Kwanini tabia za maisha ya kawaida ya viongozi wa Kitanzania wakiachia madaraka hubadilika?

Kwanini tabia za maisha ya kawaida ya viongozi wa Kitanzania wakiachia madaraka hubadilika?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kuna life style flani la viongozi wa kitanzania wakiwa maradakani huionesha jamii kupitia mitandao yao ya kijamii lakini punde wakishatoka madarakani style hiyo hupotea ghafla, labda waanze tena Leo baada ya Uzi huu!

Mfano;
  • Wakiwa madarakani utaona wakipost wapo jimu (gym) nakutufanya sisi wenye vitambi tuonekane ni wazembe sana
  • Wakiwa madarakani utaona wakifanya mazoezi ya kukimbia hata na wake zao (jogging) hadi sisi wengine huwa tunajiona wazembe
  • Wakiwa madarakani wanaonesha kusali na mahaba ndindindi hadi sisi wengine tunajiona wapagani
  • Wakiwa madarakani huona watu wengine kama hawajui maisha kwa kuwashangaa wengine kutokuona fursa (inje ya box)
  • Wakiwa madarakani kila maisha yao binafsi hutupia pichapicha
  • Wakiwa madarakani hushangaa RAIA kwanini hatufanyi utalii wa ndani
  • Wakiwa madarakani hutangaza wao wasamalia wema n.k
Sasa kwanini punde wakishatoka madarakani style zote hizo hukoma wakati ni maisha yao binafsi?
 
Public Relation (PR), image kujijenga kisiasa. Muhimu wakuone kwa mtazamo chanya
 
Na mbaya zaidi akili na maamuzi yao wakiwa madarakani ni tofauti kabisa wanapokua nje ya pie!na mifano ni mingi tu !
 
Sasa mazoezi ya kukimbia yanahusianaje na pesa

Kama huna pesa unaona hatazile dakika za mazoezi unapoteza Bora ufanye kibarua upate hata chumvi ya kupikia.umasikini Noma😂😂😂😂
 
Hakuna maisha ya upweke kama ya kutoka madarakani, kustaafu au kiongozi kwasababu marafiki wanapungua connection zinapungua depression is real.
 
Kuna meneja mmoja wa shirika X la umma,alipokaribia kustaafu alijiuzia gari vx.hajawahi kutembelea kwa miaka 7 sasa.juzijuzi aliliuza kwa jamaa wa kaskazini kwa Bei ya scrap.😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom