Kwanini sukari imekuwa ghali saaana wakati viwanda vipo nchini vya kutosha?

skfull

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
2,944
Reaction score
2,383
Ndugu zangu wana jamvi wenzanzangu, wtz wenzanzangu, habari za asubuhi,, nitumsini langu mko poo

Leo napenda tujadili sukari kidogo, niliwahi kusikia ni marufuku kuagiza sukari nje ili kulinda maslahi ya mlaji Hilo ni tamko la serikali kupitia waziri mkuu na waziri mwenye dhamana pia aliekuwa rais wa awamu ya tano.

Sasa juzi kati hapa mama ametoa tamko kuwa sukari iingie toka Uganda je mama yeye anasimamia maslahi ya nani ikiwa wenzake walisimamia maslahi ya mwekezaji?

Hapa napata tabu katika suala moja tu kwanini sisikii maslahi ya mlaji yakigusiwa? Kwa mfano sukari imekuwa ikipanda Bei juu Sana bila kukali mlaji na serikali ipo kimya ila tumekuwa mashahidi kuwa ukinunua sukari nje ya nchi yetu Bei inakua angalau kidogo ahueni kwa mlaji.

Sasa hoja yangu ni kwamba kwanini sukari imekuwa ghali saaana wakati viwanda vipo nchini vya kutosha halafu kwanini serikali haina tamko lolote kuzungumzia Bei ya sukari kabisa?

Je, kwanini serikali isirudishe viwanda vyote vya sukari mikononi mwake na ikafanya kazi yenyewe ya uzalishaji na kuuza ili kusimamia uzalishaji na uuzwaji, mapato kwa ujumla ili kujua ni wapi panakosewa hadi sukari kuuzwa Bei juu kiasi hichi?

Maana nakumbuka upandaji wa Bei ya sukari unakuwa ni wa kihuni kabisa haufuati utaratibu hata kidogo na ikipanda serikali haikemei kabisa kurudi ilipotoka Kama itapanda elf moja juu basi serikali ikiongea kidogo haiondoki elfu moja inaondoka mia moja tu, Nini maana yake hasa au serikali haina mpango wa kutetea maslahi ya mlaji wa sukari?
 
Unalijua jalala, dumping? . Sehemu kubwa ya sukari toka nje imeharibika expired.

Ni uamuzi wa ajabu kuchezea afya walaji.

Kuwalinda wawekezaji wa ndani ajira na kodi. Tunapaswa kuwa na Sera endelevu na sio hisia mzuka kiongozi. Viwanda vilivyopo vyote vina endelea na upanuzi kuongeza uzalishaji, Kuna ujenzi wa viwanda vipya na mashamba mapya mfano Bagamoyo Bakresa. Ni uwekezaji mkubwa wa pesa nyingi.Sio mtaji wa ndani pekee.

Hitaji la Katiba Bora lipo tuwe na taasis na mifumo imara.
 
sababu tunalinda viwanda vyetu hata iwe kilo 1 sh 5000 sisi hatutaagiza sukari nje tunalinda viwanda vyetu hata mwananchi ashindwe kununua sukari lakini tunalinda viwanda vyetu huu msemo wanao sana watanzania bila kijifikiria yeye mwenye au kumfikiria mtu mwingine
 
Unalijua jalala, dumping . Sehemu kubwa ya sukari toka nje imeharibika expired.

Ni uamuzi wa ajabu kuchezea afya walaji.

Kuwalinda wawekezaji wa ndani ajira na kodi. Tunapaswa kuwa na Sera endelevu na sio hisia mzuka kiongozi. Viwanda vilivyopo vyote vina endelea na upanuzi kuongeza uzalishaji, Kuna ujenzi wa viwanda vipya na mashamba mapya mfano Bagamoyo Bakresa. Ni uwekezaji mkubwa wa pesa nyingi.Sio mtaji wa ndani pekee.

Hitaji la Katiba Bora lipo tuwe na taasis na mifumo imara.
Ni kweli kabisa maana naona suala la sukari limekuwa ni Jambo la hisani za viongozi na sio sehemu ya wajibu wao viwanda vilivyopo nasema vinatosha Kama ikiwa vitafanya kazi zake ipasavyo lakini nilisikia Kuna wakati miwa hukatiwa chini na kuteketezwa wakati uhitaji wa sukari upo kwa walaji, inaonekana viwanda vinatengeneza sukari kidogo maksudi halafu wanaficha maghalani ili waje kuuza Bei wanayotaka na hili viongozi wanalijua vizuri na wamefumba macho,,, ki ukweli Kama unavyosema katiba mpya ndiyo muarubaini wa hili maana itaweza kuwekwa mipaka kwa wazalishaji walaji na wasimamizi kila mtu atapewa maslahi yake ipasavyo
 
sababu tunalinda viwanda vyetu hata iwe kilo 1 sh 5000 sisi hatutaagiza sukari nje tunalinda viwanda vyetu hata mwananchi ashindwe kununua sukari lakini tunalinda viwanda vyetu huu msemo wanao sana watanzania bila kijifikiria yeye mwenye au kumfikiria mtu mwingine
Ndiyo kitu kinanipa wakati mgumu kuwa hivi unaweza kumlinda dakitari hata wagonjwa wakifa haikuhusu maana unalinda dakitari? Sasa hii kulinda viwanda vyetu na wawekezaji wetu wakati wameshindwa kazi yao Ina maana gani?
 
