Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Huu mjadala nimeutoa Facebook tuuchakate kwa mapana yake.
Ni kwa nini taasisi za kanisa zinapotengeneza faida waumini hatuhusishwi na wala hatunufaiki na lolote?
Ukondoo sasa basi, tunatumia akili zetu kwa kila jambo.
=========
INAWEZEKANA KUNUSURU MALI ZA KANISA LA KKKT ZISIPIGWE MNADA NA MADALALI?
Nilikuwa naangalia Lamine Yamal aliyetimiza miaka 17 siku ya Jumapili akitunukiwa tuzo ya mchezaji bora mdogo baada ya kuiwezesha Hispania kutwaa ubingwa wa Euro 2024 kwa kuifunga England 2-1. Nikiwa katika hali hiyo, 'hondo hondo' alinitumia nakala ya tangazo la mnada lililochapishwa na Gazeti la Mwananchi la 14 Julai 2024. Kuwa majengo na eneo lote la kilichokuwa Chuo Kikuu, SEKOMU yatapigwa mnada 15 Agosti 2024 ni jambo lililonishtua!
Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU) kilikuwa ni Chuo Kikuu cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Tanga. Jina la Chuo lilitokana Hayati Askofu Dkt. Sebastian Kolowa aliyekuwa Mkuu wa Dayosisi ya Tanga, Mkuu wa KKKT na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). Askofu Dkt. Kolowa alifariki mwaka 1992 nilipokuwa Kidato cha 5 Sekondari ya Azania.
Chuo hicho kilianza kwa heshima kubwa kwa mtaji uliotokana na sadaka za waumini pamoja na watu wengine zikiwemo taasisi za ndani na nje ya nchi. Uchunguzi wa kijamii (sociological analysis) niliyofanya imebaini kuwa Chuo hicho kilifungwa kutokana na mambo mbalimbali ya kisiasa zikiwemo siasa za Kanisa na pia siasa za nchi za wakati ule.
Siasa za nchi zilipotuama, siasa za Kanisa ndio kwanza zilikuwa zinatuama kwa kasi iliyokuwa ikiongezeka na hivyo Chuo hicho kukosa watu wa kukitia nguvu ili kiweze kufufuka. Palipo na umoja dhaifu hapawezi kuwa na nguvu au ari ya kukusanya fedha za maendeleo. Sio lengo la andiko hili kuwanyooshea watu vidole kwani na wao wameviona vidole vyao vikiwasuta pia.
Kwamba Mahakama imetoa amri ili mali zote za Chuo hicho zipigwe mnada. Bila shaka hii ni sababu ya madeni yasiyolipika. Lakini KKKT ni taasisi kubwa na yenye umoja unaopigiwa pia mfano. Misukosuko mingi iliyowahi kuikumba haikuweza kuitikisa ikiwemo ya Meru, Mwanga, Dar es Salaam, Mbeya, Rukwa, nk. Ni vizuri pia ikaeleweka kuwa mafanikio ya KKKT ni fahari yetu tulio katika mlengo wa Kiprotestanti lakini fedheha yake (kama ipo) ni fedheha yetu pia.
Hivyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa waumini wote wa KKKT nchi nzima kwa umoja wao pamoja na waumini wa makanisa mengine yaliyo na ushirika na KKKT kuungana ili kunusuru mali na majengo yote ya SEKOMU yasipigwe mnada. Jitihada hizo zilenge kutaka kukifufua SEKOMU ili kirudie hali yake ya awali.
Pia, tunatoa wito kwa serikali ione namna ya kusaidia kunusuru taasisi hiyo ambayo miaka michache iliyopita ilisaidia sana katika kutoa wahitimu bora ikiwemo za Shahada ya Ualimu katika Mahitaji Maalum (Special Needs). Imani yetu ni kuwa andiko hili litachochea hamasa kwa Wakristo wa KKKT kutokuruhusu sadaka zao zipigwe mnada. Wapo Wakristo ambao pia Mungu amewabariki kwa mali, vipawa, uongozi na hata ushawishi katika jamii. Tunawaomba waumini hao watumie vipawa vyao kunusuru.
Tunaomba ujumbe huu usomwe pia na hawa wafuatao Malisa GJ, Tuli Mwambapa, Mwigulu Nchemba, Freeman Mbowe, Prof. Mwandosya, Mzee Kimei, Dkt. Harrison Mwakyembe, Rais Samia, Assah Mwambene, nk. Orodha ni ndefu lakini hawa tumewataja kama mfano tu. Kama kuna mtu ye yote atakayekwazika na andiko hili, basi aonyeshe hasira zake kwa kutafuta namna ya kunusuru mali za Kanisa zisinadiwe.
Inawezekana kabisa pesa zikapatikana kulipa wadai wa SEKOMU kukiwa na nia ya pamoja. Wito wa kusaidia SEKOMU isipigwe mnada humaanishi kuwa wadai wa Chuo cha SEKOMU wasilipwe, la hasha. Wito wetu ni kupatikana pesa ili wadai walipwe Chuo kisipigwe mnada. Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 15 Julai 2024; saa 8:12 usiku