Kwanini Tanzania hakuna viongozi wenye “Vision and Charisma” tena wadogo?

Hakuna Viongozi awamu hii...yani mpaka Rais wote ni shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda mwingine ili upate outcomes nzuri unaitaji kuwekeza fedha mfano kwenye sekta ya utalii, bandari na wizara nyingine karibu zote, ila cha ajabu licha ya kuwa budget ya fedha wizara zinazoomba ni chache lakini bado wanapewa OC's ndogo sana, chini ya 50% ya budget ya mwezi. Wizara ambayo naweza sema inapata zaidi ya 90% ni miundombinu. Unategemea wizara zijiendesheje? Ndio maana now days mawaziri na wakuu wa idara wanapishana ili mradi wapate allowance za kuendesha maisha yao badala ya kuja na strategic plan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Nakubaliana na wewe kuna aja ya kapanua wigo wa watu wanaonweza kua mawaziri. Sheria ibadilishwe rais aweze kuteua mtanzania yeyote mwenye zaidi ya miaka 30 na degree kua waziri.

Pia nakubaliana na wewe kua kazi ya uwaziri ingekua inatangazwa na watanzania wenye elimu ya chuo kikuu na uzoefu wanaruhusiwa kuomba na kufanyiwa interview ili kufanya selection based on merit, experience and expertise.

Pia naamini ubunge pia unahitaji term limit ya mihula 3. kama umewahi kuchaguliwa kua mbunge mara 3 usiruhusiwe tena kuwa mbunge ili kuondoa ufalme na ukiritima katika majimbo ya uchaguzi
 

Absolutely

Wizara zenye michango mikubwa zaidi katika katika pato la taifa ndio zilihitaji bajeti kubwa zaidi. Ikiwemo wizara ya kilimo kwakua asilimia 80% ya watanzania wanafanya sughul za ukulim,a ufugaji na uvuvi

Kinyume cha hapo ni kujaribu kukamua ng'ombe ambae humlishi
 

..Nakubaliana na wewe.

..kuna tatizo au changamoto ya kujieleza.

..tatizo liko ktk mfumo wetu wa elimu toka msingi mpaka chuo kikuu.

..naamini ni kwasababu watoto hawasomi vitabu vya aina mbalimbali. Hawafundishwi kuandika na kujenga hoja kupitia uandishi. Hawafundishwi kujieleza na kujengewa uwezo wa kujieleza. Hawafundishwi ushairi. Hawafundishwi kuigiza, na kuimba.

..kwasababu vijana wetu hawafundishwi yote hayo ndiyo maana unakuta watu wengi hawana nidhani ktk mijadala. Unaweza kukuta badala ya kujadili hoja iliyoko mezani wanamjadili mtoa hoja. Au wengi ni wepesi wa kutumia lugha mbaya wakidhani ndiyo maadili au " ustaarabu " ktk kujadiliana.

..pia kuna utamaduni mpya wa kutumia vitabu vya dini kujenga hoja ktk masuala ya kisiasa na kijamii. Hali hiyo pia inatokana na utamaduni wa kutokujisomea na kukosa udadisi wa kutafuta habari na maarifa kutoka vyanzo vingine.
 

Ni kweli tatizo la mfumo wa elimu ni kubwa sana

Ukitangaza nafasi ya kazi za entry level. Unaweza ukaletewa candidates ukawa interview ukakosa mtu. Ukaomba uletewe wengine ukawa interview ukakosa mtu. Vijana wenye degree hawana tofauti sana na high school graduates. Very poor. English na masuala ya Microsoft office asilimia 90 ni zero kabisa
 



Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiacha suala la mifumo wanasiasa wamegeuza siasa sehemu ya kutolea roho za watu. Unaweza kuwaza kuwasaidia wananchi ila watu wana interest zao ziko vested ukigusa mara umechukuliwa na wasiojulikana mara uchawi. Vijana wengi wanaona kuliko maisha ya kuishi usiku kwa kulala kwa waganga ni heri watafute maisha nje ya mfumo huu kandamizi usiojali vipaji wala elimu bali unamjua nani na nani na unamjua sangoma yupi na yupi.
 

Ni kweli kwasasa ili kushiriki siasa za ushindani ni lazima ujihusishe na mambo ya waganga na ushirikina. Jambo hili huwa discourage watu wengi wenye integrity
 
Kumbe hata ndugu Paschal Mayala alishawahi kubainisha jinsi ambavyo hayuko impressed na hawa mawaziri na viongozi vijana. Basi tatizo ni kubwa na liko wazi kwa wengi

 
Mawaziri na viongozi vijana kwakweli bado sana. Hawako tayari na hawaku stahili kupewa nafasi. Hapa tulikosea

 
Kudos mkuu umeongea ukweli. Hata debates siku hizi shule nyingi hazifanyi hata za private! Debates na mambo kama hayo uliyoyaeleza yakifanyika kuanzia levels za chini primary yanasaidia sana kumfanya mtu ajiamini na kuwa na udhubutu wa kuhoji au kujenga hoja kuhusu mambo mbalimbali. Kinyume chake siku hizi watoto wanamezeshwa ili wakati wa mtihani wacheuwe tu majibu, shule iongoze wapate wateja. Lakini ni wachache sana wanao weza kujieleza vizuri wakaeleweka hata kama wakiwa na performances nzuri. Tuna kazi kubwa ya kufanya kama taifa ili kuondokana na hii hali.
 
