Mkuu ukiweka steling kati, matatizo yanakua mengi kuliko faida,
1) mirrors zote zinakua na issue, kwa mfumo wa TZ kuna sehemu ubavuni mwa gari kushoto, huwezi kumuona kwa kupitia kioo cha kushoto (blindspot), ukisogea katikati maana yake na kioo cha kulia kitakua na changamoto. kioo cha kati pia hutaweza kukitumia maana kitakua juu ya kichwa chako.
2) utapoteza siti ya abiria mmoja, maana nafasi itayobaki kulia au kushoto haitofaa kwa mtu mzima kukaa.
3) Steeling inamakorokoro yake yanayosaidia kuifanya iwe nyepesi, sasa kwa kawaida nafasi ya mbele kati inachukuliwa na engine, sasa huoni km itakua ni changamoto kuweka na makorokoro ya steeling mbele kati?
4) huoni pia itakua changamoto kuingia na kutoka kwenye gari? imagine tabu anayoipata abiria wa siti ya nyuma kati kwenye kuingia na kutoka, sasa jaribu kumfikiria dreva atataabika kiasi gani.
5) ukitaka kuchungulia kama mbele kuna gari?