Ndugu zangu wana jamvi wenzanzangu, wtz wenzanzangu, habari za asubuhi,, nitumsini langu mko poo

Leo napenda tujadili sukari kidogo, niliwahi kusikia ni marufuku kuagiza sukari nje ili kulinda maslahi ya mlaji Hilo ni tamko la serikali kupitia waziri mkuu na waziri mwenye dhamana pia aliekuwa rais wa awamu ya tano.

Sasa juzi kati hapa mama ametoa tamko kuwa sukari iingie toka Uganda je mama yeye anasimamia maslahi ya nani ikiwa wenzake walisimamia maslahi ya mwekezaji?

Hapa napata tabu katika suala moja tu kwanini sisikii maslahi ya mlaji yakigusiwa? Kwa mfano sukari imekuwa ikipanda Bei juu Sana bila kukali mlaji na serikali ipo kimya ila tumekuwa mashahidi kuwa ukinunua sukari nje ya nchi yetu Bei inakua angalau kidogo ahueni kwa mlaji.

Sasa hoja yangu ni kwamba kwanini sukari imekuwa ghali saaana wakati viwanda vipo nchini vya kutosha halafu kwanini serikali haina tamko lolote kuzungumzia Bei ya sukari kabisa?

Je, kwanini serikali isirudishe viwanda vyote vya sukari mikononi mwake na ikafanya kazi yenyewe ya uzalishaji na kuuza ili kusimamia uzalishaji na uuzwaji, mapato kwa ujumla ili kujua ni wapi panakosewa hadi sukari kuuzwa Bei juu kiasi hichi?

Maana nakumbuka upandaji wa Bei ya sukari unakuwa ni wa kihuni kabisa haufuati utaratibu hata kidogo na ikipanda serikali haikemei kabisa kurudi ilipotoka Kama itapanda elf moja juu basi serikali ikiongea kidogo haiondoki elfu moja inaondoka mia moja tu, Nini maana yake hasa au serikali haina mpango wa kutetea maslahi ya mlaji wa sukari?
Inshu sio kuwa na idadi kubwa ya viwanda bali , ni uzarishaji unatosha?!!uzalishaji wa sukari kwa viwanda vyote vinne ni kama tani 320, 000 kwa mwaka, wakati mahitaji halisi kwa mwaka ni tani zaidi ya 580, 000!!!unadhania huo upungufu utajazwa vipi?miaka yote hiyo tofauti lazima iagizwe nje, na sukari ndio maana ilikuwa iko kwenye bei ya 1800 kwa kilo moja, alipoingia mwendazake na sera zake za NGUVU NYINGI MAARIFA KIDOGO, tunajua kilichotokea na ndicho kimetufikusha hapa hadi leo kwenye wastani wa 2700 kwa kilo moja!!viwanda vya ndani hata hicho kiwango tu cha tani 320, 000 wakati mwingine hakifiki mala mashamba yamejaa maji, una kuta nao tena wanafanya kazi ya kuingiza sukari kutoka nje tena!!Na kutu kingine gharama za uzarishaji wa bidhaa nchini ni mkubwa mno, sukari lazima iagizwe nje , sasa utaratibu wa uingizaji ndio mala nyingi unakuwa na matatizo.Miaka mitano yote tuliaminishwa kuwa ni muda wa kulinda viwanda vyetu ili vikue, yako wapi?kila kitu kimepanda bei, cement, nondo, vifaa vya umeme na vingi ni vya hapa hapa!!!
 
Ndiyo maana nikauliza Kama awamu ya tano ilikuwa inalinda viwanda vya ndani na wawekezaji,,. Sasa awamu ya 6 itakuwa inalinda maslahi ya nani? Jibu hapa ni rahisi kuwa analinda mlaji sasa Kama rais ameamua kulinda maslahi ya mlaji kwanini tusimuunge mkono? Maana yeye hataki tukose sukari ndiyo maana kaona jungu lake haliwezi kupika chakula Cha kutosha familia yake je Kuna dhambi gani kuomba kwa jirani? Na hawa wanaoonekana kupingana na mh rais wana maslahi gani katika janga hili la sukari? Haya maswali yanaumiza vichwani mwetu maana haiwezekani sukari isafirishwe kutoka nje ya nchi niuziewe 2000 halafu ya kutoka hapa hapa niuziewe 2700 huoni Kuna wizi na uuaji unafanywa na watu tuliowapa dhamana?
 
Labda kuna kodi zimeongezwa kwenye importation ya raw materials. Sina uhakika kama raw materials za sukari ni miwa peke yake.
 
