Kwanini Tanzania inapaswa kubadilisha jina lake kuwa la Kiswahili?

Kwanini Tanzania inapaswa kubadilisha jina lake kuwa la Kiswahili?

Lakini Wabantu si Waswahili.

Wabantu wako Africa nzima kutoka huko Nigeria, Cameroon, Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia, Botswana, Africa Kusini.

Sio tu hujui Kiswahili.

Hujui hata Wabantu ni nini.
Neno Bantu=watu,
Wabantu= ni watu wanaozungumza lugha zinazofanana katika muundo wa kisarufi na msamiati , na wanapatika kusini mwa Sahara.

Wabantu wa Tanzania na Kenya tu (hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili. Na ndio Nchi pekee Duniani ambazo lugha yao ya kwanza ya Kitaifa ni kiswahili.

Swali lako""Lakini Wabantu si Waswahili""
Ndio wabantu wote si waswahili lakini waswahili ni sehemu ya wabantu.
Wabantu wa Tanzania na Kenya(hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoibuka kutokana na mchanganyiko wa lugha za wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki na lugha za kigeni zilizowekwa na wafanyabiashara.

NB: 1% ya wanigeria ndio wabantu,
Cameron pia sio wabantu.
 
Neno Bantu=watu,
Wabantu= ni watu wanaozungumza lugha zinazofanana katika muundo wa kisarufi na msamiati , na wanapatika kusini mwa Sahara.

Wabantu wa Tanzania na Kenya tu (hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili. Na ndio Nchi pekee Duniani ambazo lugha yao ya kwanza ya Kitaifa ni kiswahili.

Swali lako""Lakini Wabantu si Waswahili""
Ndio wabantu wote si waswahili lakini waswahili ni sehemu ya wabantu.
Wabantu wa Tanzania na Kenya(hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoibuka kutokana na mchanganyiko wa lugha za wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki na lugha za kigeni zilizowekwa na wafanyabiashara.

NB: 1% ya wanigeria ndio wabantu,
Cameron pia sio wabantu.
Sasa kwa nini unataka kuipa nchi yenye watu wengi ambao si Waswahili jina la Swahili?

Na kw anini unataka kuipa Tanzania jina la Swahili wakati kuna Waswahili ambao si Watanzania?

Pia, unaelewa kuwa Tanzania kuna watu wengi si Wabantu na pia si Waswahili?
 
Hivi ndio vitu mswahili anapenda kuwaza, badala ya kutumia ubongo wake kufikiria innovations, science, tech...
 
Hivi ndio vitu mswahili anapenda kuwaza, badala ya kutumia ubongo wake kufikiria innovations, science, tech...
Kila Nchi Kuna watu wenye taalamambalimbali, SI Kila mtu ni mwanasayansi wengine ni wabobezi wa maswala kiraia na kijamii.

Unacho kiona hakina maana kwako Mwana sayansi, wengine ndio taaaluma zao ambazo zinakusaidia wewe kujitambua raia wa Nchi Gani.
 
kiswahili kinatajwa kutumiwa na afrika mashariki yote,hivyo mataifa hayo yote yatumie jina Moja?
Kenya na Tanzania tu ndio wanatumia kama lugha mama, Nchi nyingine zilizobaki wanakitumia kama lugha ya biashara(lugha ya pili).
Hili ni pendekezo Kwa ajili ya Nchi yetu tu.

NB: Kifaransa kinazungumzwa na nyingi ulaya kama ubelgiji na uswizi lakini Kuna Nchi inaitwa Ufaransa raia wake wanazungumza Kifaransa.
Kijerumani pia kinazungumzwa na nyingi ulaya kama Austria na Luxembourg lakini Kuna Nchi inaitwa ujerumani wanazungumza Kijerumani.
 
Hakuna lugha inaitwa kichina chief....
Ndio hakuna, ila ni lahaja ya mwingiliano wa lugha zinazozungumza za mandarin, Cantonese Wu na min.
Yani nikama kiswahili Cha Zanzibar, Kanda ya ziwa , mtwara na Kenya. Wote tunazungumza kiswahili lakini kunabaadhi ya maneno nitofauti kulingana na eneo.

Mfano Tanzania: Gari. Kenya: Motokaa.
Tanzania: Daladala. Kenya: Matatu.
Tanzania:Mchicha. Kenya: Sukuma wiki.
Utofauti kati ya Tanzania bara na Zanzibar
Tz: choo. Zenji: msala.
Tz: Maharage. Zenji: marage.
Tz: unaenda wapi. Zenji: waenda wapi.
 
Jina la nchi lina umuhimu mkubwa wa kitamaduni, kihistoria, na kitaifa. Linahudumia kama ishara ya utambulisho, umoja, na fahari kwa wananchi wake.
Mfano wa orodha ya baadhi ya nchi na lugha zao:- zinazohusiana:
Ufaransa - Kifaransa
Ujerumani - Kijerumani
Hispania - Kihispania
Italia - Kiitaliano
Japani - Kijapani
China - Kichina
Urusi - Kirusi
Ugiriki - Kigiriki
India - Kihindi
Saudi Arabia - Kiarabu
Korea Kusini - Kikorea
Uturuki - Kituruki

Orodha hii inaonyesha jinsi nchi nyingi zinavyokuwa na majina yao yakihusiana kwa karibu na lugha yao kuu, jambo linaloimarisha utambulisho wao wa kitamaduni na kitaifa.

Faida zitokanazo na kubadili Jina la Nchi ya Tanzania kwenda Nchi ya Swahili:-
Utambulisho wa Kitamaduni na Fahari, Lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa ya letu na ni msingi wa utambulisho wa kitamaduni wa nchi hii. Inazungumzwa na kueleweka na wananchi wengi wa Tanzania, Kuchukua jina la Kiswahili kwa nchi kungeakisi na kusherehekea umoja huu wa lugha na kuhamasisha fahari na utambulisho wa kitaifa.

Umuhimu wa Kihistoria.
Jina "Tanzania" lenyewe ni mchanganyiko wa "Tanganyika" na "Zanzibar," maeneo mawili yaliyoshirikiana kuunda nchi hii mwaka 1964. Wakati jina hili linavyoakisi muungano wa kihistoria, limetokana na nomenklacha ya kikoloni. Kubadilisha jina kuwa la Kiswahili kungeashiria hatua ya kuachana na urithi wa kikoloni na kukumbatia urithi wa kiasili.

Utambuzi wa Kimataifa.
Jina la Kiswahili lingeitofautisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa, na kuonyesha urithi wake tajiri wa kitamaduni na lugha.

Umoja wa Kitaifa.
Katika nchi yenye utofauti kama Tanzania, kuimarisha umoja wa kitaifa ni muhimu. Jina la Kiswahili lingetumika kama kiunganisho kinachounganisha makabila mbalimbali na kama ishara ya urithi wa pamoja wa lugha na utambulisho wa pamoja wa watu wa Tanzania.

Uendelezaji wa Lugha.
Kwa kuchukua jina la Kiswahili, Tanzania ingeweza kukuza lugha hii katika jukwaa la kimataifa, kuonyesha umuhimu wake na kuhamasisha matumizi na uhifadhi wake.

Hitimisho.
Kubadilisha jina la Tanzania kuwa la Kiswahili ni hatua yenye nguvu ya kukumbatia na kusherehekea utambulisho wa kitamaduni wa taifa, urithi wa lugha, na umuhimu wa kihistoria. Lingetia nguvu umoja wa kitaifa, kukuza Kiswahili katika jukwaa la kimataifa, na kuashiria hatua ya kuachana na urithi wa kikoloni. Mabadiliko haya
Hakuna lugha inayoitwa Kihindi.
 

Attachments

  • Screenshot_20240712-121809.jpg
    Screenshot_20240712-121809.jpg
    450.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom