Kwanini sukari imekuwa ghali saaana wakati viwanda vipo nchini vya kutosha?

Mie hiyo sumu nanunua Unguja1 kg kwa sh 2000/-. Inamaana hata Zanzibar wanaweza kutupatia kiasi flani cha sukari lakini na yenyewe inapigwa pini.
Itaachaje kupigwa pini wakati inaingilia maslahi ya vigogo Fulani?
 
Mimi nazani bei ya sukari kuwa juu ni kutokana na running cost mfano bei ya umeme kwa Tz ni kama sh 600/unit wakati nje ya nchi bei ni sh 40/unit Hapo ni lazima bei iwe nafuu ukilinganisha na Tz.

Hebu jiulize bei ya mafuta ya alzeti kutoka singida ni kubwa bei ya mafuta ya safi wakati safi yanatoka nje?
 
Hahahahaaa mkuu usipende kurahisisha Jambo gumu kiivyo unajua sukari inahitajika mwilini.
Sukari inayohitajika mwilini ataipata kupitia kula mihogo, viazi vitamu, ugali wa Dona etc. Sukari ya kuongeza kwenye uji na chai haina faida yoyote mwilini.....
 
Je uwezo wa viwanda vyetu ni kiasi gani ukilinganisha na mahitaji??
 
Hi vyo ndiyo vitu tunatakiwa tujiulize kwanini umeme kwetu uwe juu wakati mabwawa yanajazwa na mvua ya mungu? Na kwanini walizima mradi wa umeme wa gesi ambao ulianza kuonyesha kuwa tunaweza kuja kupata umeme wa uhakika maana uzalishaji umeme kutumia gesi haina kiangazi Wala kipupwe?,, Haya yote tukiyatafuta mchawi anabaki kuwa ni kiongozi tunaempa dhamana hatuna uwezo wakumsemesha baada ya kumpa madaraka dawa inabaki kuwa ni moja na vipengele vyake tukipata katiba mpya iliyo Bora italeta tume huru ya uchaguzi na itampa mwananchi heshima yake ambaye ndie mwenye nchi katiba mpya ni muhimu tangu muda Sana ila inahitajika Sana zaidi kwa sasa na kuendelea
 
Sukari inayohitajika mwilini ataipata kupitia kula mihogo, viazi vitamu, ugali wa Dona etc. Sukari ya kuongeza kwenye uji na chai haina faida yoyote mwilini.....
Kwa hiyo ni sahihi tuache iendelee kuwa Bei juu na unaamini kuwa mifumuko ya Bei inabaki kwenye sukari pekee bila kuathiri vitu vingine na wananchi kwa ujumla?
 
Je uwezo wa viwanda vyetu ni kiasi gani ukilinganisha na mahitaji??
Uwezo ni mdogo upo chini ya wastani kulingana na mahitaji ila ndo hivyo kwa maslahi yao hawataki sukari iingie kutoka nje
 
Kwa hiyo ni sahihi tuache iendelee kuwa Bei juu na unaamini kuwa mifumuko ya Bei inabaki kwenye sukari pekee bila kuathiri vitu vingine na wananchi kwa ujumla?
Sukari ya kuweka kwenye chai na uji ina faida ipi mwilini hasa ituchezeshe ngoma kiasi hiki?? Tuanzie hapa Kwanza.
 
Sukari ya kuweka kwenye chai na uji ina faida ipi mwilini hasa ituchezeshe ngoma kiasi hiki?? Tuanzie hapa Kwanza.
Mkuu wewe na jamii yako haitumii sukari kabisa?
 
That is NONSENSE, bei sio kubwa πŸ’
 
Mwendazake alituweza sana
 
inapaswa mtu anapotamka tunalinda viwanda vyetu, VIWE VYA BABA AKE!!!
 
Uwezo wa viwanda vya ndani kuzalisha sukari ya kutosha ni mdogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…