Kwanini Tanzania inapaswa kubadilisha jina lake kuwa la Kiswahili?

Jina la nchi lina umuhimu mkubwa wa kitamaduni, kihistoria, na kitaifa. Linahudumia kama ishara ya utambulisho, umoja, na fahari kwa wananchi wake.
Mfano wa orodha ya baadhi ya nchi na lugha zao:- zinazohusiana:
Ufaransa - Kifaransa
Ujerumani - Kijerumani
Hispania - Kihispania
Italia - Kiitaliano
Japani - Kijapani
China - Kichina
Urusi - Kirusi
Ugiriki - Kigiriki
India - Kihindi
Saudi Arabia - Kiarabu
Korea Kusini - Kikorea
Uturuki - Kituruki

Orodha hii inaonyesha jinsi nchi nyingi zinavyokuwa na majina yao yakihusiana kwa karibu na lugha yao kuu, jambo linaloimarisha utambulisho wao wa kitamaduni na kitaifa.

Faida zitokanazo na kubadili Jina la Nchi ya Tanzania kwenda Nchi ya Swahili:-
Utambulisho wa Kitamaduni na Fahari, Lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa ya letu na ni msingi wa utambulisho wa kitamaduni wa nchi hii. Inazungumzwa na kueleweka na wananchi wengi wa Tanzania, Kuchukua jina la Kiswahili kwa nchi kungeakisi na kusherehekea umoja huu wa lugha na kuhamasisha fahari na utambulisho wa kitaifa.

Umuhimu wa Kihistoria.
Jina "Tanzania" lenyewe ni mchanganyiko wa "Tanganyika" na "Zanzibar," maeneo mawili yaliyoshirikiana kuunda nchi hii mwaka 1964. Wakati jina hili linavyoakisi muungano wa kihistoria, limetokana na nomenklacha ya kikoloni. Kubadilisha jina kuwa la Kiswahili kungeashiria hatua ya kuachana na urithi wa kikoloni na kukumbatia urithi wa kiasili.

Utambuzi wa Kimataifa.
Jina la Kiswahili lingeitofautisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa, na kuonyesha urithi wake tajiri wa kitamaduni na lugha.

Umoja wa Kitaifa.
Katika nchi yenye utofauti kama Tanzania, kuimarisha umoja wa kitaifa ni muhimu. Jina la Kiswahili lingetumika kama kiunganisho kinachounganisha makabila mbalimbali na kama ishara ya urithi wa pamoja wa lugha na utambulisho wa pamoja wa watu wa Tanzania.

Uendelezaji wa Lugha.
Kwa kuchukua jina la Kiswahili, Tanzania ingeweza kukuza lugha hii katika jukwaa la kimataifa, kuonyesha umuhimu wake na kuhamasisha matumizi na uhifadhi wake.

Hitimisho.
Kubadilisha jina la Tanzania kuwa la Kiswahili ni hatua yenye nguvu ya kukumbatia na kusherehekea utambulisho wa kitamaduni wa taifa, urithi wa lugha, na umuhimu wa kihistoria. Lingetia nguvu umoja wa kitaifa, kukuza Kiswahili katika jukwaa la kimataifa, na kuashiria hatua ya kuachana na urithi wa kikoloni. Mabadiliko haya
Jambo moja ambalo Hujalifikiria hizo lugha ulizo taja ni according to Kiswahili ndio zinaitwa hivyo ila not necessarily kimataifa zinatambulika hivyo.

Mfano Kichina lugha kabisa inaitwa Mandarin ikiwa mainland Ama Cantonese ikiwa maeneo kama Hongkong ila kiswahili ndio tunasema kichina,
 
USwahili ni utamaduni wa pwani, tena ni utamaduni uliovuka mipaka ya Tanzania ya sasa, upo mpaka Kenya.

Zaidi, Uswahili si utamaduni wa sehemu nyingi za Tanzania zilizo bara.

Mpaka hapo hoja yako ishashindwa.

Kwq sababu, kuna sehemu ambazo haziko Tanzania ila zina utamaduni wa Uswahili.

Halafu kuna sehemu zilizo Tanzania ambazo hazina utamaduni wa Uswahili.
 
Hizo nchi zote ulizotaja ni kama zinaundwa na kabila moja japo zinaweza kuwa na koo mbalimbali ndo maana ikawa rahisi nchi nzima kuwa na utamaduni na lugha inayofanana. Tz tuna makabila zaidi ya 120 hili haliwezekani.
 
