Kwanini Tanzania inapaswa kubadilisha jina lake kuwa la Kiswahili?

Neno Bantu=watu,
Wabantu= ni watu wanaozungumza lugha zinazofanana katika muundo wa kisarufi na msamiati , na wanapatika kusini mwa Sahara.

Wabantu wa Tanzania na Kenya tu (hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili. Na ndio Nchi pekee Duniani ambazo lugha yao ya kwanza ya Kitaifa ni kiswahili.

Swali lako""Lakini Wabantu si Waswahili""
Ndio wabantu wote si waswahili lakini waswahili ni sehemu ya wabantu.
Wabantu wa Tanzania na Kenya(hasa pwani) ndio walio Unda lugha ya kiswahili.

Kiswahili ni lugha ya Kibantu iliyoibuka kutokana na mchanganyiko wa lugha za wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki na lugha za kigeni zilizowekwa na wafanyabiashara.

NB: 1% ya wanigeria ndio wabantu,
Cameron pia sio wabantu.
 
Sasa kwa nini unataka kuipa nchi yenye watu wengi ambao si Waswahili jina la Swahili?

Na kw anini unataka kuipa Tanzania jina la Swahili wakati kuna Waswahili ambao si Watanzania?

Pia, unaelewa kuwa Tanzania kuna watu wengi si Wabantu na pia si Waswahili?
 
Hivi ndio vitu mswahili anapenda kuwaza, badala ya kutumia ubongo wake kufikiria innovations, science, tech...
 
Hivi ndio vitu mswahili anapenda kuwaza, badala ya kutumia ubongo wake kufikiria innovations, science, tech...
Kila Nchi Kuna watu wenye taalamambalimbali, SI Kila mtu ni mwanasayansi wengine ni wabobezi wa maswala kiraia na kijamii.

Unacho kiona hakina maana kwako Mwana sayansi, wengine ndio taaaluma zao ambazo zinakusaidia wewe kujitambua raia wa Nchi Gani.
 
kiswahili kinatajwa kutumiwa na afrika mashariki yote,hivyo mataifa hayo yote yatumie jina Moja?
Kenya na Tanzania tu ndio wanatumia kama lugha mama, Nchi nyingine zilizobaki wanakitumia kama lugha ya biashara(lugha ya pili).
Hili ni pendekezo Kwa ajili ya Nchi yetu tu.

NB: Kifaransa kinazungumzwa na nyingi ulaya kama ubelgiji na uswizi lakini Kuna Nchi inaitwa Ufaransa raia wake wanazungumza Kifaransa.
Kijerumani pia kinazungumzwa na nyingi ulaya kama Austria na Luxembourg lakini Kuna Nchi inaitwa ujerumani wanazungumza Kijerumani.
 
Hakuna lugha inaitwa kichina chief....
Ndio hakuna, ila ni lahaja ya mwingiliano wa lugha zinazozungumza za mandarin, Cantonese Wu na min.
Yani nikama kiswahili Cha Zanzibar, Kanda ya ziwa , mtwara na Kenya. Wote tunazungumza kiswahili lakini kunabaadhi ya maneno nitofauti kulingana na eneo.

Mfano Tanzania: Gari. Kenya: Motokaa.
Tanzania: Daladala. Kenya: Matatu.
Tanzania:Mchicha. Kenya: Sukuma wiki.
Utofauti kati ya Tanzania bara na Zanzibar
Tz: choo. Zenji: msala.
Tz: Maharage. Zenji: marage.
Tz: unaenda wapi. Zenji: waenda wapi.
 
Hakuna lugha inayoitwa Kihindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…