Kwanini Tanzania hakuna viongozi wenye “Vision and Charisma” tena wadogo?


Ni kweli mazingira ya sasa yanawabana sana mbavu viongozi. Ni lazima upate OK ya jumba jeupe for everything. Lakini bado nadhani viongozi wenye charisma wanaweza kushine na kufanya mapinduzi ya kiuchumi. Mfano mdogo ni Bwana Hussein Bashe na Anthony Mtaka - wanaonekana wana uelewa mpana wa majukumu yao na wana nia na uthubutu wa kufanya makubwa. Wanaonekana wa vision na charisma
 

Nakubaliana na analysis yako on the source of problem. Ni kweli watu wastaarabu hawawezi kuingia kwenye siasa hivyo kama nchi haina namna ya kuwatafuta na kuwatambua basi itabidi ku settle for these mediocre leaders. Hiii ndio maana watu wastaarabu kama Augustine Mahiga na Augustino Ramadhani hawawezi kugombe ubunge - too rough and dirty
 


Ushauri Mzuri. Actually hata mimi nadhani watanzania tunakosea kwa kutegemea sana uongozi na wanasiasa jambo ambalo sio sahihi. Hii ni kasumba na ndio maana unaona watu ambao wamewahi kua mawaziri wakuu kama Lowassa na Sumae bado wanahangaika kugombea nafasi za uongozi na siasa. Ni kasumba na ushamba

Nipatapo nafasi nitatoa mapendekezo kwa wizara kama 4 au 5 on how to bring revolutionary changes in their respective sectors
 
Wizara ya afya magonjwa sugu karne hii wanajenga Dispensaries
 
Wapo kibao mtaani ila hawajapata nafasi ya kuonekana
 

Tatizo kubwa ni kuwa asilimia kubwa ya wale wenye CHARISMA na VISION hawawezi kuwa wanasiasa. Hivyo wakati mwingine au wakati wote inabidi uchague THE BEST from THE WORST.
Uliza waliosoma kigoma sec na shy bush jinsi kigwangala alivyokuwa mbwiga.
Mfano mzuri ni Makonda a.k.a ....
mfano mwingine, ni zzzzz, ukimpigia simu CAG hapatikani na ukienda kwake hayupo unarudi twita kuwa wa kwanza kutoa taarifa kuwa ......
 
Viongozi, mfano wabunge, wenye vision wakianza kung'ara kwa kuikosoa serikali bungeni, wanapewa vyeo vya unaibu waziri serikalini, wanafungwa mdomo na kanuni ya "collective responsibility" inayowakataza kuisema vibaya serikali waliyomo.

Wanaisema katika vikao vya ndani, na huko wanapigwa daflao la kanuni ya "wengi wape".

Mwishowe wanachoka na kutumia kanuni ya "if you can't beat them, join them".

Mfano wa karibuni ni Hussein Bashe.

Tafuta video za Bashe alivyokuwa backbencher bungeni uone alivyoichachafya serikali kwa data za bluebooks kama analala library.

Halafu linganisha na Bashe wa sasa hivi Naibu Waziri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nakubaliana na wewe especially upande wa kina mama. Waliopo kwenye siasa uwezo wao ni mdogo sana. Wenye uwezo hawapendi siasa. hivyo inabidi kuchagua among the few mediocre ones
 


Ni kweli

Hata mzee njelu kasaka alinyamazishwa kwakupewa unaibu waziri. Mrema walitaka kumnyamazisha kwakumpa unaibu waziri mkuu but it did not work
 
Mkuu upo sahihi kwa kiasi fulani. Nionavyo mimi watanzania tulio wengi hatufahamu majukumu ya waziri na mipaka yake ya kiutendaji. Pia ripoti za maendeleo ya wizara yanayotokana na waziri mwenye dhamana hatuna.

Hii inasababisha kutoona kazi za mawaziri au jitihada wanazofanya. Ki ukweli wengi wa viongozi wamebweteka na nafasi walizonazo ila baadhi wanapiga kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Intelecuals wengi hawana kadi wala utashi wa siasa za aina iliyopo! Visionaries wengi ni opposition wa oppressing mornachies, soma historia ya kina Sankara, Obama na kina J.J Rawlings hata JK Nyerere .
 
Sahihi Mkuu Ngwanakilala
Watawala wa siku hizi wala si Viongozi wa siku hizi, hapa ndipo shida inapoanza.

Zamani wakati wa Mwl Nyerere ilikuwa inatangazwa ' Rais Atahutubia siku fulani muda fulani sawa na siku ya Budget ilikuwa inatangazwa' kusema kweli watu walikuwa watafanya wafanyavyo kusikia Mkuu wa Nchi anasema nini. Siku hizi ni Usanii kwa kila jambo nani anataka kupoteza muda wa Kuwasikiliza hawa wahuni!

Hatuna viongozi tuna Wafanya Biashara aka Watawala hakuna charisma hapo itaanzia wapi kwa mfano!?
 
..Lion is tourism au Kigwangala is tourism?

..hilo bango ni kwa ajili ya utalii na simba, au kwa ajili ya Mh.Kingwangala?

Nimeshangaa sana kwanini picha yake iko pale. Is this the new breed of African leaders?
 

Hili nalo neno

Naona siku hizi itifaki hakuna kabisa. Full ubabe na kufoka foka. Vikao vya ndani hamna full kuaibishwa mbele za watu. Sidhani kama huo ni uongozi bora wenye lengo la kujenga - constructive and transformative leadership
 
Intelecuals wengi hawana kadi wala utashi wa siasa za aina iliyopo! Visionaries wengi ni opposition wa oppressing mornachies, soma historia ya kina Sankara, Obama na kina J.J Rawlings hata JK Nyerere .

Ni kweli watu kama Prof Assad wanaonekana outsiders kwenye current political arena
 
Nchi inaangozwa na chama waabudu mwenge mungu wao Nyamrunda ,Hawa ndio wawe na vision,wanaopata madarakani kwa human sacrifice..
 
Mzee una hoja kuntu, hoja zako zote zimekwenda shule, nimekuelewa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kwa mifano ya hao wawili

Na kingine ukifanya mambo kwa kujiamini na kwa weledi hata kama hutakuwa miongoni mwa wanakundi la kusifu na kuabudu lazima Boss wako atakuheshimu tu. Ilimradi umpe heshima yake tu.

Mtaka si miongoni mwa waimba masifu ya asubuhi na jioni ila nina uhakika ni miongoni mwa viongozi wanaoheshimika kwa Boss mkubwa

Siku moja kulikuwa na maadhimisho ya kitaifa mkoani kwake (nimesahau yalikuwa maadhimisho ya nini)

Kila aliyesimama aliishia kuimba masifu ya asubuhi hadi wakamaliza na ya jioni kabisa wakati jioni ilikuwa bado

Aliposimama Mtaka, hakuna cha masifu wala nini! Badala yake alitumia muda aliopewa kuelezea plan alizojiwekea kwenye mkoa wake

Alielezea namna pamba inavyoweza kuzalisha nguo humu humu ndani na soko la kwanza likawa wanafunzi, askari, na wafungwa

Akaelezea ngozi inavyoweza kuongezwa thamani humu humu ndani kwa kuzalisha viatu

Akaelezea mpango wake wa kiwanda cha chaki

Akaelezea namna anavyo target kujenga vyuo vya ufundi VETA Mkoani kwake na namna wahitimu watakavyonufaika kwa kufanya kazi kwenye viwanda vya nguo, chaki, ngozi nk

Kifupi alielezea vitu vingi sana ambavyo havikuwa vinachosha kusikiliza kiasi kwamba hata Mc wa shughuli ile hakuficha hisia zake

Na ukiangalia yote hayo kwa sasa yako kwenye vitendo

Tungepata watu kama hao wanaojua wanachofanya na kwanini wanafanya, hawa waimba masifu ya asubuhi na jioni kama masisita shirikani wangekaa pembeni wenyewe au wangejichagulia kanisa la kwenda kuimba masifu yao

2020 kama muheshimiwa atataka kuivusha Tanzania, inabidi atume kikosi kazi kitakachohakikisha hawa waimba masifu hawapati nafasi ya kupenya kwenye kura za maoni kuanzia nafasi ya ubunge hadi diwani

Waandaliwe watu smarter aina ya kina Mtaka, Bashe na wengineo maana naamini wako wengi ila kwasababu siasa zimekuwa uropokaji na figisu nyingi huamua kujikalia pembeni tu

Hao ndo wapenye ili tuwe na Baraza la mawaziri linalojitambua lisilosubiri kamera. Halafu mawaziri wasipowajibika wakutane na kibano cha wabunge smarter wa pande zote mbili

Kusiwe na wale wa ndiooo kwa kila hoja ya serikali na wabunge wa sioooo kwa kila hoja

Wawepo wabunge wa kusema ndio with reasons na sio with reasons! Na isiwe kwamba kuwa chama tawala lazima useme ndio na kuwa kambi pinzani lazima useme sio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…