Kwanini supermarkets kubwa zimeshindwa soko la Tanzania na ndogo haziwezi kuwa kubwa?

Kwanini supermarkets kubwa zimeshindwa soko la Tanzania na ndogo haziwezi kuwa kubwa?

Labda kama Wewe huishi hapa nchini.....

Watanzania wengi ni wahanga wa customer care...!!!

Mimi huwa nikisogelea huduma yeyote ambayo inamhusisha mtu basi camera ya simu yangu huwa on.

Ili kuweka ushahidi wa huduma nitakayopewa.

Siku nyungine fanya hivyo mkuu halafu unamtolea taarifa kwa kiongozi wake.

Wasipolifanyia kazi unaweka malalamiko mitandaoni watu wajionee.

Hakuna atakekubali kuchafua "brand" yake kwa kumvumilia mfanyakazi anaetoa huduma mbovu kwa mteja
 
Nakubaliana na wewe kwa pointi hiyo ikichagizwa na mindiset zetu kua humo vitu ni gharama sana, huwezi amini nimesoma pale Ardhi sijawahi nunua kitu pale mlimani nikiamini ni bei kubwa, siku moja nikapelekwa nikashangaa nanunua bei nyepesi kuliko hata kwanye maduka ya mitaani

2. hazijitangazi vya kutosha juu ya bidhaa zao

Mkuu kwani mangi mtaani wanajitangaza vya kutosha?

Nakumbuka shoprite walikuwa wanajitangaza sana hadi vipeperushi vya discount walikuwa wanagawa all the way kwenye makutano ya barabara kubwa.

Kubwa ni swala mindset tuu kwamba vitu vya supermarkets ni bei kubwa.
 
M napenda vitu fresh zaidi kuliko ambavyo vimekaa zaid ya wiki. Halafu kununua vitu super market sio ujanja saana!

Hata supermarkets zinauza vitu fresh pia
 
Mazoea tu. Binafsi napenda product ya sokoni kwa mkulima pia naamin naturality ipo huko hasa kwa mahitaji ya chakula. Unaweza kuona, kwa mtazamo huu Supermarkets haziendelei hata kama bei za bidha zao ni poa kuliko mtaani.
 
Hapo Ireland kuna sheria za EU zinazowalinda wafanyakazi na suppliers. Pia wakulima wanapata ruzuku nyingi sana. Kwa hiyo hata sisi we need system which allow competition, efficiency and freedom but also offer protection for certain groups and sector of society. Mixed economy with certain controls.

Unregulated free market and laissez-faire economy to which both government and the whole society are subordinate to market forces of supply and demand will always end in disaster like 2008 credit crunch and financial crisis.

There is really no 100% unfettered free market and laissez-faire economy anywhere in the world as far as i know. USA (Steel), EU ( Common Agriculture Policy, CAP), China (currency manipulation), Russia and India all of them protect certain sectors. It is all about proper checks and right balance for the economy.

Mkuu tumekaririshwa vibaya kwamba laissez-faire basi ni completely free.

Ukimsoma Adam smith kuna concept ya 'invisible hand' ambayo ni part ya government kufanya regulation kwenye market.

Japo best word ya kutumia ni 'mixed economy'
 
Lakini wapiga debe wa Tanzania ya viwanda hawajaweza kuweka fungamano hilo.

Cultural problem- Tumezoea viduka vya kwa mangi kwenye corner ya mtaa supermarket is not our thing.....!
 
Hatuna mazoea ya kununua mahitaji super market, binafsi napenda product ya mkulima pia naamin naturality haipo huko hasa kwa mahitaji ya chakula. Ingawa unafuu wa bei ya bidhaa ipo super market. Kutoka na mtazamo kama huu hasa wangu, super markets haziwezi kuendelea.

Kuna hadi organic product mkuu
Tena wanaofanya hiyo biashara wanakuwa regulated kabisa wanapofanya uzalishaji wa chakula.

Gengeni unaweza kwenda na kununua mboga ukifikiri ni freah kumbe sio.

Mimi imeshawahi kunitokea nimenunua mboga za majani kufika home naanza kuzikata nasikia harufu ya dawa kabisa.
 
Naona kuna businesa model hapo mkuu!

Wajasiriamali wanaweza fanyia kazi wazo lako na kuuza vitu fresh lakini kwenye mazingira mazuri zaidi na yatakayoinua uchumi kwa ujumla
Asante sana. Na mimi ndiyo hasa wazo langu. Tukiweza kutengeneza kitu ambacho ni chotara kati ya Super Market za Ulaya na Masoko yetu tunaweza kuja na kitu kizuri sana.
 
Kuna hadi organic product mkuu
Tena wanaofanya hiyo biashara wanakuwa regulated kabisa wanapofanya uzalishaji wa chakula.

Gengeni unaweza kwenda na kununua mboga ukifikiri ni freah kumbe sio.

Mimi imeshawahi kunitokea nimenunua mboga za majani kufika home naanza kuzikata nasikia harufu ya dawa kabisa.
Mkuu kwa Bongo yetu kuwa-regulate watu wa Super Market ni ngumu. Niliwahi kufanya kazi super market za majuu na ukiona watu walivyo waaminifu huwezi kuamini. Kitu kama keki kinaweza kuanguka chini (kabla hata duka halijafunguliwa na yupo mpangaji peke yake) na akiweka kwenye dust bin. Hapo bado sijaongelea mavyakula na vinywaji vinavyotupwa kila siku kwa sababu muda umeisha.
 
Mkuu kwa Bongo yetu kuwa-regulate watu wa Super Market ni ngumu. Niliwahi kufanya kazi super market za majuu na ukiona watu walivyo waaminifu huwezi kuamini. Kitu kama keki kinaweza kuanguka chini (kabla hata duka halijafunguliwa na yupo mpangaji peke yake) na akiweka kwenye dust bin. Hapo bado sijaongelea mavyakula na vinywaji vinavyotupwa kila siku kwa sababu muda umeisha.

Culture hutengenezwa na kuanza kwa kufikiri kwanza inawezekana kufika kule tunapotaka na tujiandae kukumbana na kila aina ya ugumu njiani
 
umejibu ki ccm zaidi ungetakiwa upanue ubongo wako ujibu pasi kufungamana upande wowote
Jibu ni rahisi tu, purchasing power Tanzania ni ndogo sana, yaani watu wenye uwezo wa kununua vitu vingi kwa wakati mmoja ni wachache sana hivyo hawatoshi kuifanya Supermarket itengeneze faida.

Sehemu kubwa ya Watanzania wanamudu kununua vitu gengeni au sokoni!
 
Tatizo ni BEI JUU MKUU,,huko SOUTH AFRICA ,,SUPER MARKET ndy sehemu ambazo WATU WA HALI YA CHINI hujipatia MAHITAJI YAO,,,,tena super market huingia kila MTU,,lakini hapa kwetu SHOPRITE wanaingia MADARAJA FULANI YA JUU,.. SHOPRITE WANAUZA bidhaa rahisi kuliko MADUKA YA NJE MITAANI HUKO SOUTH,,,hata hilo DUKA LA NGUO LA MR PRICE huko south ukivaa UNACHEKWA,,,ni maduka wanayovaa WANYONGE, lakini hapa kwetu WANAUZA BEI juu hatari,, ..na ukivaa unaonekana wewe mjanja,,nadhani kuna tatizo sehemu,,ila SUPER MARKET INAPASWA IUZE VITU RAHISI KULIKO MADUKA YA MANGI NA SHIRIMA...MITAANI..
 
Back
Top Bottom