Kwanini supermarkets kubwa zimeshindwa soko la Tanzania na ndogo haziwezi kuwa kubwa?

Kwanini supermarkets kubwa zimeshindwa soko la Tanzania na ndogo haziwezi kuwa kubwa?

tatizo ni locations ya hizo supermarket ni mtihani kwa wanyonge kufika..embu nambie mtu wa Mbagala anafikaje Mliman city

kwanini umetolea mfano wa mbagala ambapo ni mbali sana na mlimani city?

kwanini usingetolea mfano wa mwenge,ubungo,kijitonyama,kawe,mikocheni,ostyerbay,na makongo juu!?

hawa wote kwa hoja ya location walikuwa wanatosheleza mauzo ya hpo mlimani city
 
Lifestyle ya tajiri isn't defined niga, Bill Gates alikuja bongo, alikula wali maharage, kuna wanaoprefer kuishi high life. You're simply short sighted.
Unataka kuniambia bill gate angekuwa mkazi wa hapa angekuwa anakula kwa mama ntilie?
 
Tatizo kumbwa kwanini hizo supermarket kumbwa zimeshidwa na ndogo hazikuwi....tzn hatuna middle income class kumbwa ambayo inajali quality badala ya quantity yani population yetu kubwa ni (marginal consumers ) cha pili hatuna local manufactured items vingi to import bei inakua juu kwa wateja na shida ya tatu serikali yetu itabiliki anything can happen any time to any body's bussiness

Asante sana mkuu kwa kuandika point ambayo pia ndipo umasikini wa Tanzania ulipo na ndipo utajiri wa Kenya ulipo...Wakati mwingine napata shida sana na wasomi wetu kiasi cha kuwadharau maana suala hili sijui hawalioni...!!

Tunaamini kwenye heavy industry ambazo kurun na kuanzisha kunahitani mitaji mikubwa hivyo lazima wageni ndio waje kuwekeza na ili waje lazima wajiridhishe na siasa zetu wasije kurisk mitaji yao.. Hizi heavy industry nyingi raw material nyingi huagizwa hivyo kwenye production cost lazima watupige..

Ni wakati wa serikali kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo vinavyotumia mazao ya kilimo kama raw material ili mwisho wa siku tulishike kisawasawa soko la ndani ikwezekana na kuifikia east Africa population yoote..
 
Umesema kweli. Lakini nadhani super market za bongo nazo zimekosa ubunifu. Wangejaribu kuzibadili ziendane na mazingira yetu. Nikipata muda nitaelezea zaidi

Wapange mafungu ya nyanya, vitunguu, wauze utumbo, waning'inize nyama juu.. Nafikiri nyingi zinajaribu kwenda na international standard... Nyanya Lazima uipreserve ndio uuze, pilipili, hoho nk ni hivyo hivyo pia....
 
Super market Sio utamaduni wetu, mtaa una magenge kumi sasa supermarket nikafanye nini?? Binafsi supermarket nanua vitu ambavyo kitaa siwez kuvipata. Ukiangalia mazingira ya masoko ya huku kwetu na Kwa wenzetu ni tofauti. Huku Kwetu Kila kona kumejaa wachuuz na maduka.
 
Wapange mafungu ya nyanya, vitunguu, wauze utumbo, waning'inize nyama juu.. Nafikiri nyingi zinajaribu kwenda na international standard... Nyanya Lazima uipreserve ndio uuze, pilipili, hoho nk ni hivyo hivyo pia....
Sawa sawa...... lazima tubadilika sambamba na international standards
 
Life style tu watu hawajazoea kutokana na lack of exposure mbona supermarkets vitu ndio vinauzwa cheaper kuliko maduka ya mtaani

Supermarkets za bongo: Fungu la nyanya gengeni 500 supermarkets 1000. Kwa wenzetu ni vice versa. Pia zipo kila sehemu.

Supermarkets zikienea sana zinaweza kuua biashara za wafanyabiashara wadogowadogo. Bora kuongeza na kuboresha masoko (usafi, accessibility, visibility, security).
 
Mkuu hilo ni sawa, ila sio kila siku kuna nyama ya juzi ata ilioletwa leo inatuzwa kwenye freeza, ni dhana ilio jengeka na tabaka la ma peasant eti supermarket vitu ni vya siku nyingi....pia quality ya bidha ni kitu muhimu katika supermarket, pia kodi inapatikana kuliko gengeni ambao ni informal, pia it's ameeting place kwa tabaka fulani(middle class) security ya gari na mari zako ni muhimu supermarket kuna usafi na mazingira rafiki yakununua vitu vingi kwa wakati mdogo time saving.

Mkuu umeona mbali. Hoja zako ni murua kabisa. Hata waTanzania wenye uwezo bado wako ki peasant tuu. Hatuangalii quality. in addition, kwa sababu ya nature ya maisha yetu wengi hawako busy ndo maana watapata mda wa kwenda Kariakoo nk. Siku hizi unakuta bucha wanauza nyama za mifugo iliyokufa...mambo yanaogopesha.

Huwezi kupiga box asubuhi mpaka jioni upate mda wa kwenda Kariakoo. Never. Wengi wanadhani supermarket ni luxury. Far from that. Inahusisha convenience, usafi, usalama wa mali za mteja, wide choices na mengine lukuki.

Mfano huwezi kuwa unaendesha gari ya 50M ukaenda kunywa bia uswahilini. Si kwamba unapadharau, Lakini unaweka usalama wa gari lako mashakani! Hata watu unaokutana nao ni muhimu sana.

Na hapo ndo tunakosea. Huwezi kujenga uchumi bila kuwa na middle class! kwa sababu middle class ndo consumers wakubwa na ndo wana taste ya luxuries! Sasa wewe kila siku lalamika kwamba Tanzania ni ya wanyonge....itakuwa ya wanyonge kweli na sijui utakusanya kodi kwa nani!
 
Lifestyle ya tajiri isn't defined niga, Bill Gates alikuja bongo, alikula wali maharage, kuna wanaoprefer kuishi high life. You're simply short sighted.

wewe ndo uko shortsighted! Hata wewe ukienda kwenye msiba unaweza kula hata kwenye majani ya mgomba! mazingira yana determine ubehave vipi. high life ni very subjective. Jamaa anachoongea ni swala la watu kufanya shoping supermarket. ndo akatoa mifano....

Una uwezo kweli halafu uendeshe gari kwenda Kariakoo kununua mchele na nyanya? where do you get that time??
 
Jibu ni rahisi tu, purchasing power Tanzania ni ndogo sana, yaani watu wenye uwezo wa kununua vitu vingi kwa wakati mmoja ni wachache sana hivyo hawatoshi kuifanya Supermarket itengeneze faida.

Sehemu kubwa ya Watanzania wanamudu kununua vitu gengeni au sokoni!
Unadhan kwann purchasing power ya watanzania wengi ni ndogo??
 
Supermarkets za bongo: Fungu la nyanya gengeni 500 supermarkets 1000. Kwa wenzetu ni vice versa. Pia zipo kila sehemu.

Supermarkets zikienea sana zinaweza kuua biashara za wafanyabiashara wadogowadogo. Bora kuongeza na kuboresha masoko (usafi, accessibility, visibility).

Hapana....supermarket zinaongeza ajira kipato cha serikali uzalishaji wandani (local production) nakupunguza mgojwa ya mlipuko kama kipindupindu kuharisha nk. Kwamfano supermarke ya kati inauwezo wa kuajiri watu 50-150....kwahiyo mtaa moja ukiwa na supermarket 4 tu vijana zaidi ya 500 watapata ajira za wakika kila kijana akiwa na mke nawatoto 2 = 500×3 wtz watapata maisha mazuri, serikali intapata mapato mzri tu.....kuliko ku angaika na vigenge vinavyo saidia familia chache na pia havina good hygiene and sanitation
 
Mkuu umeona mbali. Hoja zako ni murua kabisa. Hata waTanzania wenye uwezo bado wako ki peasant tuu. Hatuangalii quality. in addition, kwa sababu ya nature ya maisha yetu wengi hawako busy ndo maana watapata mda wa kwenda Kariakoo nk. Siku hizi unakuta bucha wanauza nyama za mifugo iliyokufa...mambo yanaogopesha.

Huwezi kupiga box asubuhi mpaka jioni upate mda wa kwenda Kariakoo. Never. Wengi wanadhani supermarket ni luxury. Far from that. Inahusisha convenience, usafi, usalama wa mali za mteja, wide choices na mengine lukuki.

Mfano huwezi kuwa unaendesha gari ya 50M ukaenda kunywa bia uswahilini. Si kwamba unapadharau, Lakini unaweka usalama wa gari lako mashakani! Hata watu unaokutana nao ni muhimu sana.

Na hapo ndo tunakosea. Huwezi kujenga uchumi bila kuwa na middle class! kwa sababu middle class ndo consumers wakubwa na ndo wana taste ya luxuries! Sasa wewe kila siku lalamika kwamba Tanzania ni ya wanyonge....itakuwa ya wanyonge kweli na sijui utakusanya kodi kwa nani!

hongera mkuu kwa ufafanuzi makini

attitude ya kiongozi wetu inawadicourage wananchi wsnaopambana na umaskini

imefikia hatua umaskini unaonekana km sifa nzuri na utajiri ni sifa mbaya!
 
Kitu kikubwa ambacho wengi hawakioni na kinaua sana biashara ni customer care.......

Wahudumu wetu kwenye maduka haya hawako friendly na wateja........

Wao wenyewe wanaamini kuwa hizo shops ni kwa ajili ya watu wenye kipato kikubwa....ukienda Mtu kama mimi wanaanza kukuonyeshea dharau nje nje.....sasa ni nani anapenda kudharaulika na pesa yake wakati hizo huduma zinapatikana mtaa wa pili.......

Haya mambo ni mageni kwenye jamii za Watanzania lakini wahudumu wa hayo maduka makubwa wangefanikiwa kuifuta hii dhana kwa huduma nzuri kwa wateja.........

Pamoja Na sababu zingine nyingi lakini hilo la customer care ni jambo la msingi snaa na biashara nyingi zimekufa kwa kuchangiwa na hilo......
 
So mkuu kazi ihamie kwanza kutengeneza middle class income?
Na ni vipi itengenezwe hiyo class?
"Middle Class" hutengenezwa kwa serikali kutoa fursa kwa wananchi wake,bila "Middle class", watu wenye uchumi wa kati sio matariji sio maskini ni watu muhimu kwenye kila taifa,hawa watu ndio wanaleta mzunguko wa Pesa kwenye nchi.,hawa watu ndio wenye "Purchasing Power"

Serikali inabidi itoe fursa kwa mashirika binafsi,wafanya biashara,nk, yaani kwa ufupi sekta binafsi inabidi iinuliwe ili watu wajiweze na wawawezeshe..

Serikail ya Jakaya Kikwete iliweza kidogo kuwainua watanzania wakawa katika hali ya "Middle class",kulikuwa na mzunguko wa Pesa kila raia alikuwa na uwezo wa kununua kile anachotaka,bila ya kufikria mara mbili..

Serikali ya Magufuli imezima ukuwaji wa "Middle class" hakuna mzunguko wa Pesa,raia anajiuliza mara mbili mbili vipi atumie Pesa zake,hali hiyo inafanya maduka ya kawaida pamoja na Super Market kufungwa..hakuna "Purchasing Power"

Moja katika kuleta mzunguko wa Pesa kwa raia ni kuziruhusu kampuni au mashirika binafsi yafanye biashara na Serikali,Serikali ya Magufuli imekataza hilo,kufanya hivyo zimefanya biashara nyengine zidorore nyengine zifungwe kabisa,hali hiyo imefanya raia wengine wakose kazi,wakose kuwa na uwezo wa kununua vitu madukani,mzunguko wa Pesa imekatika..

Nitakupa mfano mdogo wa Jeshi la Marekani,Jeshi kubwa na tajiri duniani,Jeshi la Marekani lina vitengo (Base)sehemu mbali mbali duniani,lakini utakuta Meli zinazopeleka vyakula na vifaa vyengine vya kawaida kwa wanajeshi wake ni Meli za kampuni binafsi,wafanyakazi wa meli hizo sio majeshi ni raia wa kawaida, huo ni mfano mdogo tu wa kuenua "Private sector",sekta binafsi katika nchi,...

Serikali ya Magufuli ilipokata kampuni binafsi au wafanya biashara wasifanye kazi na vyombo vya dola kama Magerza na Jeshi,wafanyakazi wa serikali wasifanye mikutano yao kwenye Hoteli za watu binafsi,hio ilikuwa moja katika kukata mzunguko wa Pesa kwa raia,hiyo ni mifano midogo tu,kuna mifano mingi vipi Serekali ya Magufuli inavyokatisha mizungiukowa Pesa ,vipi inaua "Middle class"

Magufuli anafikri utajiri ni ubebari,Ubepari ni uhalifu...alishawahi kusema "Matajiri wataishi kama mashetani...",Magufuli na serikali yake ina mawazo ya "Kimasikini",kuna mwanasiasa mmoja wa Kenya simkumbuki jina lake alishawahi kusema kuwa "Magufuli ana cheo kikubwa katika nchi kubwa lakini mawazo na maamuzi yake ni sana na mwenyekiti wa kijiji"
 
Na hapo ndo tunakosea. Huwezi kujenga uchumi bila kuwa na middle class! kwa sababu middle class ndo consumers wakubwa na ndo wana taste ya luxuries! Sasa wewe kila siku lalamika kwamba Tanzania ni ya wanyonge....itakuwa ya wanyonge kweli na sijui utakusanya kodi kwa nani!
Umesema vyema mkuu,maendeleo ya watu ni muhimu kuliko maendeleo ya vitu. Serikali ingeweka mazingira mazuri ya wananchi wake wengi kumiliki njia kuu za uchumi,maendeleo ya vitu yangekuja automatically. Kwa hali ilivyo sasa huko tuendapo hata hiyo kodi haitaweza kukusanywa watu watakua hoi taabani.
 
