Kwanini TANESCO hawatekelezi STIEGLER'S Gorge project?

Mradi wa gesi ulikuwa na hela nje nje za bomba la kusafirishia gesi.

Hiyo HEP itawalaza njaa wapiga dili, japo ndio suluhisho la kudumu kwa upatikanaji wa Umeme kwa nchi yetu.

Mungu pekee atunusuru.
 


Kwa sababu Mzungu hataki, kumbuka kwamba 38% ya ardhi ya JMTZ ni Hifadhi kwa ajili Mzungu kuja kuwinda na kuangalia Wanyama, na namba inaongezeka siku hadi siku wakati wa Uhuru ilikuwa 17%!

Mwafrika ni mutoto wa Muzungu!
 
Ngoja tumaluzue Chato International Airport.
 
Sijawahi kumuona mpinzani akihoji hili bungeni...
walihoji, Muhongo akasema maji hayatoshi, water budget, blah blah blah blah blah blah. naona waithiopia wana maji mengi sana.
 
Mkuu VP hashtag ikianzishwa haiwezi saidia kweli?
 
Kumbe kulikuwa na haya, shukurani kwa kuibua habari hii. Itakuwa vizuri

Labda hii pia ni moja ya yale makaburi Mkulu hataki hata kuyafukua.

Wathubutu kuutekeleza wakione kilicho mtoa kanga manyoya, ni wazi kibarua chao kitakuwa katika hati hati, kwani umeisahau serikali yetu kwa kuwamwaga watumishi wao tena kwa gafla gafla???

nawashauri wasithubutu, wajifanye tu kama hawaujui vile huo mradi
 
Ila kufanya kazi TANESCO ni nusu peponi eeh! Dili nje nje!
 
Bado mnaamini kwenye miradi ya maji? mmejifunza nini kutoka Mtera na Kidatu? kumbuka wakati wanawekeza huko maji yalikuwa ya kumwaga leo hii ikifika kiangazi tunatafutana.

Tuwekeze mabilioni Rufuji, alafu miaka kumi baadae tuanze kujuta...na mtakuja hukuhuku mtandaoni kulamu huo uwekezaji.
 
The project is Still viable Serikali inakwepa miradi yenye uwekezaji mdogo kwa Sababu tu ya Ubinafsi
Ukisema serikali unakosea bora useme baadhi ya watu wenye positions za kufanya maamuzi....Yaani serikali iache miradi ya bei rahisi? Ili iweje? 10% mjomba ndizo zizlizo sababisha yote haya hadi wakaona wajiingize kwenye ujenzi wa majumba yasiyo na wakazi ili tu kuongeza ukubwa wa mgao....Tena bila huruma wala aibu kwa mtaji wa wazee wastaafu ambao wanalipwa kiduchu na viunua mgongo visivyokidhi haja....Sasa jiulize kama disposable income ipo kwanini hawawarejeshei wazee na wasiojiweza kama social objective ya mashirika hayo yalivyo?

Kama kweli ni wabunifu, si wangetafuta mitaji katika sector za uzalishaji kwakuwawezesha kwanza raia kuongeza tija kwenye uzalishaji ili hatimaye waweze kuwapa wao mitaji through mahitaji yao ya nyumba? Utagundua kuna kitabia cha wizi kimejificha nyuma ya chaka la kuleta maendeleo...Bila tathmini watu hao ndiyo wanapigiwa makofi kwamba wamefanya vyema...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…