Kwanini taasisi za kanisa zinapotengeneza faida waumini hatuhusishwi na wala hatunufaiki na lolote?

Kwanini taasisi za kanisa zinapotengeneza faida waumini hatuhusishwi na wala hatunufaiki na lolote?

mali za kkkt lazima zipukutike kwanza nyingi zilijengwa au kuanzishwa na wazungu waafrika kuziendeleza ni ngumu shule kibao zimepigwa mnada kwakua usimamizi ulikua mbovu shule kushuka kiwango mwishoe wazazi kutopeleka watoto ndio basi tena shule inaingia madeni inadaiwa inapigwa mnada..

kkkt kuna katabia ka kutamani madaraka kila mtu anataka awe zimba
 
Niliwahi kulisema hili
 
Kwahiyo watanzania tumekuwa mazuzu Kiasi cha kutojua kutofautisha imani na biashara?

Yani zile biashara za makanisa nayo ni sehemu ya imani?

Kwamba imani hairuhusu kuhoji biashara za haya makanisa?

Aisee! Tunakoelekea makanisa yatakuwa nikwajili ya watu wajinga tu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuelewa huu wizi unaoendelea huko makanisani
Mkuu ndio maana nikasisitiza IMANI haitaki matumizi ya LOGIC
Haijalishi upo Tz au Kenya au ulaya

Kwa mujibu wa IMANI ukitoa sadaka yako kwa Mwingira mkataba wako na Mungu unaishia pale utakapotoa sadaka...... habari ya sadaka Mwingira ataitumiaje sio jukumu lako

Utashirikishwa tu kutoa sadaka na sio kuitumia

Miradi(biashara) ya kanisa haipo kwaajili kutoa gawio kwa waumini, wajibu wako kama muumini ni kuendelea kutoa sadaka tu na sio kufuatilia sadaka inafanyiwa nini
Yaani mradi ukiyumba wewe endeleza mkataba wako na Mungu wa kuendelea kutoa sadaka ili siku ya mwisho uje kula naye bata peponi

Mkuu sipendi kutumia neno WAJINGA kwasababu itaonekana kama unawatusi waamini hizi dini
Ila ukweli ni kwamba makanisa yamejaa watu wenye akili zao timamu lakini wameamua kuacha kutumia akili hizo linapokuja swala la Imani

Wewe ukitaka gari nyumba mchungaji anakuombea ila yeye utoe sadaka apate nyumba na gari
 
Back
Top Bottom