Kwanini Tanganyika iliuhitaji zaidi Muungano kuliko Zanzibar?

mwanaume si ndo analipa mahari, anajenga, anamuhudimia make wake mahitaji mbali mbali,

ni kama vile Tanganyika ilimuoa Zanzibar
 
Zanzibar wasomi wake wengi miaka hio walikwenda Russia(Soviet union) na Cuba hofu ya Uingeraza. Ikaona Zanzibar itakuja kuwa sababu kuu ya kushawishi nchi za East Africa kuwa communist nao.
sasa kama ndio hivyo mbona baada ya muungano Nyerere akadeclare ujamaa policy ambayo ni ucommunism na hiyo zanzibar ndio iliugonea huo ujamaa na wakawa wa kwanza kuachana nao kabla yetu??
 
kama wakitaka muungano huu uendelee, watatue kero za watanganyika,
 
Halafu Tambua kabisa kwenye huu muungano Wananchi hawakuhusishwa.
unaposema wananchi hawakuhusishwa unatakiwa ujue nchi ilikuwa katika haki gani, enzi hizo unaambiwa dar tu ilikuwa na watu hawafikii lako tano, watu wapo vijijini, wengine kiswahili hawajui wala serikali hawajui ndio nini, kwenda morogoro tu unalala njiani,

kwa hali hiyo wangeweza vipi kufanya michakato ya kitaifa kiwepesewepesi tu? ilibidi iwe kama ilivyokuwa,
 
udini udini udini, kwanza kinachowafanya mfikirie sana tanganyika wakati huu ni kuona Rais mzanzibari na muislamu anayejitambua ndio roho zinawauma, na wazanzibari washikilie hapohapo wasiachilie
 
Nyerere anapenda sifa,alitaka ndo awe Rais wa Jamhuri ya Muungano. Unajua kwa nini Africa walishindwa kuungana?

Moja ya sababu ni personal ambitions. Nyerere alitaka ndo awe Rais wa Muungano wa Africa huku Nkurumah nae anataka.
I admire your candor.
 
na walifikiri wazanzibari ni mbumbumbu,

hawakuzingatia kuwa ijapokuwa sultani alikuwa ni muarabu, himaya yake ilijitanabaisha kama taifa, wananchi wake walikuwa raia

tofauti na bara ambayo ilikuwa koloni na raia wake kwa mantiki hiyo walikuwa ni kama wana uraia wa malkia
 
Hili wazo la kuifanya zanzibar mkoa, Nyerere angeanza nalo. Leo tusingekuwa tunapoteza muda kujadili jambo hilo.
muungano ungekuwa umekufa zamani sana.

wazanzibari walianza harakati za kukataa muungano tangu enzi hizo za karume

bila kutongozwa na muungano jinsi ulivyo wasingekubali
 
Naomba kuuliza, mana mimi najaribu kutumia nadharia za kihistoria kwamba Zanzibar na Tanganyika ziliungana hasa kwa sababu za kiusalama kwa wakati huo.

1. Baada ya Waafrika wakiongozwa na Mganda John Okelo kumpindua Sultan wa Zanzibar (Mwarabu kutoka Oman), je Karume angeweza kuendelea kutawala kwa uhuru bila kuungana na Tanganyika?

2. Je, baada ya Sultan kupinduliwa na Zanzibar kuanza kujitawala, je, Sultan hakuwa na mpango wa kurudi Zanzibar kwa nguvu endapo isingeungana na Tanganyika? Wazanzibar Waafrika wangeweza kujilinda wao wenyewe bila Tanganyika?
 
Yaani maadui wa Nyerere washindwe kutumia nchi ambazo zimepakana na Tanganyika, kama Ziaire, Rwanda, Burundi na Kenya, waamue kutumia kakisiwa ambako kapo mbali kabisa na Tanganyika?

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣​
 
Ndo ushangae hawa hawajui kuwa Nyerere alitaka kuungana na Kenya pia.Sema Jomo Kenyata alikataa.Si Kenya tu yaani almost nchi zote majirani .Na ndoto yake kubwa alita Africa yote iungane ila yeye ndo awe Rais.All in all ambition kubwa ya Nyerere ilikuwa ni yeye kuwa Rais wa watu wengi.
 
Wanaokerekwa na huu muungano wangejikusanya wakafanya kweli lkn hii kupiga makelele hapa jf haitasaidia chochote maana nyuzi za aina hii za kupinga huu muungano haujaanza leo sasa kwanini msiamue kufanya kweli mkaacha kuimba hiz taarabu kila siku
 
Katika utamaduni ambao watanzania hawakujengewa ni ule wa kupenda kusikia ukweli ambao hawaupendi. Nyerere was a good leader, but he had issues with EGO.

The old man had a BIG EGO, the size of a Grand Canyon.​
 
Kila mara mmeshaambiwa kule Zanzibar ni Nchi ndogo, maana yake na Ardhi ni ndogo pia ,

Mnasema Muungano hauna faida kwani nani anayemg’ang’ania mwenzake ??!

Muarobaini wa huu Muungano ni kuwepo na Serikali tatu kwa sababu kusema kwamba iwepo Serikali moja hilo Wazanzibari hawataki hata kulisikia !
Kwa sababu wanaamini kutokana na uchache wao wakikubali watakuwa wamemezwa kabisaaa !
 
basi tuambieni, kitu hata kimoja tu ambacho watanganyika wanafaidika na muungano. taja kimoja tu.
 
basi tuambieni, kitu hata kimoja tu ambacho watanganyika wanafaidika na muungano. taja kimoja tu.
Kama wewe na mimi hatufaidiki chochote na huu Muungano ujue wapo Watanganyika wengine wanafaidika sana na huu Muungano na wanafanya maombi kila siku huu Muungano uendelee kudumu 😅🙏🙏 !
 
sasa kama ndio hivyo mbona baada ya muungano Nyerere akadeclare ujamaa policy ambayo ni ucommunism na hiyo zanzibar ndio iliugonea huo ujamaa na wakawa wa kwanza kuachana nao kabla yetu??
Hakukuwa na ucommunism kwa Nyerere bali Usoshalist !
Socialism = Ujamaa = sote ni dugu moja hakuna kunyonyana hapa 🙏🙏😅 .
Wajanja wakaona maisha gani haya bila kunyonyana ??!
Kila mtu apambane na hali yake !!
🙏🙏.

Wakati ule wa Cold War ya NATO na USSR jamaa walikuwa wanawahiana katika zile sehemu walizoona wao ni strategically kwa mambo yao ya Usalama !
Kila mmoja alitaka awahi kuidhibiti sehemu aliyoiona ni muhimu kwa mambo yake !
Lakini zote hizi ni Speculations tu na zitaendelea kuwa ni Speculations tu !
All in all Waswahili walisemaga Umoja ni nguvu na Utengano ni Udhaifu !

Tuulinde Muungano wetu 🙏🙏
 
Huu mpango ulishindikana ila znz ipo siku itanyakuliwa kinguvu tu maana tukiwaacha hawa magaidi watajazana huko ndo jwtz itachukua mazima
Endelea kuota ndoto za Ali Nacha. Wewe unaisikia tu Zanzibar kutoka pande hizo. Tupo tunasubiria.
 
Umenena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…