"Middle Class" hutengenezwa kwa serikali kutoa fursa kwa wananchi wake,bila "Middle class", watu wenye uchumi wa kati sio matariji sio maskini ni watu muhimu kwenye kila taifa,hawa watu ndio wanaleta mzunguko wa Pesa kwenye nchi.,hawa watu ndio wenye "Purchasing Power"

Serikali inabidi itoe fursa kwa mashirika binafsi,wafanya biashara,nk, yaani kwa ufupi sekta binafsi inabidi iinuliwe ili watu wajiweze na wawawezeshe..

Serikail ya Jakaya Kikwete iliweza kidogo kuwainua watanzania wakawa katika hali ya "Middle class",kulikuwa na mzunguko wa Pesa kila raia alikuwa na uwezo wa kununua kile anachotaka,bila ya kufikria mara mbili..

Serikali ya Magufuli imezima ukuwaji wa "Middle class" hakuna mzunguko wa Pesa,raia anajiuliza mara mbili mbili vipi atumie Pesa zake,hali hiyo inafanya maduka ya kawaida pamoja na Super Market kufungwa..hakuna "Purchasing Power"

Moja katika kuleta mzunguko wa Pesa kwa raia ni kuziruhusu kampuni au mashirika binafsi yafanye biashara na Serikali,Serikali ya Magufuli imekataza hilo,kufanya hivyo zimefanya biashara nyengine zidorore nyengine zifungwe kabisa,hali hiyo imefanya raia wengine wakose kazi,wakose kuwa na uwezo wa kununua vitu madukani,mzunguko wa Pesa imekatika..

Nitakupa mfano mdogo wa Jeshi la Marekani,Jeshi kubwa na tajiri duniani,Jeshi la Marekani lina vitengo (Base)sehemu mbali mbali duniani,lakini utakuta Meli zinazopeleka vyakula na vifaa vyengine vya kawaida kwa wanajeshi wake ni Meli za kampuni binafsi,wafanyakazi wa meli hizo sio majeshi ni raia wa kawaida, huo ni mfano mdogo tu wa kuenua "Private sector",sekta binafsi katika nchi,...

Serikali ya Magufuli ilipokata kampuni binafsi au wafanya biashara wasifanye kazi na vyombo vya dola kama Magerza na Jeshi,wafanyakazi wa serikali wasifanye mikutano yao kwenye Hoteli za watu binafsi,hio ilikuwa moja katika kukata mzunguko wa Pesa kwa raia,hiyo ni mifano midogo tu,kuna mifano mingi vipi Serekali ya Magufuli inavyokatisha mizungiukowa Pesa ,vipi inaua "Middle class"

Magufuli anafikri utajiri ni ubebari,Ubepari ni uhalifu...aloshawahi kusema "Matajiri wataishi kama mashetani...",Magufuli na serikali yake ina mawzo ya "Kimasikini",kuna mwanasiasa mmoja wa Kenya simkumbuki jina lake alishawahim kusema kuwa "Magufuli ana cheo kikubwa katika nchi kubwa lakini mawazo na maamuzi yake ni sana na mwenyekiti wa kijiji"
Umenena vyema.
 
Purchasing power ya tanzania ipo chini sana. Hii inatokana na uchache wa watu wenye kipato cha kati kuwa kidogo sana kiasi wanaomudu hawawezi kutosheleza hizo biashara.

Lakini pia mfumo wa maduka ya mtaani ni tatizo kubwa kwa uwepo wa supermarket. Nchi nyingine mahitaji yote ya kila siku kama sukari, unga, vinywaji nk unapata supermarket lakini bongo kuna utitiri wa viduka ambavyo viko karibu na makazi hivyo supermarket inakuwa haina ulazima tena labda kwa vitu visivyopatikana kwenye viduka mtaani.

Hata hapo nairobi tu ni nadra kukuta viduka mtaani hii hulazimisha watu kwenda supermarket.
 
tatizo ni locations ya hizo supermarket ni mtihani kwa wanyonge kufika..embu nambie mtu wa Mbagala anafikaje Mliman city
Kwanza mbagala supermarket zipo kulekule kwa mahitaji ya majumbani, Mlimani city labda kwa bidhaa kubwa tu.

Mbagala sasa hivi inajitosheleza kwa mambo mengi,
 
Back
Top Bottom