So mkuu kazi ihamie kwanza kutengeneza middle class income?
Na ni vipi itengenezwe hiyo class?
"Middle Class" hutengenezwa kwa serikali kutoa fursa kwa wananchi wake,bila "Middle class", watu wenye
uchumi wa kati sio matariji sio maskini ni watu muhimu kwenye kila taifa,hawa watu ndio wanaleta mzunguko wa Pesa kwenye nchi.,hawa watu ndio wenye "Purchasing Power"
Serikali inabidi itoe fursa kwa mashirika binafsi,wafanya biashara,nk, yaani kwa ufupi sekta binafsi inabidi iinuliwe ili watu wajiweze na wawawezeshe..
Serikail ya Jakaya Kikwete iliweza kidogo kuwainua watanzania wakawa katika hali ya "Middle class",kulikuwa na mzunguko wa Pesa kila raia alikuwa na uwezo wa kununua kile anachotaka,bila ya kufikria mara mbili..
Serikali ya Maguful
i imezima ukuwaji wa "Middle class" hakuna mzunguko wa Pesa,raia anajiuliza mara mbili mbili vipi atumie Pesa zake,hali hiyo inafanya maduka ya kawaida pamoja na Super Market kufungwa..hakuna "Purchasing Power"
Moja katika kuleta mzunguko wa Pesa kwa raia ni kuziruhusu kampuni au mashirika binafsi yafanye biashara na Serikali,Serikali ya Magufuli imekataza hilo,kufanya hivyo zimefanya biashara nyengine zidorore nyengine zifungwe kabisa,hali hiyo imefanya raia wengine wakose kazi,wakose kuwa na uwezo wa kununua vitu madukani,mzunguko wa Pesa imekatika..
Nitakupa mfano mdogo wa Jeshi la Marekani,Jeshi kubwa na tajiri duniani,Jeshi la Marekani lina vitengo (Base)sehemu mbali mbali duniani,lakini utakuta Meli zinazopeleka vyakula na vifaa vyengine vya kawaida kwa wanajeshi wake ni
Meli za kampuni binafsi,wafanyakazi wa meli hizo sio majeshi ni raia wa kawaida, huo ni mfano mdogo tu wa kuenua "Private sector",sekta binafsi katika nchi,...
Serikali ya Magufuli ilipokata kampuni binafsi au wafanya biashara wasifanye kazi na vyombo vya dola kama Magerza na Jeshi,wafanyakazi wa serikali wasifanye mikutano yao kwenye Hoteli za watu binafsi,hio ilikuwa moja katika kukata mzunguko wa Pesa kwa raia,hiyo ni mifano midogo tu,kuna mifano mingi vipi Serekali ya Magufuli inavyokatisha mizungiukowa Pesa ,vipi inaua "Middle class"
Magufuli anafikri utajiri ni ubebari,Ubepari ni uhalifu...alishawahi kusema "Matajiri wataishi kama mashetani...
",Magufuli na serikali yake ina mawazo ya "Kimasikini",kuna mwanasiasa mmoja wa Kenya simkumbuki jina lake alishawahi kusema kuwa
"Magufuli ana cheo kikubwa katika nchi kubwa lakini mawazo na maamuzi yake ni sana na mwenyekiti wa kijiji"