Kwanini Tanganyika ilikufa na Zanzibar ikabaki?

Kwanini Tanganyika ilikufa na Zanzibar ikabaki?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Huu muungano huu kiukweli pamoja na kusoma kwangu shule zote sijawai kupata majibu kutoka kwa wanasiasa au walimu wanaofundisha !

Nina maswali wataalamu naomba mnijibu

Tanganyika iko wapi?

Mbona Zanzibar ipo?

Kwanini Zanzibar utoa Rais wa Tanzania wakati Tanganyika haiwezi kutoa Rais Zanzibar?

Kwanini watumishi wa umma wa Zanzibar wanaweza kuja kufanya kazi bara bila shida lakini watumishi wa Tanganyika hawawezi kwenda kufanya kazi Zanzibar?

Kwanini watumishi wa vyama vya siasa wa Zanzibar wanaweza kuja bara kufanya kazi lakini wa Tanganyika hawawezi kwenda Zanzibar kufanya kazi?

Kwanini bendera ya Tanganyika haipo lakini Zanzibar wana bendera?

Kwanini Zanzibar Wana Rais lakini Tanganyika haina Rais ?

Kwanini Zanzibar Wana budget, bunge, na mifumo yote ya kiserikali lakini Tanganyika hakuna !

Watanganyika kuishi Zanzibar na kumilki kiwanja hakuna ila wanzanzibar wanamiliki kila wakitakacho kutoka bara?

Tanganyika iko wapi? Imepokwa kwa maslahi ya Nani?kwenye majibu ya hayo maswali anisaidie ??

Where is Tanganyika?

Pia soma
- Tanganyika imezikwa kwenye kaburi la Muungano, haiwezi kuvaa koti la Muungano
 
CCM ni watu hatari Ndio walioharibu muungano Kwa maslahi ya chama Chao sio maslahi ya taifa ,Kwa mfano Leo Zanzibar wanakatiba yao ambayo inapingana na Jamhuri ya muungano halafu CCM wamekaa kimya kabisa kana kwamba hawajui wenzao huko unguja wamebadilisha,kifupi huu sio muungano,duniani kote hakuna muungano wa aina hii
 
mh! acheni kutafuta sababu sababu ni fikra duni kuwaza hivyo!
 
Mimi nafikiri huu muungano ilitengenezwa kwa sababu za kiusalama kwa ajili ya Tanganyika na ilibidi Karume ashawishiwe kwa staili hiyo na kitu kikubwa alichonyimwa ni vyombo vya ulinzi na usalama. Ukiangalia kwa undani Tanganyika bado ipo na ndio tunasherehekea uhuru wake leo ila kwa kivuli cha Tanzania.
 
Zanzibar ilipaswa kutawaliwa na Tanganyika kimabavu yote haya ya "Sababu za kiusalama" yasingekuwepo.
 
It all begani with Nyerere.

Kuliko kuachia Madaraka, CCM kwao ni bora nchi ipotee au hata irudishwe kwenye Ukoloni.
Ili kuendelea kutawala, Nyerere aliona ni bora amuachie Uwaziri Mkuu Kawawa ili yeye abaki kuongoza Chama na kum control na kumuendesha Waziri mkuu.

Kuliko kuongoza Tanganyika na Zanzibar zenye serikali zake, akaona ni heri aiue ya Tanganyike ili yeye awe wa Muungano usio na Tanganyika.

Akaja kuona ili iwe rahisi zaidi dawa ni kuunganisha vyama vya Tanganyika na Zanzibar , na yeye kama rais wa Muungano atakuwa na power over Zanzibar kwa kofia ya uenyekiti wa Chama
 
Hapo ndio watanzania watambue Mwl.Nyerere ni akili kubwa sana. Kwa muundo wa jiji la Dar kabla ya kuvunjwa na Rais Magufuli, jiji halikuwa na eneo la kiutawala kitu ambacho kilipelekea malalamiko mengi ya gharama yaliyopelekea kuvunjwa kwa muundo huo Ila hiki mwalimu alikiona miaka mingi iliyopita.

Kama mwalimu asingefikiria alichofikiria leo tungekuwa na Tanganyika, Zanzibar na JMT na mbaya zaidi JMT ingekuwa inaendeshwa kwa gharama kubwa bila kuwa na eneo la kiutawala. Kama gharama za kuendesha jiji zilikuwa kubwa je gharama za kuendesha nchi ingekuwaje?

Ndio maana katika kupunguza gharama Rais wa JMT ni Rais pia wa Tanzania ndio maana uchaguzi mkuu tunamchagua Rais wa Tanzania lakini kwa nafasi yake Kama Rais wa Tanzania anakuwa Rais wa JMT.

Mpaka hapo unaona Tanzania na JMT ni vitu viwili Tofauti na Tanganyika ilibadilishwa kuwa Tanzania na sio JMT
 
Huu muungano huu kiukweli pamoja na kusoma kwangu shule zote sijawai kupata majibu kutoka kwa wanasiasa au walimu wanaofundisha !

Nina maswali wataalamu naomba mnijibu

Tanganyika iko wapi?

Mbona Zanzibar ipo?

Kwanini Zanzibar utoa Rais wa Tanzania wakati Tanganyika haiwezi kutoa Rais Zanzibar?

Kwanini watumishi wa umma wa Zanzibar wanaweza kuja kufanya kazi bara bila shida lakini watumishi wa Tanganyika hawawezi kwenda kufanya kazi Zanzibar?

Kwanini watumishi wa vyama vya siasa wa Zanzibar wanaweza kuja bara kufanya kazi lakini wa Tanganyika hawawezi kwenda Zanzibar kufanya kazi?

Kwanini bendera ya Tanganyika haipo lakini Zanzibar wana bendera?

Kwanini Zanzibar Wana Rais lakini Tanganyika haina Rais ?

Kwanini Zanzibar Wana budget, bunge, na mifumo yote ya kiserikali lakini Tanganyika hakuna !

Watanganyika kuishi Zanzibar na kumilki kiwanja hakuna ila wanzanzibar wanamiliki kila wakitakacho kutoka bara?

Tanganyika iko wapi? Imepokwa kwa maslahi ya Nani?kwenye majibu ya hayo maswali anisaidie ??

Where is Tanganyika?

Pia soma
- Tanganyika imezikwa kwenye kaburi la Muungano, haiwezi kuvaa koti la Muungano
Ujinga na upumbavu wetu.
 
Ndio maana sasa wanahakikisha sherehe za Uhuru wa Tanganyika hazifanyiki ila Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kufanyika zikitanguliwa na mashindano ya Kombe la Mapinglduzi zenye kushirukisha timu kadhaa zikiwemo Simba na Yanga ambazo zimetufanya Watanganyika kuendele kuwa wajinga.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom