Wanafunzi wa Darasa la Saba wamemaliza Mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi, lkn ktk tathimini ya haraka haraka wanafunzi wengi wanalalamika kuwa mtihani wa somo la Hisabati ulikuwa mgumu sana.
Swali ambalo nimejiuliza:
1. Kuna tatizo gani ktk somo la Hisabati kwa Elimu ya Tanzania?
2. Ni somo la Hisabati ndio Gumu au Wanao tunga mitihani ya somo la Hesabati ndio wanafanya somo lionekane kuwa gumu?
nadhani kuna haja kwa mamlaka ya Elimu kutazama kwa makini ili ibainike.
Tusitunge mitihani kama vile tunawakomoa wanafunzi. tuwapime kwa viwango vyao na kwa kulingana na upeo wao wa akili tusiwape mitihani ambayo iko juu ya uwezo wao.
Kwani kuna ulazima wa kutunga maswali "complicated"? kwa maoni yangu sioni kama kuna ulazima.
Mkuu; Naomba nianze hv: Nyumba inakuwa imara kutokana na uimara wa msingi wake. Somo la Hisabati linajengwa tangu mtoto akiwa nyumbani, then chekechea, halafu darasa la kwanza n.k. Kwa hiyo kama NYUMBANI mtoto hajapata exposure ya hesabu ni wazi Mwl. wa chekechea ana kazi ngumu sana. Na kama Wazazi wa Mtoto nao watasema na Kuamini kwamba Hesabu ni ngumu na hawamtii moyo (Encourage) mtoto wao kupenda Hisabati basi ni mlolongo unaendelea hadi chuo kikuu. Watoa Mitihani wanazingatia sana Syllabus na pengine kuna kitu kinaitwa
Moderation. Maswali yanayoulizwa yanakuwa yamepitiwa tena na kurekebishwa kiwango cha kila Mwanafunzi ALIYEKUWA MSIKIVU kwa Mwl. wake anayamudu. Ni ukweli usiopingika (Hata ww ni shahidi) Mitihani ya shuleni ile ya Kumaliza Muhula
Terminal exams au
Mock huwa ni migumu zaidi ya ile ya Kitaifa.
Sasa, kwa vile Msingi wa Somo la Hisabati kwa mwanafunzi tangu mwanzoni ni Mbovu na ameaminishwa kuwa Hisabati ni Ngumu tutegemee nini hapo? Kumbuka hata watunga mitihani nao ni wazazi na pengine wanao watoto waliofanya Mtihani huo wa Hisabati ambao wameutunga.
Tusilaumu Watoto, Waalimu, Watunga mitihani peke yao Bali tuanzie HASA HASA kwa sisi wazazi ambao hatujali kufuatilia daftari la Hisabati (
IKiwa ni pamoja na masomo mengine) ya mtoto na MBAYA ZAIDI tunawasikiliza/Tunawadekeza watoto wanapodai Hisabati ni ngumu. Mitihani haitoki nje ya kile Mwanafunzi alichofundishwa darasani -Never. Sasa kama mtoto alishaaminishwa kwamba Hisabati ni ngumu tutegemee nini? Utakapomwuliza habari ya Mtihani Atakujibu - Hisabati ilikuwa Ngumu. Tukumbuke Hisabati ndio mambo yote- Hakuna Shule, Chuo au Course yeyote ambayo Hisabati haitatakiwa kwa namna moja au nyingine. Kwa hiyo Tupende-Tusipende hatuna budi kujikita kwenye kuipend na kuifahamu Hisabati. (
By the way, mm co Mwl.) lakini naipenda Hisabati.