Kwanini Tanzania hakuna viongozi wenye “Vision and Charisma” tena wadogo?

Kwanini Tanzania hakuna viongozi wenye “Vision and Charisma” tena wadogo?

Hili unalolitaka kwa ccm ya magufuli haliwezekani,Ccm ya magufuli inafaidika na hii product inayozalishwa sasa.Nchi yetu ina bahati mbaya kwa kuwa na hili kundi linaloitwa ccm
Akishatoka madarakani ndiyo anaaza kuona kama kuna sehemu alikosea na kuwa na uongo uongo mwingi kama anavyofanya mkapa kujifanya anaandika andika tujivitabu twa uongo ili baadhi ya watu wasahau madhambi yake na kumuonea sympathy.

Anajitibia nafsi yake maana siyo siri kama ilivyo pesa hata madaraka yanalevya na baada ya kuondoka madarakani, kuna vitu vinasuta nafsi na kumfanya mtu akose amani. Hivyo kuamua kuanza kujikosha kwa jamii na kwa kuwa unakuwa huna uwezo wa kupata platform ya kuongelea, njia pekee ni kujifanya unaandika tujivitabu twa majuto majuto kama anavyofanya mkapa mzee wa kiwira, NBC, nk nk. Kweli duniani wasanii wapo wengi!!
 
Brother viongozi wazuri wapo na visionary leaders wapo. Tatizo ni mfumo wa kuwagroom hawa watu. Kibongo bongo kuwa kiongozi mzuri unapimwa kwa mlengo wa siasa. Sasa Kuna watu potential sana nje ya CCM&CHADEMA ila hawana platform ya kuonekana.

Tubadili mifumo ya Nchi tu, japo jambo hili ni gumu sana kwa bongo. Hata hivyo kiasi fulani nampongeza kigwangala anajitahidi ukilinganisha na mawaziri waliomtangulia.



Sent using Jamii Forums mobile app

Hapa mkuu umenena. Mfumo wetu ni mbovu sana.
 
Kama viongozi wanazaliwa au kutokana 'na jamii ya watu wenye vision basi nao ndivyo watakavyokua, kama sivyo basi nao sivyo watavyokuwa.
 
Umeongea mengi ila kwa mimi ninavyo jua nchi yetu ilianza kuyumba baada yakutoka kwenye azimio la Arusha na kuja azimio la Zanzibar ambalo lilipelekea tuwe na vacum katika siasa za Tanzania yaani (ombwe la uongozi) sasa kukiwa na vacum inafanya hata mifumo isifanyekazi vizuri ndio hapo unakuta kazi ya kongosho inafanywa na moyo au kazi ya utumbo inafanywa na meno ndo kama hapo ulipoona waziri king`wangala anaenda kufanyakazi za kufunga mageti..kunasiku niliona hata Magufuli anaenda kukagua mafuta bandarini ...itaendelea.
 
Juzi Mh Rais alitoa siku 5 Waziri na Katibu Mkuu wizara ya Mali Asili wamalize tofauti zao,binafsi naliona suala hili ni mgongano wa kiutendaji Waziri ni Mwanasiasa anataka siasa ifanye kazi na Katibu Mkuu ni mtalaamu anataka utalaamu utumike matokeo yake kila mmoja ni mbabe je Wizara itaendelea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom