Kwanini Tanzania hatufundishwi kuhusu 'ma-genius' maarufu wa Kizungu?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Sijui wengine labda ni mimi tu lkn mpaka namaliza Sekondari nilikuwa sijawahi kusikia chochote kuhusu William Shakespeare, yaani mtu kama angeniuliza kuhusu Shakespeare kipindi namaliza Sekondari nisingejua anaongelea nini, mimi nilifundishwa kuhusu Achebe, Ngugi wa Thiongo au labda Owino hao niliwajua kweli kweli, lkn baada ya kutoka Shuleni nimekuja kugundua kwamba nimenyimwa fursa ya kujua mambo mengi sana, mfano nilikuwa sijawahi kusikia kuhusu musical genius kama Mozart, Beethoven, wanafalsafa magenius kama akina Nietzsche na wengineo.

Naelewa kuna umuhimu wa Uafrika tukiwa kama Waafrika, lkn genius ni genius tu na haijalishi ni Mwafrika, Muzungu au Mchina, tuwajue wote na tunufaike nao, bila ya jitihada zangu binafsi ningebakia kama Watanzania wengi wanaishi mpaka wanafariki hawajawahi kupata bahati ya kumsikiliza Beethoven au kumsoma Shakespeare, ...
 
Watunzi wa mtaala wa Tanzania wenyewe na watoto wao hawatumii huo mtaala kwahiyo hawana muda huo.

Na pia waafrika tuna vijiroho mbaya na ubinafsi.

Baba yuko tayari adhurumiwe mali na wahuni kuliko kumwachia mwanae, utasikia itabidi uteseke kama mimi.

Magufuli hajui Kiingereza, Sasa badala kutia nia na kuboresha mazingira ya ualimu yeye anapobda, hataki anataka watu wote wawe wajinga kama yeye.
 
Wote hao wako overrated hata huyo Mozart hamna kitu
Kinachofanya Mozart awe exceptional ni vile alianza mziki akiwa mdogoo sana. Ndani ya muda mfupi alikua ameshakua na mafanikio makubwa katika muziki
 
Naam nilisoma kuhusu hiyo history yake ..lakini huo mziki unao zungumziwa kwamba ulikuwa unakonga nyoyo za watu na mpaka leo bado unakonga hizo nyonyo hata siuoni ... Labda nikwakuwa Ni miaka mingi Sasa imepita na mziki umepitia mabadikiko makubwa ya kiteknolojia na kwa Wakati wao Aina ya mziki aliokuwa anapiga ndio ilikuwa flavor zao
 
Ila Mozart Naona Kama Yuko overrated sana

Labda ukitaka kuelewa ugenius wa Mozart sikiliza kazi zake halafu tambua kwamba alizaliwa miaka ya 1700 na mpaka leo hii mziki ni kama umepangiliwa jana, ...
 
Nimeshasikiliza sijaona chamaaana ...labda uniambie ujuzi wake wa upigaji ala za music akiwa bado mdogo. Lakini hayo mengine Naona kawaida tu
 
Watunzi wa mtaala wa Tanzania wenyewe na watoto wao hawatumii huo mtaala kwahiyo hawana muda huo.

Na pia waafrika tuna vijiroho mbaya na ubinafsi.

Baba yuko tayari adhurumiwe mali na wahuni kuliko kumwachia mwanae, utasikia itabidi uteseke kama mimi.

Magufuli hajui Kiingereza, Sasa badala kutia nia na kuboresha mazingira ya ualimu yeye anapobda, hataki anataka watu wote wawe wajinga kama yeye.
👍👍
 
Kinachofanya Mozart awe exceptional ni vile alianza mziki akiwa mdogoo sana. Ndani ya muda mfupi alikua ameshakua na mafanikio makubwa katika muziki

Siyo hiyo tu, kumbuka Mozart alifanya kazi zake zaidi ya miaka 200 iliyopita na mpaka leo ukisikiliza utafiri ni wa jana, ...
 
Nimeshasikiliza sijaona chamaaana ...labda uniambie ujuzi wake wa upigaji ala za music akiwa bado mdogo. Lakini hayo mengine Naona kawaida tu

Yupi labda ungeweza kumfananisha naye? Wakati mwingine ni vizuri kulinganisha , ...
 
Naam nilisoma kuhusu hiyo history yake ..lakini huo mziki unao zungumziwa kwamba ulikuwa unakonga nyoyo za watu na mpaka leo bado unakonga hizo nyonyo hata siuoni ... Labda nikwakuwa Ni miaka mingi Sasa imepita na mziki umepitia mabadikiko makubwa ya kiteknolojia na kwa Wakati wao Aina ya mziki aliokuwa anapiga ndio ilikuwa flavor zao
Ok. Mtu gani unaona ww alikua genius kuliko yoyote
 
Siyo hiyo tu, kumbuka Mozart alifanya kazi zake zaidi ya miaka 200 iliyopita na mpaka leo ukisikiliza utafiri ni wa jana, ...
Binafssi mm namkubali sana Mozart kwa umri wake alijitahidi sana
 
Back
Top Bottom