Hata Rais Mkapa kwenye kitabu chake kipya amesema anasikitika jinsi vijana wadogo wasio na mafunzo wanapopewa nafasi za uongozi bila kujiandaa wala kuandaliwa
Binafsi nadhani shida siyo vijana wadogo (wasiyo na mafunzo). Shida ni kitu hiki kinachoitwa "mtanzania". Sasa watu kama kabudi, ndalichako, kangi, nk wana udogo gani? Sema tu mfumo wetu wa elimu ndio mbovu, products nyingi za elimu yetu ni viini macho. Shida!!!!
 
Mkuu sio kwenye vyama vya siasa tu hata huku kwenye kazi zingine watu ni wale wale new entry ni chache sana,Ccm inatoa elimu hewa kwa watanzania na hivyo kupata wasomi vyeti kuliko maarifa,hata Magufuli ni PhD cheti ila maarifa sina hakika kama anayo,ndo maana alivyoingia ikulu yeye hakuhangaika na ujuzi au maarifa aliyonayo mtu bali cheti chake,I am so sorry for him
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni siasa.Viongozu wetu wanapatikana kupitia wanasiasa,na hao wanasiasa ndio watunga sera sheria na kanuni za kuwapata watendaji.Watendaji kazi yao ni kutekeleza na kusimamia sera zilizoandaliwa na wanasiasa unatarajia nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli. Tatizo letu haliko sehemu moja tu ya siasa ni kila sehemu. Na chanzo kikubwa cha matatizo ni hicho ulichokisema, elimu yetu ni mbovu na mbaya zaidi ni ya kuangalia cheti pasipo kuangalia maarifa/uwezo alionao mtu.

Pia mfumo wetu wa kufanya mambo wa toka juu kwenda chini (top - down) unawafanya wanaopewa madaraka hata kama ni matahira kufanya utahira wao watakavyo. Ndiyo maana jitu ni jinga na unaona kabisa linafanya ujinga lakini kwa kuwa labda lina mamlaka ya uwaziri basi linaamrisha kufanyika mambo ya kijinga na yanafanyika pasipo kuhoji, kwa maana ya kwamba ni "maagizo toka juu" Mfano mzuri ni wa ndalichako kuwafukuza wanafunzi/viongozi wa daruso pasipo sababu za msingi pale udsm!!!
 

Nadhami tunahitaji kua na mjadala wa kitaifa na kuibadili kabisa system yetu ya elimu. Ningependa kujua nchi nyingine za east africa wanatumia mitaala mipya ya elimu au ile ile aliyoacha mkoloni
 

Ni kweli mashirika mengi ya umma yanafanyakazi kupitia maagizo ya wanasiasa. Annual strategy ni ile ambayo waziri aliongea kwenye mkutano fulani akiwa ametoka tu nyumbani asubuhi kanywa chai na chapati kaja mkutanoni kufungua kitu fulani na mkasi wake. Kuna wakati national housing waliambiwa wajenge viwanda. nilishangaa
 

Yes hii top down approach inaathiri sana ufanisi wa mashirika na taasisi nyingi
 
Nadhami tunahitaji kua na mjadala wa kitaifa na kuibadili kabisa system yetu ya elimu. Ningependa kujua nchi nyingine za east africa wanatumia mitaala mipya ya elimu au ile ile aliyoacha mkoloni
Hili unalolitaka kwa ccm ya magufuli haliwezekani,Ccm ya magufuli inafaidika na hii product inayozalishwa sasa.Nchi yetu ina bahati mbaya kwa kuwa na hili kundi linaloitwa ccm
 
Nadhami tunahitaji kua na mjadala wa kitaifa na kuibadili kabisa system yetu ya elimu. Ningependa kujua nchi nyingine za east africa wanatumia mitaala mipya ya elimu au ile ile aliyoacha mkoloni
Hii uliyopendekeza hata mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, nadhani ndiyo njia sahihi kabisa. Lakini sasa wenye mamlaka sidhani kama wanadhani hili wazo lako lina umuhimu. Tunarudi kule kule kwenye mada kujiuliza ikiwa uwezo wa viongozi tulionao kweli utatufikisha kwenye nchi ya ahadi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…