Kwanini Tanzania hakuna viongozi wenye “Vision and Charisma” tena wadogo?

Tatizo ni namna tunavyowapata hao viongozi wetu.watu wenye akili na wastaarabu wameshajiweka mbali na siasa hizi nyepesi na uchwara zinazofanywa Tanzania, tumebaki na wachumia tumbo tu.
 
Akili ndogo inapoongoza akili kubwa haya ndiyo matokeo..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bandiko zuri sana. Ila tatizo ni siasa ndugu yangu? Mtu hajawahi kumiliki kiwanda alaf unamfanya kuwa Waziri wa Viwanda. Binafsi ninaamini akiteuliwa mtu ambae amefanya kazi TTB kwa miaka kadhaa anaweza ongoza Wizara ya Utalii kwa ufanisi kabisa. Kama nilivosema mwanzo, tatizo ni siasa!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
nchi nyingi za kiafrika tuna shida kubwa...eti tunategemea utaalam utoke kwa wanasiasa!.
bahati mbaya wenyewe asilimia mia moja akili zao kiduchu walizojaliwa wameelekeza kwenye matumbo yao.
Wakipata fursa ya kushika kipaza sauti mwendo ni kusifia na kuabudu tu...huwa natamani hizo macrophone ziwakabe ni basi tu haitokei!!
yaani hadi kinyaa...mtu kama bashite, jerry muro (nimeandika majina yao makusudi kwa herufi ndogo!!)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli, na tumeshaongea humu sana tu. Watu wanafikiri uongozi ni kufanya ziara na safari za kushtukiza! Za nini? Kutoa matamko na kufokea watu ili tuonywesha kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku ya azam tv, ITV na tbc. Maujinga ya micromanagement na cheap populism agenda. Kutafuta misifa ya kishamba. Kiongozi unapaswa kuwa strategic,visionary and thoughtful sio kufanya kazi impulsively! Yataendelea kuimpress majinga menzao.
 
Nadhani kuna kasoro ilitokea sehemu katika mfumo mzima either wa elimu au kwingineko na inaendelea kuadhiri kila mtanzania kadiri siku zinavyosonga hali inazidi kuwa mbaya.

Siyo kwenye siasa tu ni karibia kila sehemu watu hawako innovative. Angalia taasisi nyingi za umma kama vyuo vikuu mfano udsm juzi juzi wameamrishwa kuwafukuza wanafunzi wasiokuwa na makosa. Nao bila hata kuhoji wamewafukuza kwa amri za wanasiasa tena hao udsm ni ma professors.

Kuna shida mahali, hata kwenye taasisi ndogo ndogo kama shule za primary na secondary mambo hayako sawa kama zamani na yanaonekana kuendelea kuharibika badala ya kuimarika. Mfumo wetu wa elimu unazalisha watu mbumbumbu zaidi wasioendana na ulimwengu wa sasa. Mtu anamaliza university awezi hata kujieleza achilia mbali kuhoji kwa sababu tu akitaka kujieleza/kuhoji chochote, waziri wa elimu anatoa amri afukuzwe chuo!!!

Kwa mfumo huu mbovu wa elimu unatawaliwa na wanasiasa wabovu utampata wapi viongozi wadogo wenye udhubutu wa fufanya mambo innovatively?
 
Uko sahihi sana
 
Tatizo ni namna tunavyowapata hao viongozi wetu.watu wenye akili na wastaarabu wameshajiweka mbali na siasa hizi nyepesi na uchwara zinazofanywa Tanzania, tumebaki na wachumia tumbo tu.

Ni kweli siasa zetu kwakiasi kikubwa ni majitaka
 

Hilo ni tatizo kubwa sana. Wanasiasa wasio na uzoefu au taaluma ya taasisi fulani kuwa viongozi wa taasisi hizo nyeti inaleta ugumu sana. Tumeona wenyewe jinsi zao la korosho lilivyo vurugwa na siasa
 

Hata Rais Mkapa kwenye kitabu chake kipya amesema anasikitika jinsi vijana wadogo wasio na mafunzo wanapopewa nafasi za uongozi bila kujiandaa wala kuandaliwa
 


Ni kweli mimi naona hata miaka 3 ya chuo kikuu ni michache sana. Watu wanaingia na kutoka wako vile vile hawajabadilika wala kuelimika
 
Ni kweli mimi naona hata miaka 3 ya chuo kikuu ni michache sana. Watu wanaingia na kutoka wako vile vile hawajabadilika wala kuelimika
Mkuu kwa hali ilivyo kwa sasa elimu inayotolewa vyuo vikuu vingi nchini Tanzania iko very diluted. Hata wakikaa miaka minne bado wanaweza wakatoka vile vile kama walivyoingia. Hakuna kitu cha maana zaidi ya kukaririshwa tudesa tusiyokuwa na maana yoyote. Ndiyo maana nikasema karibia taasisi nyingi hasa za elimu Tanzania ziko almost paralyzed.

Technical universities hakuna hata DIT wameivuruga sasa hivi haiko kama zamani, inavyatua tu degrees zile zile za kwenye makaratasi zisizokuwa na tija! Hata hizi wanazoziita so&so university of science and technology nazo ni magumashi ili mradi tu maisha yanaendelea.
 
Mleta mada umechambua na kutoa mchango wako vizuri kabisa mkuu.

Napenda kuongeza kuwa inabidi turejee ni namna gani viongozi wanasukwa na kutengenezwa. Kwa sasa ukiingia chama chochote cha siasa, iwe ni Upinzani au CCM utagundua kuna watu wamehodhi mamlaka na nafasi za ngazi za uongozi as if wao tu wapo entitled kuwa viongozi.

Kuna vijana wengi sana wapo visionary na wanauwezo ila hawapati hizo nafasi za uongozi sababu ya figisu na ukiritimba uliopo katika mfumo wetu wa kisiasa.

Leo kijana visionary ataingia ccm ili aweze kukwea nafasi za juu ila utaona sasa vikwazo atawekewa na vijana ambao wamekaa ccm tokea utotoni hadi vyuoni.

Yaani kukwea nafasi za uongozi Tanzania ni kama jeshi, kwamba lazima upitie vitani na maeneo tofauti kuonyesha mashiko yako na chama. Hii ni kikwazo sana kwa vijana ambao interest yao sio kufanya shughuli za vyama bali kupambania maendeleo na kuleta vitu vipya.

Mheshimiwa Rais magufuri ninampongeza sana kwakulijua na kulitambua hili na ndio maana alipoingia akawafumua watu wote wanaoleta siasa za makundi na mazoea.....

Teuzi zake zimehusisha hadi watu wa nje ya CCM. Hii tayari inaonyesha rais ana nia ya kuweka pandikizi ya wapenda mabadiliko na sio wanaokwenda kimazoea.

Watu kama akina nape nauye, January makamba, lizzy, polepole ni vijana ambao wapo kichama tu ila kichwani hakuna wanalolijua kuhusu far vision ya taifa. Huwa nawasikilizaga ila naona ni ujuaji tu upo mbele ila vichwani ni watupu wamekaa upigaji.

Hawa ambao Mheshimiwa Rais J. P. MAGUFURI amewateua ndio ambao wameonekana kuwa na afadhali ila sio kwamba ni the best. Ila ndio the only available candidates.... Ila ninachompendea magufuri ameshajua hayo mapungufu, ni katiba ya chama tu inamuangusha kuteua nje ya mfumo au hadi mtu awe mbunge ndio awe katika wizara kitu ambacho ni changamoto.

Katiba ingesema kazi za uwaziri ni za kuomba kama kazi nyingine aiser sidhani kama kuna ccm wangepata position awamu hii ya magu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Topic nzuri sana toka kwako mtoa mada.

Honestly; Tanzania tuna all it takes kutokuwa na maisha ya umasikini na ku-import mpaka leso, toothpick...

Tanzania tunahitaji viongozi wenye capacity ya ku-translate vison 2025 kwa vitendo na kimkakati bila kuwa selfish. Na selfishness ndiyo inawakwamisha baadhi ya viongozi na inturn kama taifa tunakwama.

Fikiria, wakati wa Rais Mkapa mmoja wa mawaziri akampa sumu JPM kwa kuwa aliitwa askari wa mwavuli.

Wakati wa Rais Kikwete, sote twakumbuka nini kilimkuta Mwakyembe mpaka nywele zikanyonyoka.

Sasa kwa hayo yaliyotokea yanatupa picha kama ndani ya cabinet kuna watu hawaivi, bila shaka sisi kama Taifa kuna wakati tunasahau ku-deal na our common enemies ambao ni ujinga umasikini na Maradhi na tunaanza kuharibiana au kuuwana.

We have very visionary leaders, but we also have leaders who have just happen to fill the vacancies but, upstairs hawana IQ ya kutatua matatizo ya Watanzania.

Sio ndani ya serikali hata kwenye vyama. Imagine, toka Nyerere atoke CCM nadhani inamiliki property zilezile achilia mbali majengo machache yalijengwa kwa deal kwenye same plots za CCM. CDM nao waliwahi kupewa na Sabodo 100% kujenga ofisi, badala hata ya kununua kiwanja mpaka leo imebaki kumbukumbu.

I wish tungekuwa na sort of panel, au Intelligence community inayoweza ku-scout people who are visionary to solve our problems whether wako serikalini au nje ya serikali.
Imagine watu kama Tesla, Google, Facebook, Uber hizi zote ni projects za private sector ambapo venture capitalist wamewekeza hela zao kwenye technology. In turn ajira zinazaliwa na USA inapata kodi za kutosha.

Leo hii, tuna mawaziri, ma-RC wangapi ambao wako tayari kukaa chini kuja na strategic investment projects ambazo zinaweza kutuvusha? Natumai wapo na kwa kuwa wapo ni wachache sana. Baadhi wana-rely kwa maafisa wa wizara ambao ni senior officers kuwashauri namna gani ya kuwekeza kwenye projects ambazo watavuta.
Imagine TAMISEMI. Kuna projects kibao za kujenga stand za mabasi. Hivi kama unaboresha maegesho ya mabasi kupita wakati collection ya mabasi ni ile ile, kwanini TAMISEMI wasingewekeza kwenye industrial projects kama kutengeneza mbolea za viwandani hata kama ni kwa ubia na private sector ya Watanzania. Tunajua mbolea na viwatilifu by almost 80% tuna-import.

Kwanini tusiwekeze hata kwenye kuzalisha raw milk ili kumuuzia Bakheresa ambae kwa siku viwanda vyake vinatumia lita laki 180 (lita 180,000x siku 300 x kiasi cha kununua 1,500) hii ni takribani bili 97.2 ambayo ingeingia kwenye mzunguko wa Watanzania; matokeo yake inakwenda India kununua maziwa ya unga.

Kuna wakati nimewahi kuandika hapa, kuwa kuna kijana anamtafuta Waziri wa uvuvi akiomba kukaa nae ili apate govt endorsement ili Tanzania iweze kuzalisha kwa ubia na serikali walau tani laki 180 za samaki. Tanzania tuna deficit ya tani laki 400 na tuna-agiza china. Simu ya waziri inaita haipokelewi, barua hazijibiwi na sio rahisi ku-gamble kwenda dodoma maana huenda Waziri akawa ziarani na hata ukifika huenda ukakutana na wangeni na siku nzima ikaisha bila mafanikio. Kama huo uwekezaji ungefanyika au ukifanyika ni sawa na mzunguko wa 1.6-1.8 tril kama kila samaki waa gram 500 atauzwa kati ya sh. 4,500 mpaka 5,000. Ukiongeza logistics za kuwasafirisha toka chanzo mpaka kufika sokoni kuna fedha nyingi sana itasambaa katika mikono ya Watanzania pamoja na kukuza lishe.
Yet hatujaamua kwenda soko la nje ya Tanzania kama Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Zimbabwe, South Africa. Hapa ni biashara ya fresh fish hatujagusa samaki wa maji chumvi.

Labda sisi hatuoni sawasawa; ila nasikitika kuona Rwanda ka-nchi kadogo kamekuwa na akili ya kuwekeza kwenye competitive advantage na kwa sasa kanavutia fedha nyingi kwa mikutano ya kimataifa, hotels kujaza watalii, hata michezo kama basket ball, kuitangaza kupitia Arsenal na PSG visit Rwanda.

Sasa, baadhi ya wasaidizi wa Mhe. Rais badala ya kuuza big picture ya nchi ambayo ni Tanzania,wao wako busy kuuza sura zao na baadhi wako busy kwenye instagram na kutukana watu kwenye twitter mambo ambayo hayana mashiko kwenye kutengeneza tija na kujenga uchumi wa kati.

Anyway, huenda kuna siku wakajua hili, ila wasijikute wanajua wakati kiza kimekaribia kuingia. Panapo jua kali ni wakati wa kufanya mambo ya maana
 
Uko sahihi Kabisa Freddie Matuja

Kwakua asilimia 80 ya watanzania wanajihusisha na kilimo basi almost asilimia 50 ya bajeti ya nchi ilitakiwa kupelekwa kwenye sekta ya kilimo na supporting infrastructures za sekta ya kilimo. Lakini naamini the truth is opposite. Furthermore Kilimo cha kutegemea mvua na jembe la mkono hakiwezi kumkomboa mkulima. Lazima twende kwenye kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha mashine. Uvuvi na ufugaji pia ni sekta ambazo zinaachwa zistawi zenyewe bila kupata enough support.

Nadhani vipaumbele vya serikali vina uwalakini mkubwa
 
Hasa majinga yaliyojazana ccm
 
wewe unazungumzia huyu Magufuli rais wa JMT na mfia ccm au unamzungumzia magufuli yupi?Hivi Bashite zaidi ya umatonya na ujambazi nini kingine anajua?je Muro na wenzake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…