munisijo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 1,126
- 942
Wakuu
Baada ya kupata bahati ya kuwemo katika magari aina tofauti tofauti, makubwa na madogo lakini kubahatika kuendesha umbali mrefu kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kitu kimoja nimekuwa nikijiuliza, ni kwa nini magari ''karibia'' yanaonesha uwezo wa kwenda kasi kufikia mwendo wa 180 km/h?
Nilichogundua, mwendo kasi wa 180 km/h ni mkubwa sana sana sana, haufikiki, ni hatari na sio halisi hasa kwa aina ya magari yetu mengi ambayo ni mtumba huku barabara zetu nazo zikiwa sio rafiki.
Kwa mfano, magari ya cc 900 mpaka 2000cc haya kuwekewa mwendo kasi wa 180 km/h ni sahihi? Kwanini wasingeweka tu mfano 140 km/h? Hebu tuangalie uhalisia, katika mazingira yoyote yenye cc chini ya 1500 inaweza kweli kufika mwendo kasi wa let say 160km/h? Binafsi sidhani. Kwa gari maalumu za kwenda kasi na safari ndefu, ama zenye cc zaidi ya 2500 uwezekano unaweza kuwepo lakini kwa hizi nyingine, nahisi watengenezaji wanatulipisha gharama kubwa kwa kitu ambacho hakipo ama kwa kifupi wanatuibia.
Nini mtazamo wako?