGI kabla ya kufika sekondari.

Nashauri sera iangaliwe upya.
Sasa, mbona miaka ya 90 kurudi nyumba walimu waliotufundisha walipata daraja la nne hilohilo na hali haikuwa mbaya kama miaka hii? Viwango vya ufaulu kwa waliokwenda kujifunza ualimu ngazi ya cheti ni kilekile toka zama hizo hadi leo. Tena kadiri miaka inavyosonga, ndipo unaweza kukuta mpaka division two na three wapo vyuo hivi vya ualimu ngazi ya vyeti. Siku hizi mwanao akipata four chakavu, kupata chuo cha serikali ni mtihani.

Kwa taarifa yako, ualimu wa shule ya msingi wala hauhitaji division one. Ukweli ni kwamba elimu imeshuka, la saba wa mwaka 1985, si la saba wa leo. Form four wa mwaka 1980, si form four wa leo. Kwahiyo, japo wengi wa mtazamo wako mtabisha, lakini amini usiamini, mwalimu wa shule ya msingi wa miaka ya 80 hadi 90 (pamoja alikuwa division four) alikuwa mzuri kuliko mwalimu wa sasa mwenye shahada(digrii). Yani chukua fresh graduate wa leo, mpeleke shule ya msingi , anapigwa na yule division four miaka tajwa hapo juu. Mimi sitoshangaa graduate wa leo akishindwa kutafuta KIVIMBE cha duara.
 
Sasa, mbona miaka ya 90 kurudi nyumba walimu waliotufundisha walipata daraja la nne hilohilo na hali haikuwa mbaya kama miaka hii? Viwango vya ufaulu kwa waliokwenda kujifunza ualimu ngazi ya cheti ni kilekile toka zama hizo hadi leo. Tena kadiri miaka inavyosonga, ndipo unaweza kukuta mpaka division two na three wapo vyuo hivi vya ualimu ngazi ya vyeti.

Kwa taarifa yako, ualimu wa shule ya msingi wala hauhitaji division one. Ukweli ni kwamba elimu imeshuka, la saba wa mwaka 1985, si la saba wa leo. Form four wa mwaka 1980, si form four wa leo. Kwahiyo, japo wengi wa mtazamo wako mtabisha, lakini amini usiamini, mwalimu wa shule ya msingi wa miaka ya 80 hadi 90 (pamoja alikuwa division four) alikuwa mzuri kuliko mwalimu wa sasa mwenye shahada(digrii). Yani chukua fresh graduate wa leo, mpeleke shule ya msingi , anapigwa na yule division four miaka tajwa hapo juu. Mimi sitoshangaa graduate wa leo akishindwa kutafuta KIVIMBE cha duara.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa na chache nakataa kukubaliwa. Waalimu wa zamani wale wa UPE waliokuwa wameishia darasa la 5 au la 7 au la nane enzi hizo walikuwa ni waalimu wenye ufaulu wa juu kwenye mitihani yao ya darasa la 5 au la 7 au la 8. Nakukumbusha zamani kuferi la 7 au la 8 kulikuwa sio sana ila kukosa nafasi kwenda form one ndo kulikuwepo. Hivyo hawa waalimu wa UPE hawakuwa vilaza ila walikuwa waalimu VIPANGA MACHACHARI wa HISABATI ni kwamba walikosa nafasi kutokana na shule za sekondari kuwa chache na uwezo mdogo kudahili woote waliofaulu.
Wale waalimu wa UPE akikufundisha hesabu mbinu anazotumia huwezi linganisha na hawa wa sasa. Mtu amepata division 4 ya 28 B.MATHS kapata F ya form 4 atafundishaje HISABATI shule ya msingi. Hapo ndipo msingi mbovu unajengwa
 
Sijui ulichokataa ni kipi. Mimi ninaona unazungumza hayohayo niliyoyaandika. Kwanza, si walimu wote walitoka UPE. UPE ilikuwa programu maalumu kujaza pengo la walimu baada ya kuwa na upungufu. Na kama mwenyewe unavyothibitisha, bado walikuwa wazuri (kwa kulinganisha na wahitimu wa sasa). Hii ndo hoja yangu,japo mimi nilikuwa najibu hoja ya kidato cha nne na division four ya 28 kama ulivyowasilisha hapo juu.

Hata hivyo, suala la ubora wa elimu ni tata, linatazamwa kwa mengi. Hapa tunalinganisha tu vya leo na vya jana. Tunaona kwamba kule nyuma kulikuwa afadhali. Ukweli ni kwamba elimu imekuwa ikishuka toka tulipoachiwa nchi na mkoloni, yani wa jana ana nafuu kuliko wa leo.
 
Pamoja na kukosekana kwa walimu weledi ktk somo la Hisabati lkn kwa maoni yangu Hesabu za Darasa la Saba walimu wengi wanazimudu ila naona tatizo lipo kwa NECTA, Baraza la Mitihani linatunga Mitihani ya luwakomoa watoto wa Darasa la Saba badala ya kupima uwezo wao.
Mtoto wa Darasa la Saba hawezi kumtungia mtihani sawa na wa form 4 au form 2.
NECTA wanapaswa watunge mitihani kulingana na uwezo wa watoto wa Darasa la 7. mtihani uwe standard kulingana na maarifa yao/umri wao.
 
Back
Top Bottom