Kwanini Tanzania haiko tayari kunakili mfumo wa maendeleo ambao tayari umeonekana kufanikiwa katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya na Amerika/US?

Kwanini Tanzania haiko tayari kunakili mfumo wa maendeleo ambao tayari umeonekana kufanikiwa katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya na Amerika/US?

Mfumo ambao Tanzania unaweza kuunakili na kufanikiwa ni mfumo wa China tu kwa sababu katika kipindi cha ukuaji wa kimaendeleo China na Tanzania hatujapishana sana yaani maendeleo haya yaliopo China ni ya miaka 20-30 tu hivyo tukijifunza kutoka kwao itakuwa ni rahisi kuwafikia ila kwa Marekani na Ulaya mifumo yao imejengwa kwa karne kadhaa na huwezi kutumia mfumo wa karne kadhaa na ufanikiwe kufika walipofika
 
Maendeleo yatakuja yenyewe endapo kodi zetu zitatumika vizuri.
 
Huwa najiuliza sana hili swali lakini sipati picha majibu kabisa..

Mfumo wa utawala, sheria, elimu, miundo mbinu, jamii, n.k. ni mzuri sana ukilinganisha na nchi ya Tanzania.

Kwanini?
Fuatilia dunia kwa undani. Hakuna maendeleo yaliyopatikana kwa mifumo. Maendeleo yamepatikana kwa:
1. Vita
2. Uporaji
3. Ugunduzi
4. Uvamizi.
 
Kuna shida gani kuwa na mahakama Huru?
Kuna shida gani kuwa na tume huru?
Kuna shida gani kuwa na chaguzi huru?
Kuna shida gani kuwa na utawala bora na uwajibikaji wake?

Hizo ndio basics za ku copy and paste. Mengine yatafuata na yataletwa na viongozi bora waliopatikana kutoka mifumo bora ya utawala.
Nani alikwambia ulaya na Marekani kuna ukamilifu huo unaoufikiria? Nani alikwambia Marekani kuna chaguzi huru? Unajua kuna aina ngapi za kura hadi anapatikana Rais wa Marekani?
Nani alikwambia Marekani na Ulaya kuna Mahakama huru? Umewahi kuona mara ngapi viongozi wa nchi zenye uchumi mkubwa Duniani wamewahi kushtakiwa, kutiwa hatiani na kupata adhabu kutoka Mahakama ya ICC?
Fikiria nje ya box mkuu, usidanganywe na tiles za juu ya kaburi ilihali ndani kuna mifupa iliyooza
 
Hatuna viongozi wenye utashi. Kiu yao ipo ktk kujitajirisha tu.
 
Watu Huwa wanaamini ni vigumu kuwatawala watu waliosoma, lakini sivyo hamna kazi ngumu kama kuwatawala watu wenye maendeleo. Yaan upate maendeleo tushindwe kukutawala
 
Back
Top Bottom