Asili ya kiswahili ni pwani ndio,

Halafu kuna sehemu zilizo Tanzania ambazo hazina utamaduni wa Uswahi

USwahili ni utamaduni wa pwani, tena ni utamaduni uliovuka mipaka ya Tanzania ya sasa, upo mpaka Kenya.

Zaidi, Uswahili si utamaduni wa sehemu nyingi za Tanzania zilizo bara.

Mpaka hapo hoja yako ishashindwa.

Kwq sababu, kuna sehemu ambazo haziko Tanzania ila zina utamaduni wa Uswahili.

Halafu kuna sehemu zilizo Tanzania ambazo hazina utamaduni wa Uswahili.
Utamaduni wa pwani ya wapi, na inaongeleka wapi zaidi?

Mfano Kingereza ni lugha ya waingereza lakini asili yake ni lugha ya kabila la kijeruma lililowahi kuitawala uingereza na kupeleka lugha hiyo kusaamba Nchi nzima.

Pia hakuna sehemu iliyoTanzania ambayo haina utamaduni wa kiswahili Kwa sababu kiswahili ni kibantu ambacho ni mjumuiko wa Makabila yote ya Tanzania.
 
Hizo nchi zote ulizotaja ni kama zinaundwa na kabila moja japo zinaweza kuwa na koo mbalimbali ndo maana ikawa rahisi nchi nzima kuwa na utamaduni na lugha inayofanana. Tz tuna makabila zaidi ya 120 hili haliwezekani.
Nchi kama Burundi na Rwanda Zina Makabila matatu matatu, watutsi, watwa na wahutu ambao lugha zao zinamungiliani mkubwa wakuunda lugha zao za Kirundi na kinyarwanda
 
Jambo moja ambalo Hujalifikiria hizo lugha ulizo taja ni according to Kiswahili ndio zinaitwa hivyo ila not necessarily kimataifa zinatambulika hivyo.

Mfano Kichina lugha kabisa inaitwa Mandarin ikiwa mainland Ama Cantonese ikiwa maeneo kama Hongkong ila kiswahili ndio tunasema kichina,
Lakini Kwa upande wa Tanzania, Makabila yote ya raia wake wa asili ni wabantu ambao wanaunganishwa na lugha ya kiswahili.
Jina la Nchi ya china linatikana na jina la Nchi hiyo asilia "Qin" ambalo hawakupewa na mkoloni. Mkoloni alilikuta na akaendelea kulitumia.

Sisi kama watanzania tunahitaji kubadili jina la Nchi ambalo mkoloni alitupatia na kuweka jina letu tutakalo pendezwa nalo.

Mfano mkoloni kakuita mbwa baada ya kukuachia na kupata uhuru bado unajiita mbwa wakati unao uwezo wa kujiitq jina zuri.
 
Asili ya kiswahili ni pwani ndio,

Utamaduni wa pwani ya wapi, na inaongeleka wapi zaidi?

Mfano Kingereza ni lugha ya waingereza lakini asili yake ni lugha ya kabila la kijeruma lililowahi kuitawala uingereza na kupeleka lugha hiyo kusaamba Nchi nzima.

Pia hakuna sehemu iliyoTanzania ambayo haina utamaduni wa kiswahili Kwa sababu kiswahili ni kibantu ambacho ni mjumuiko wa Makabila yote ya Tanzania.
Kwa nini unalazimisha habari ya Uswahili, na habari ya utamaduni, iishie kwenye lugha tu?

Na hata hapo kwa nini unaongelea asiki za lugha, kitu ambacho hakina hata mipaka?

Watu wa Mombasa ni Waswahili, lakini hawako Tanzania.

Wakisema msiiite Tanzania Swahili kwa sababu Waswahili tupo hata nje ya Tanzania, utawabishia vipi?

Wasukuma wananutamaduninwa Kisukuma, si wa Kiswahili.

Wakisema Tanzania isiitwe Swahili kwa sababu Uswahili si utamaduni wa Tanzania nzima, Wasukuma utamaduni wao ninwa Kisukuma, si Kiswahili, utawakatalia vipi?

Unaelewa kuwa Uswahili ni zaidi ya lugha?
 
Kifaransa kinzungumzwa Nchi ngapi ulaya(ufaransa ubelgiji, usizi), Kijerumani je mbona Nchi nyingi tu ulaya(ujerumani, austria , Luxembourg)wanazungumza na hawajaenda kuwazuia.

Kiswahili ni kibantu, kisukuma ni Moja ya lugha za kibantu zilizochangia maneno katika lugha ya kiswahili (form 2).
Kwahiyo kubadili jina la Nchi Kuwa la kiswahili ni kuonyesha mungano wetu.
 
Kwa wasio jua asili ya jina "Tanganyika" inatokana na maneno ya lugha za kienyeji zilizozungumzwa katika eneo hilo. Neno hili lina asili ya Kiswahili, ambapo "Tanga" inamaanisha "pwani" au "bandari" na "nyika" inamaanisha "nchi kavu" au "eneo lenye nyika" katika lugha ya Kiswahili. Kwa pamoja, "Tanganyika" linamaanisha "eneo la pwani au bandari kwenye nchi kavu". Jina hili lilitumika na wakoloni kuashiria eneo la Tanganyika.

Hili jina walitupa wakoloni lakini sasa niwakati wa sisi kujipatia jina letu wenyewe.
 
Kifaransa kinzungumzwa Nchi ngapi ulaya(ufaransa ubelgiji, usizi), Kijerumani je mbona Nchi nyingi tu ulaya(ujerumani, austria , Luxembourg)wanazungumza na hawajaenda kuwazuia.

Kiswahili ni kibantu, kisukuma ni Moja ya lugha za kibantu zilizochangia maneno katika lugha ya kiswahili (form 2).
Kwahiyo kubadili jina la Nchi Kuwa la kiswahili ni kuonyesha mungano wetu.
Bado unalazimisha utamaduni uishie kwenye lugha.

Hujaelewa swali, hivyo huwezi kulijibu.
 
Swali ulilouliza ni hili hapa chini,

""Wakisema Tanzania isiitwe Swahili kwa sababu Uswahili si utamaduni wa Tanzania nzima(Makabila asilia ya Tanzania yote ni ya kibantu), Wasukuma utamaduni wao ninwa Kisukuma, si Kiswahili, utawakatalia vipi?""

Nimekujibu kwamba wasukuma ni washahili Kwa sababu Makabila ya watanzania wote ni ya kibantu.
Kisukuma nimoja ya lugha ya kibantu,
Kisuma=kibantu,
Kiswahili=kibantu.
Pili hakuna wakutuzuia watanzania tusiite Nchi yetu "kiswahili" Kwa sababu Kuna Nchi(mfano Kenya ,watu wa Mombasa) wanazungumza kiswahili. Nikakupa na mifano ya Nchi kama ufaransa wanaozungumza lugha ya Kifaransa wakati huohuo Ubelgiji wanaongea Kifaransa na hajawahi kuwazuia waongeaji wa 'Kifaransa Nchini ufaransa kujiita wafaransa.'
NB:Nekujibu ila haujaelewa, nimekufafanulia.
 
This fallacy is logical non sequitur.

Nchi haitakiwi kuitwa Kiswahili, Kiswahili kinaweza kuwa ni lugha, mapishi ya, etc. Ni sifa. Si jina.

Kama vile ambavyo nchi ya England haiitwi English, English ni lugha ya watu wa England.

Again, usifanye lugha kuw ndiyo utamaduni wote.

Inabidi ujifunze hicho Kiswahili kwanza kabla ya kusema nchi iitwe Kiswahili.

Inaonekana hata Kiswahili hujui.
 
Tuitwe Serengeti na kisha tukishabadili jina tubadili na katiba ili mihimili mikuu ya serekari iwe huru kufanya kazi zake [emoji1787]
 
This fallacy is logical non sequitur.

Nchi haitakiwi kuitwa Kiswahili, Kiswahili kinaweza kuwa ni lugha, mapishi ya, etc. Ni sifa. Si jina.

Kama vile ambavyo nchi ya England haiitwi English, English ni lugha ya watu wa England.

Again, usifanye lugha kuw ndiyo utamaduni wote.

Inabidi ujifunze hicho Kiswahili kwanza kabla ya kusema nchi iitwe Kiswahili.

Inaonekana hata Kiswahili hujui.
Iko hivi Anglo-saxon(Anglophone) ni watu wanao zungumza lugha ya ki English na wako Nchini England.
Waswahili(wabantu) wanazungumza kiswahili na ifanywe wawe wanatoka Nchi ya Swahili(Tanzania)

Anglo➡️ English ➡️ England
Bantu=waswahili ➡️ kiswahili ➡️Swahili.
 
Lakini Wabantu si Waswahili.

Wabantu wako Africa nzima kutoka huko Nigeria, Cameroon, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia, Botswana, Africa Kusini.

Sio tu hujui Kiswahili.

Hujui hata Wabantu ni nini.
 
Back
Top Bottom