Kwanini Tanzania inunue ndege? Soma hoja kuu hizi nne...

Kwanini Tanzania inunue ndege? Soma hoja kuu hizi nne...

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
652
Reaction score
443
KWANINI TANZANIA INUNUE NDEGE?​

Na Bwanku M Bwanku

Kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt John Pombe Magufuli kulifungua ukurasa mwingine mpya kwenye sekta ya usafiri wa anga baada ya nguvu kubwa ya Serikali kulifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likitembelea machela na kufa kabisa. Mpaka sasa Serikali imefanikiwa kununua ndege 8 kwa cash huku ikitegemea kuongeza zingine 5 kwa miaka mitano ijayo kama ikichaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu huu.

Mtiririko wa ununuzi wa ndege hizi umekuwa na maswali na mijadala mingi sana mitaani na mitandaoni hasa kwenye vipalila vya kahawa na kwenye makundi mbalimbali kwa Watanzania wengi wakihoji kila mmoja kwa upande wake kuhusu maamuzi haya ya Serikali.

Upande mmoja ukikubaliana na kupongeza maamuzi ya Serikali kununua ndege hizi huku upande wa pili ukikosoa maamuzi hayo ya Serikali. Hawa wa pili wanahoji kama kweli ndege ni hitaji muhimu la Mtanzania kwasasa? Je ndege inamsaidiaje Mtanzania wa kawaida wa Katavi au Mtwara ndani ndani huko tena wa kipato cha chini asie na uhakika hata wa mlo mmoja? Ni Watanzania wangapi wanao uwezo wa kukidhi na kutumia usafiri wa ndege? Hawa wanajiuliza maswali mengi sana kuhusu ununuzi wa hizi ndege. Yani ni kama hawaelewi elewi hivi.

Sasa leo ngoja tupeane somo la kwanini nchi yetu inunue ndege ili kuondoa upotoshaji wa baadhi ya wenzetu Watanzania wanaonanga ununuzi huo wa ndege wakati wao wenyewe wakiwa ndio wa kwanza kuonekana wakitumia ndege hizo licha ya kukashfu na kukosoa ununuaji wake.

Kwanini Tanzania inunue ndege?

Tafakuri hii ni nyepesi sana. Mtaalamu wa uchumi wa Uingereza Adam Smith aliwahi kusema kwamba uchumi imara ni Cycle Economic Engaged Routine yaani uchumi ulioko kwenye mzunguko na unaoishi na kutegemea maeneo mengi. Unapotaka kujenga uchumi imara na vita yenyewe ya kusukuma uchumi uende mbele ni lazima uwe na nyenzo za kukufikisha na kukupeleka huko mbele. Nyakati hizi ambazo Tanzania inahaha kutekeleza azma yake ya kujenga uchumi wa viwanda inahitaji sana ndege kwa sababu zifuatazo:-

Mosi; Tanzania inatajwa kuwa nchi mojawapo iliyobarikiwa kila aina ya vivutio vya utalii hapa duniani. Tanzania inatajwa kuwa namba mbili duniani kwa uwingi wa vivutio vya utalii baada ya Brazil. Nchi hii iliyobarikiwa kila aina ya kivutio cha kumvutia mtalii kuja kwenye mbuga, bahari, mito, maziwa, mabonde, visiwa, hifadhi, milima, mapango ya kale, makumbusho ya kale na vingine kedekede ni lazima iwe na ndege ili kuzitumia ndege hizo kuwashawishi watalii kuja nchini kutalii.

Mfano ukiwa na ndege zako mwenyewe ni rahisi kumtoa mtalii moja kwa moja kutoka New York, Paris au Brussels kuja hapa kwa ndege zako bila kutumia za nchi nyingine ambazo nazo zina vivutio pia.

Ni hivi. Mfano mtalii anayetoka Marekani na anataka kuja kutalii Tanzania lakini akabebwa kwa ndege ya Kenya automatically Kenya itamshawishi atalii pale pale Kenya kwa kumuonyesha Turkana, Mt Meru ama Mombasa na moja kwa moja nchi yetu itamkosa yule Mtalii, mapato yake na hata kama atakuwa na Partners wa kutalii wote wataishia Kenya. Kwahiyo ukiwa na ndege zako mwenyewe utatangaza utalii wako kwa ndege zako kupitia TV zilizo ndani ya ndege hizo na hakuna mtalii atakaekuchoropoka kwenda kwingine. Tena ndege zenyewe zina majina ya vivutio vyetu.

Hii inasaidia sana kukuza sekta ya utalii na kuwaleta watalii wengi sana hapa kwetu na hivyo kuikuza Sekta hii ya utalii ambayo ni sekta mojawapo 3 muhimu sana kwenye ukuaji wa uchumi wa Tanzania na ndio mana leo sekta ya utalii imeendelea kuongeza idadi ya watalii wanaoingia kutoka 1,137,182 mwaka 2015 mpaka zaidi ya 1,510,151 hivi sasa na mapato ya watalii kudouble kutoka Dola za Marekani Bil 1.6 mwaka 2015 hadi 2.6 sasahivi. Unaona faida ya ndege? sasa kwanini zisinunuliwe.

Pili; Kiuchumi ndege ni Strategic sana hasa kwa dunia ya leo ambayo imehamia sana kwenye anga. Licha ya ukweli kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni wakulima lakini hiyo haina maana Serikali iwezekeze tu kwenye kilimo na kuziacha Sekta zingine. La hasha! Uchumi imara ni mnyumbuliko, kimombo wanaita Diversification of economy yaani uchumi unaotegemea sekta zaidi ya moja. Yaani uwe na sekta nyingi zinazochangia nguvu kwenye ukuaji wa uchumi wako. Taifa linalotaka kujenga Stable Economic base lazima lipinduke pinduke kwa kutegemea sekta anuai kama viwanda, madini, uwekezaji, usafiri, biashara, utalii na mengine mengi na sio kulalia sekta moja pekee na hizo sekta zinachangiwa sana ukuaji na uendeshwaji wake kwa kutumia anga. Leo huwezi kufanya biashara na Uholanzi au China kwa basi, yaani haiwezekani. Marekani, China, Japan na Ufaransa ndio wanachokifanya.

Hao wako vizuri kwenye Air economy, viwanda, biashara za kimataifa na uwekezaji na mengine. Ukinunua ndege maana yake tayali umeinua sekta zingine. Utalii, usafiri na biashara zinakuwa zimenyanyuka pia.

Kwa hiyo kununua ndege kunapanua wigo wa unyumbulifu wa uchumi na kuepusha uchumi dormant unaotegemea sekta moja na badala yake uhamie kwenye sekta nyingi (Diversity). Ukitegemea kilimo, usafiri, anga, viwanda, madini, utalii n.k maana yake ndiyo maendeleo. Economic Prosperity ya Taifa lolote lile duniani inapimwa na sekta imara na nyingi zilizopo ndani yake na jinsi zinavyochangia kwenye pato la taifa (National income).

Tatu; Dunia hii ya karne ya 21 sasa inahamia sana kwenye uchumi wa anga, wanauita Space Economy. Uchumi wa anga unakua kwa kasi sana kwa sasa duniani na mataifa makubwa yameweka nguvu Kubwa sana huko. Marekani yenyewe kawekeza zaidi ya U$ 20 Billion huko China anafata kisha Ufaransa na Korea Kusini kwa mbali. Uchumi wa anga ni pamoja na kununua ndege, kujenga na kuboresha viwanja vya ndege, Kufunga rada na satellite angani za kuongozea ndege na mengine mengi. Ukiwekeza vizuri kwenye uchumi wa anga (Space economy) kwa kutawala anga za mataifa mbalimbali unakuwa pazuri kuimarisha uchumi mana ndiko dunia iliko.

Ununuzi huu wa ndege wa Tanzania unaoambatana na upanuzi na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege unapita mkondo huo. Kwa jinsi biashara za kimataifa na muingiliano unavyokua kila siku basi kuwekeza kwenye anga ni strategy kubwa sana hasa ndege inayosafiri kwa haraka zaidi. Unaharakisha biashara za kimataifa na uwekezaji kwa haraka sana.

Nne na mwisho; Ununuzi wa ndege ni silaha ya kujenga uchumi unaotegemeana. Faida inayopatikana kwenye uwekezaji wa ndege tayali inaingia kwenye uboreshaji wa huduma zingine za wananchi kama afya, barabara na mengine mengi. Mfano Yapo maeneo kwenye nchi hii kiwango chao cha ukusanyaji wa mapato ni kidogo sana. Maeneo kama haya yanategemea bajeti kutoka Serikali kuu ili yajiendeshe. Kwa maana Serikali itafanya resources distribution kutoka palipokusanywa sana na kuallocate palipo na upungufu (Budget deficit). Faida inayopatikana kwenye sekta hii ya anga moja kwa moja inaenda kwenye mzunguko wa Maendeleo wa sekta zingine.

Bado zipo pia faida zilizozoeleka. Hapo tunategemea marubani wetu wa Watanzania watapata ajira, Wahudumu wa hizo ndege, maofficers mbalimbali wa viwanjani na kundi kubwa lililopo ndani ya sekta ya usafirishaji litapata ajira na kupunguza tatizo la ajira nchini. Yan ni maeneo mengi sana. Sasa utakuwa na uwezo wa kulala Dar na kuwahi kuhudhuria mkutano ama semina Mwanza au Kigoma. Hii ndiyo sababu kwanini Tanzania inunue ndege. Nani anabisha?

0657475347
 
Ndege zinatia HASARA.

Kenya wanakula hasara.

Rwanda ni hasara kwa miaka 10 mfululizo.

Afrika kusini kila mwaka wanalazimika kuli-bail out shirika lao.

Tanzania hatukupaswa kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga.

Wanaoweza kufanya biashara ya anga ni nchi zenye utajiri mkubwa na mapesa yasiyo na kazi kama Qatar, United Arab Emirates, etc
 
KWANINI TANZANIA INUNUE NDEGE?.

Na Bwanku M Bwanku

Kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt John Pombe Magufuli kulifungua ukurasa mwingine mpya kwenye sekta ya usafili wa anga baada ya nguvu kubwa ya Serikali kulifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likitembelea machela na kufa kabisa. Mpaka sasa Serikali imefanikiwa kununua ndege 8 kwa cash huku ikitegemea kuongeza zingine 5 kwa miaka mitano ijayo kama ikichaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu huu.
Hakika umeongea vyema
 
Nipo kwenye utalii, hujui usemalo. Sababu ya tickets za ndege kufikia Nairobi Ni landing fee na makodi mengi

Pili, Tangu mipaka kufunguliwa Tena, sijaona Air Tanzania ikileta watalii...ni mashirika yale Yale. KLM, Ethiopian airlines, Qatar, Emirates...

Hata kabla ya Corona, Air Tanzania haijaleta watalii

Hakuna mtalii aliyetaka kuja Tanzania akashindwa kufika.

Ndege ipi ya Air Tanzania umeenda new york, Frankfurt, Paris, uk?

Mataga hamuwezi propaganda

Watanzania hawajawahi kuona mtalii akija na Airtanzania..

Utanunuaje ndege Cash halafu uwakope Korosho wakulima? Hakuna nyongeza ya mishahara?

Hizo ndege wanapanda vigogo wa mataga wanaokula Kodi zetu
 
Ndege oyee

IMG-20200907-WA0069.jpg
 
Hapan ni kuweka mikakat mizuri tu

Sio nchi zote znazorusha ndege zmeingia hasara

Rwanda walisema hivyohivyo kwamba wataweka mikakati mizuri.

lakini leo hii Rwanda amesalimu amri na anauza hisa za shirika lake kwa Qatar Airways.

Na kwa jinsi corona ilivopiga nadhani atalazimika kuuza hisa hizo kwa hasara kubwa.
 
ATC ina wafanyakazi wengi mahitaji mengi kuliko kinachoingizwa na hizo Ndege zilizonunuliwa kifisadi kwa 10% nyingi baada ya wajanja kulipa kwa cash ili wale chao kwa cash pia, Gharama za kuendesha shirika la Ndege Tanzania ni kubwa mno na ukichanganya na gharama za ujanja ujanja za service za hizo Ndege ndipo huzidisha balaa, wanufaika wa mfumo huo hawataki mabadiliko kamwe.
 
Wavuvi wengi wa kanda ya ziwa wanalia NYAVU zao kutiwa kiberiti.

Unadhani unaweza kuwavutia kwa habari ya ndege?

kwani kabla ya atcl si kulikuwa na mashirika binafsi ya ndege hapa nchini ambayo mumeyafukuza ili atcl ifanye kazi?
ATCL inaendeshwa kwa hasara kubwa mno lakini kwa kuwa wanufaika ni wanaccm ni vigumu kusikiliza kilio cha wengi
 
Sina matatizo na Magu kununua ndege- Zitapandwa na pesa zitaingia - na ni prestige kwa nchi
Sina matatizo na Magu kujenga bwawa la umeme- Umeme ni nguvu ya uchochezi wa viwanda - Nishati mubadala
Sina matatizo la Magu kujenga Reli nzuri - investment ya infrastructure watu watapanda na watu watasafirisha mizgo uchumi utaenda mbele

TATIZO LA HUYU MTU NI: UKATILI, kukosa utu, kumtwanga Risasi 16 Lisu. Huu ni unyama, unafuta mazuri yote aliyoyafanya!!!!!!
Amen
 
Tatizo mnaongea vitu bila ushahidi!Kama mnasema ndege zimeongeza watalii kwa kuwabeba kuwaleta,hebu tupeni route hizi ndege ilizopiga toka zimenunuliwa!

Tupeni na idadi ya raia wa kigeni waliozipanda kuja kutalii ili tuamini hilo ongezeko sekta ya utalii ni kutokana na ndege tulizonunua na si factor nyingine kwa asilimia kubwa!

Binafsi siamini kama ndege zetu zimeleta tija kwenye utalii zaidi ya kuona propaganda!
 
..ndege zinatia HASARA.

Kenya wanakula hasara.

Rwanda ni hasara kwa miaka 10 mfululizo.

Afrika kusini kila mwaka wanalazimika kuli-bail out shirika lao.

Tz hatukupaswa kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga.

Wanaoweza kufanya biashara ya anga ni nchi zenye utajiri mkubwa na mapesa yasiyo na kazi kama Qatar, United Arab Emirates, etc
Kenya ina raia wangapi?!

Wangapi wanauwezo wa kumudu kutumia ndege?!

Kenya na Tanzania zinafanana?!

Je, mbinu za kiuchumi za kenya na Tanzania hutungwa katika bunge moja?!
 
Hapan ni kuweka mikakat mizuri tu
Sio nchi zote znazorusha ndege zmeingia hasara
Kwa sasa hatujui kama tunakula hasara au vipi!CAG kapigwa pini kukagua shirika hili!
Usiri uliopo kwenye hili shirika una jambo!
 
..Afrika Kusini inapokea wasafiri/abiria/watalii wengi kuliko Tz lakini wanapata hasara kila mwaka.

..hakuna sababu ya Tz kuingia ktk biashara yenye changamoto kiasi hicho tena kwa kutumia KODI za wananchi.

How South African Airways ended up in bankruptcy protection

How South African Airways ended up in bankruptcy protection
Hebu mtufafanulie hiyo hasara imekaaje maana huwa mnasema hasara ila hatuoni ushahidi?!
 
Back
Top Bottom