Serikali ya Tanzania haimjali mtanzania. Inachoangalia yenyewe ni kupata kodi na tozo. Unaona kbs viwanda vya ndani havitoshi kwa uzalishaji halafu unazuia sukari ya nje. Unategemea nini?
Angalia mishahara ya wabunge, mawaziri na raisi uone km watashindwa kununua hiyo sukari ya 2700.
 
Nadhani kila kitu kikipanda tunapata taarifa zilizo na zisizo rasmi sasa ajitokeze muhusika yeyoye aweze kutoa mnyumbulisho wa gharama za uzalishaji ili walaji tusinung'unike kuona hali ya Bei!!
Japo Hilo najua litakua gumu maana Kuna usiri Sana katika suala la sukari na lengo hapa ni ili wapige madili yao hila kushtukiwa, inavyoonekana hatuna uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha nchi nzima lakini pia hatutaki kuingiza sukari toka nje wewe unaona Nini hapo Kama sio uhuni Kama huwezi kuzalisha sukari ya kutosheleza walaji roho mbaya ya Nini sasa?
 
Kweli kabisa ina maana viongozi watanzania wanapenda maziwa lakini hawampendi ng'ombe hiyo ndiyo hali halisi kupenda Kodi wakati humjali mlipa Kodi ni sawa na kumkamua ng'ombe maziwa wakati anahali mbaya na hapo hapo umesahau kuwa ng'ombe huyu huyu anae ndama anatakiwa kunyonya maziwa hayo hayo anayategemea Kama chakula chake
 
Ndiyo maana nikauliza Kama awamu ya tano ilikuwa inalinda viwanda vya ndani na wawekezaji,,. Sasa awamu ya 6 itakuwa inalinda maslahi ya nani? Jibu hapa ni rahisi kuwa analinda mlaji sasa Kama rais ameamua kulinda maslahi ya mlaji kwanini tusimuunge mkono? Maana yeye hataki tukose sukari ndiyo maana kaona jungu lake haliwezi kupika chakula Cha kutosha familia yake je Kuna dhambi gani kuomba kwa jirani? Na hawa wanaoonekana kupingana na mh rais wana maslahi gani katika janga hili la sukari? Haya maswali yanaumiza vichwani mwetu maana haiwezekani sukari isafirishwe kutoka nje ya nchi niuziewe 2000 halafu ya kutoka hapa hapa niuziewe 2700 huoni Kuna wizi na uuaji unafanywa na watu tuliowapa dhamana?
Hao wanaopinga ndio wametufikisha hapa, waliaminishwa na jpm kuwa nchi inaweza kwenda kwa kuwaona waliokuzidi ni maadui wako, unafikiria hata mafuta ya kula tatizo lilianzia pale alipopiga marufuku uingizaji wa mafuta ghafi kwa kuweka kodi ya juu sana kikichotokea hadi leo ni kilio!!yeye mama aruhusu tu bidhaa zenye upungufu nchini ziingie tu ili hata kwa mlaji kuwe na unafuu!!tatizo la wafuasi wa awamu ya tano, bado wanafirikia mama amemshikia tu jamaa atarudi.hivyo zile sera zake za hovyo ziendelee kukumbatiwa.
 
Nadhani kila kitu kikipanda tunapata taarifa zilizo na zisizo rasmi sasa ajitokeze muhusika yeyoye aweze kutoa mnyumbulisho wa gharama za uzalishaji ili walaji tusinung'unike kuona hali ya Bei!!
Japo Hilo najua litakua gumu maana Kuna usiri Sana katika suala la sukari na lengo hapa ni ili wapige madili yao hila kushtukiwa, inavyoonekana hatuna uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha nchi nzima lakini pia hatutaki kuingiza sukari toka nje wewe unaona Nini hapo Kama sio uhuni Kama huwezi kuzalisha sukari ya kutosheleza walaji roho mbaya ya Nini sasa?
Wanataka tu kutukomoa na kupandisha bei kila kitu bila sababu maalumu. Kila kitu kitasingiziwa soko la dunia
 
Nadhani kila kitu kikipanda tunapata taarifa zilizo na zisizo rasmi sasa ajitokeze muhusika yeyoye aweze kutoa mnyumbulisho wa gharama za uzalishaji ili walaji tusinung'unike kuona hali ya Bei!!
Japo Hilo najua litakua gumu maana Kuna usiri Sana katika suala la sukari na lengo hapa ni ili wapige madili yao hila kushtukiwa, inavyoonekana hatuna uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha nchi nzima lakini pia hatutaki kuingiza sukari toka nje wewe unaona Nini hapo Kama sio uhuni Kama huwezi kuzalisha sukari ya kutosheleza walaji roho mbaya ya Nini sasa?
Miaka yote Tz, tunaagiza sukari toka nje sijui kwanini hii kauli ya rais imeonekana ya ajabu au ni kwakuwa ni kutoka UGANDA, ila brazil ni sawa!!
 
Back
Top Bottom