Wana bodi, kwenye kufanya utafiti wangu mkubwa nimegundua na kuona kwamba taifa la Nigeria limedominate Karibu mambo mengi sana mfano kwenye muziki Muziki na Wana muziki wa Nigeria ni maarufu sana Africa na duniani kwa ujumla mfano Wizkid, patoranking, chidinma, yemi alade, femi kuti, davido, Mr favour, falz, tiwa savage, don Jazzy, p square, kipengele cha pili ambacho Nigeria wame dominate ni Kwenye fasihi na sanaa itakuwa movies za Nigeria zinatamba Africa na duniani kote kutokana na waigizaji mahiri na wenye passion na moyo na kazi yao mfano Hawa vijana Kama kina Aki na ukwa etc, kwenye uwanda wa Fasihi kwa Hapa Africa Nigeria imebeba wana fasihi wakubwa na mahiri mfano Huyu Wole Soyinka ambaye ni Mshindi wa tuzo ya amani ya 'Nobel Prize ' kwenye fasihi mwaka 1986, Mwingine ni huyu Chinua Achebe Wengi wetu tumemsoma kwenye 'Things Fall apart ' ni mwana fasihi aliyetukuka na kuheshimika
hapa barani Africa,
Kwenye kipengele cha michezo hususan mpira Nigeria wenyewe mnaona 'super eagles ' wakiingia Mara kadhaa kwenye kombe la dunia,
Kipengele kingine ni mabilionea Nigeria kuna mataycoon maarufu sana mfano tajiri Aliko dangote, Mike Adenuga, Alakija
Kipengele cha idadi ya watu Nigeria wanaongoza hapa Africa wapo milioni 200+
Kipengele kingine cha Uchumi nigeria wanawongoza hapa Africa
Kipengele kingine japo sio cha muhimu ni kwamba makabila ya Nigeria ni makubwa sana yaani yana idadi kubwa Sana ya watu mfano Wahausa, Yoruba etc
Hebu tujadili why Nigeria hawa wame dominate mambo mengi sana kiasi cha kwamba kuonekana Hawa wanaigeria kuonekana wao Kama hawapo Africa vile wao ni level ya mataifa makubwa duniani!
Nb Nigeria ni moja ya nchi ambazo Hapa Africa wamepinduana Sana /marais wamepinduliwa sana!