Kwanini Tanzania inunue ndege? Soma hoja kuu hizi nne...

Kwanini Tanzania inunue ndege? Soma hoja kuu hizi nne...

Kenya ina raia wangapi?!

Wangapi wanauwezo wa kumudu kutumia ndege?!

Kenya na Tanzania zinafanana?!

Je, mbinu za kiuchumi za kenya na Tanzania hutungwa katika bunge moja?!

..faida au hasara haitokani na idadi ya raia.

..uwezo wetu wa ku-invest ili tuweze kushindana ni mdogo.

..pia hakuna idadi ya abiria wa kutosha kuweza kutengeneza "hub," na ku-justify manunuzi ya ndege za kutosha.

..bila kuwa na "hub" huwezi kupata faida ktk biashara ya shirika la ndege.
 
Nisamehe but hii analysis yako ni takataka isiyostahili hata kuwekwa kwenye dustbin!!!
 
Nisamehe but hii analysis yako ni takataka isiyostahili hata kuwekwa kwenye dustbin!!!

..kwanza walisema ndege zinasafirisha watalii.

..wakaulizwa mbona haziendi ktk nchi zinazoleta watalii wengi zaidi nchini?

..baada ya kukosa majibu, sasa wamekuja na hoja eti ndege zinasafirisha samaki.
 
..kwanza walisema ndege zinasafirisha watalii.

..wakaulizwa mbona haziendi ktk nchi zinazoleta watalii wengi zaidi nchini?

..baada ya kukosa majibu, sasa wamekuja na hoja eti ndege zinasafirisha samaki.
MTU makini hawezi kupoteza muda wake kujibizana na hao vilaza! Sijui kwanini mtu akiwa CCM anapungukiwa na akili kabisa!
 
Ndege zinatia HASARA.

Kenya wanakula hasara.

Rwanda ni hasara kwa miaka 10 mfululizo.

Afrika kusini kila mwaka wanalazimika kuli-bail out shirika lao.

Tanzania hatukupaswa kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga.

Wanaoweza kufanya biashara ya anga ni nchi zenye utajiri mkubwa na mapesa yasiyo na kazi kama Qatar, United Arab Emirates, etc
Running cost kubwa ya ndege ni fuel cost. Those guys are pissing oil. Waki flush toilet yanatoka mafuta.
 
Akiingia Lissu, hizo ndege zote zinapigwa mnada.
 
Tatizo mnaongea vitu bila ushahidi!Kama mnasema ndege zimeongeza watalii kwa kuwabeba kuwaleta,hebu tupeni route hizi ndege ilizopiga toka zimenunuliwa!
Tupeni na idadi ya raia wa kigeni waliozipanda kuja kutalii ili tuamini hilo ongezeko sekta ya utalii ni kutokana na ndege tulizonunua na si factor nyingine kwa asilimia kubwa!
Binafsi siamini kama ndege zetu zimeleta tija kwenye utalii zaidi ya kuona propaganda!

Zaidi ya kufata wanafunzi china na india sijawahi kusikia Kama zimeenda hata ulaya
 
..kwanza walisema ndege zinasafirisha watalii.

..wakaulizwa mbona haziendi ktk nchi zinazoleta watalii wengi zaidi nchini?

..baada ya kukosa majibu, sasa wamekuja na hoja eti ndege zinasafirisha samaki.

Wakati rwanda air ndio mara zote inabeba samaki
 
KWANINI TANZANIA INUNUE NDEGE?.

Na Bwanku M Bwanku

Kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya 5 chini ya Dkt John Pombe Magufuli kulifungua ukurasa mwingine mpya kwenye sekta ya usafiri wa anga baada ya nguvu kubwa ya Serikali kulifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likitembelea machela na kufa kabisa. Mpaka sasa Serikali imefanikiwa kununua ndege 8 kwa cash huku ikitegemea kuongeza zingine 5 kwa miaka mitano ijayo kama ikichaguliwa tena kwenye uchaguzi mkuu huu.

Mtiririko wa ununuzi wa ndege hizi umekuwa na maswali na mijadala mingi sana mitaani na mitandaoni hasa kwenye vipalila vya kahawa na kwenye makundi mbalimbali kwa Watanzania wengi wakihoji kila mmoja kwa upande wake kuhusu maamuzi haya ya Serikali.

Upande mmoja ukikubaliana na kupongeza maamuzi ya Serikali kununua ndege hizi huku upande wa pili ukikosoa maamuzi hayo ya Serikali. Hawa wa pili wanahoji kama kweli ndege ni hitaji muhimu la Mtanzania kwasasa? Je ndege inamsaidiaje Mtanzania wa kawaida wa Katavi au Mtwara ndani ndani huko tena wa kipato cha chini asie na uhakika hata wa mlo mmoja? Ni Watanzania wangapi wanao uwezo wa kukidhi na kutumia usafiri wa ndege? Hawa wanajiuliza maswali mengi sana kuhusu ununuzi wa hizi ndege. Yani ni kama hawaelewi elewi hivi.

Sasa leo ngoja tupeane somo la kwanini nchi yetu inunue ndege ili kuondoa upotoshaji wa baadhi ya wenzetu Watanzania wanaonanga ununuzi huo wa ndege wakati wao wenyewe wakiwa ndio wa kwanza kuonekana wakitumia ndege hizo licha ya kukashfu na kukosoa ununuaji wake.

Kwanini Tanzania inunue ndege?

Tafakuri hii ni nyepesi sana. Mtaalamu wa uchumi wa Uingereza Adam Smith aliwahi kusema kwamba uchumi imara ni Cycle Economic Engaged Routine yaani uchumi ulioko kwenye mzunguko na unaoishi na kutegemea maeneo mengi. Unapotaka kujenga uchumi imara na vita yenyewe ya kusukuma uchumi uende mbele ni lazima uwe na nyenzo za kukufikisha na kukupeleka huko mbele. Nyakati hizi ambazo Tanzania inahaha kutekeleza azma yake ya kujenga uchumi wa viwanda inahitaji sana ndege kwa sababu zifuatazo:-

Mosi; Tanzania inatajwa kuwa nchi mojawapo iliyobarikiwa kila aina ya vivutio vya utalii hapa duniani. Tanzania inatajwa kuwa namba mbili duniani kwa uwingi wa vivutio vya utalii baada ya Brazil. Nchi hii iliyobarikiwa kila aina ya kivutio cha kumvutia mtalii kuja kwenye mbuga, bahari, mito, maziwa, mabonde, visiwa, hifadhi, milima, mapango ya kale, makumbusho ya kale na vingine kedekede ni lazima iwe na ndege ili kuzitumia ndege hizo kuwashawishi watalii kuja nchini kutalii.

Mfano ukiwa na ndege zako mwenyewe ni rahisi kumtoa mtalii moja kwa moja kutoka New York, Paris au Brussels kuja hapa kwa ndege zako bila kutumia za nchi nyingine ambazo nazo zina vivutio pia.

Ni hivi...Mfano mtalii anayetoka Marekani na anataka kuja kutalii Tanzania lakini akabebwa kwa ndege ya Kenya automatically Kenya itamshawishi atalii pale pale Kenya kwa kumuonyesha Turkana, Mt Meru ama Mombasa na moja kwa moja nchi yetu itamkosa yule Mtalii, mapato yake na hata kama atakuwa na Partners wa kutalii wote wataishia Kenya. Kwahiyo ukiwa na ndege zako mwenyewe utatangaza utalii wako kwa ndege zako kupitia TV zilizo ndani ya ndege hizo na hakuna mtalii atakaekuchoropoka kwenda kwingine. Tena ndege zenyewe zina majina ya vivutio vyetu.

Hii inasaidia sana kukuza sekta ya utalii na kuwaleta watalii wengi sana hapa kwetu na hivyo kuikuza Sekta hii ya utalii ambayo ni sekta mojawapo 3 muhimu sana kwenye ukuaji wa uchumi wa Tanzania na ndio mana leo sekta ya utalii imeendelea kuongeza idadi ya watalii wanaoingia kutoka 1,137,182 mwaka 2015 mpaka zaidi ya 1,510,151 hivi sasa na mapato ya watalii kudouble kutoka Dola za Marekani Bil 1.6 mwaka 2015 hadi 2.6 sasahivi. Unaona faida ya ndege? sasa kwanini zisinunuliwe.

Pili; Kiuchumi ndege ni Strategic sana hasa kwa dunia ya leo ambayo imehamia sana kwenye anga. Licha ya ukweli kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni wakulima lakini hiyo haina maana Serikali iwezekeze tu kwenye kilimo na kuziacha Sekta zingine. La hasha! Uchumi imara ni mnyumbuliko, kimombo wanaita Diversification of economy yaani uchumi unaotegemea sekta zaidi ya moja. Yaani uwe na sekta nyingi zinazochangia nguvu kwenye ukuaji wa uchumi wako. Taifa linalotaka kujenga Stable Economic base lazima lipinduke pinduke kwa kutegemea sekta anuai kama viwanda, madini, uwekezaji, usafiri, biashara, utalii na mengine mengi na sio kulalia sekta moja pekee na hizo sekta zinachangiwa sana ukuaji na uendeshwaji wake kwa kutumia anga. Leo huwezi kufanya biashara na Uholanzi au China kwa basi, yaani haiwezekani. Marekani, China, Japan na Ufaransa ndio wanachokifanya.

Hao wako vizuri kwenye Air economy, viwanda, biashara za kimataifa na uwekezaji na mengine. Ukinunua ndege maana yake tayali umeinua sekta zingine. Utalii, usafiri na biashara zinakuwa zimenyanyuka pia.

Kwa hiyo kununua ndege kunapanua wigo wa unyumbulifu wa uchumi na kuepusha uchumi dormant unaotegemea sekta moja na badala yake uhamie kwenye sekta nyingi (Diversity). Ukitegemea kilimo, usafiri, anga, viwanda, madini, utalii n.k maana yake ndiyo maendeleo. Economic Prosperity ya Taifa lolote lile duniani inapimwa na sekta imara na nyingi zilizopo ndani yake na jinsi zinavyochangia kwenye pato la taifa (National income).

Tatu; Dunia hii ya karne ya 21 sasa inahamia sana kwenye uchumi wa anga, wanauita Space Economy. Uchumi wa anga unakua kwa kasi sana kwa sasa duniani na mataifa makubwa yameweka nguvu Kubwa sana huko. Marekani yenyewe kawekeza zaidi ya U$ 20 Billion huko China anafata kisha Ufaransa na Korea Kusini kwa mbali. Uchumi wa anga ni pamoja na kununua ndege, kujenga na kuboresha viwanja vya ndege, Kufunga rada na satellite angani za kuongozea ndege na mengine mengi. Ukiwekeza vizuri kwenye uchumi wa anga (Space economy) kwa kutawala anga za mataifa mbalimbali unakuwa pazuri kuimarisha uchumi mana ndiko dunia iliko.

Ununuzi huu wa ndege wa Tanzania unaoambatana na upanuzi na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege unapita mkondo huo. Kwa jinsi biashara za kimataifa na muingiliano unavyokua kila siku basi kuwekeza kwenye anga ni strategy kubwa sana hasa ndege inayosafiri kwa haraka zaidi. Unaharakisha biashara za kimataifa na uwekezaji kwa haraka sana.

Nne na mwisho; Ununuzi wa ndege ni silaha ya kujenga uchumi unaotegemeana. Faida inayopatikana kwenye uwekezaji wa ndege tayali inaingia kwenye uboreshaji wa huduma zingine za wananchi kama afya, barabara na mengine mengi. Mfano Yapo maeneo kwenye nchi hii kiwango chao cha ukusanyaji wa mapato ni kidogo sana. Maeneo kama haya yanategemea bajeti kutoka Serikali kuu ili yajiendeshe. Kwa maana Serikali itafanya resources distribution kutoka palipokusanywa sana na kuallocate palipo na upungufu (Budget deficit). Faida inayopatikana kwenye sekta hii ya anga moja kwa moja inaenda kwenye mzunguko wa Maendeleo wa sekta zingine.

Bado zipo pia faida zilizozoeleka. Hapo tunategemea marubani wetu wa Watanzania watapata ajira, Wahudumu wa hizo ndege, maofficers mbalimbali wa viwanjani na kundi kubwa lililopo ndani ya sekta ya usafirishaji litapata ajira na kupunguza tatizo la ajira nchini. Yan ni maeneo mengi sana. Sasa utakuwa na uwezo wa kulala Dar na kuwahi kuhudhuria mkutano ama semina Mwanza au Kigoma. Hii ndiyo sababu kwanini Tanzania inunue ndege. Nani anabisha?

0657475347
Usafiri wa anga haukwepeki,especially ukiwa na National airlines ni ajira,ni biashara,ni usafiri,ni utalii ni uwezo,ni mapato.
Panua viwanja vya mkakati ziweze kutua ndege kubwa.
 
Uliyoyandika ni sawa kwa mtazamo wako ila hayakutakiwa yafanyike kwa pupa kipindi hichi.hiyo mipango ya madege mengi ilitakiwa iwe miaka 30 ijayo Kwasasa ndege 3 tu zingetutosha.Fedha zilizobaki ziende kwenye changamoto nyingine zinazotukabili.Hizo sekta zote ulizozitaja hizo ndege kwa kipindi hichi hazijafanya mambo yoyote ya msingi nahii nikwasababu bado hatujafanya mambo ya msingi kufikia uchumi utakazifanya hizo ndege zifanye kazi kusudiwa.kwa mfano ni utalii gani unaouzungumzia uliofanywa au utakaofanywa na hizi ndege?.
 
Kenya ina raia wangapi?!

Wangapi wanauwezo wa kumudu kutumia ndege?!

Kenya na Tanzania zinafanana?!

Je, mbinu za kiuchumi za kenya na Tanzania hutungwa katika bunge moja?!
Stupid questions from a stupid fellow a member of a stupid Party. CCM balaa!
 
Ndege zinatia HASARA.

Kenya wanakula hasara.

Rwanda ni hasara kwa miaka 10 mfululizo.

Afrika kusini kila mwaka wanalazimika kuli-bail out shirika lao.

Tanzania hatukupaswa kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga.

Wanaoweza kufanya biashara ya anga ni nchi zenye utajiri mkubwa na mapesa yasiyo na kazi kama Qatar, United Arab Emirates, etc
Mbona Viongozi wako hatuyajui hayo usemayo. Wewe kijana wayatoa Wapi?
4912ce9ebf39433d964bc270b224a0f2.jpg
9965d0fd318841c0b2e2d1dcde538646.jpg
 
Mbona Viongozi wako hatuyajui hayo usemayo. Wewe kijana wayatoa Wapi?View attachment 1563768View attachment 1563769

..Nice try.

..hoja ya kwanza ni kama serikali inunue ndege, au isinunue.

..hoja nyingine ni kama shirika la ndege linaweza kuendeshwa kwa faida, au litatuletea hasara.

..sasa hoja hizo hapo juu huwezi kuzijibu kwa kupiga picha viongozi wa upinzani wakiwa wanasafiri kwa ndege.

..Vijana wa CCM mna matatizo kwasababu kila hoja na kila jambo mnataka kulitetea kwa picha.

..Bila picha you can not argue anything.
 
..Nice try.

..hoja ya kwanza ni kama serikali inunue ndege, au isinunue.

..hoja nyingine ni kama shirika la ndege linaweza kuendeshwa kwa faida, au litatuletea hasara.

..sasa hoja hizo hapo juu huwezi kuzijibu kwa kupiga picha viongozi wa upinzani wakiwa wanasafiri kwa ndege.

..Vijana wa CCM mna matatizo kwasababu kila hoja na kila jambo mnataka kulitetea kwa picha.

..Bila picha you can not argue anything.
Wanatumia lugha ya picha Ili ujumbe uwafikie hata wasiojua kusoma.
tapatalk_1599279840294.jpg
tapatalk_1599279784400.jpg
 
Ndege zinatia HASARA.

Kenya wanakula hasara.

Rwanda ni hasara kwa miaka 10 mfululizo.

Afrika kusini kila mwaka wanalazimika kuli-bail out shirika lao.

Tanzania hatukupaswa kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa anga.

Wanaoweza kufanya biashara ya anga ni nchi zenye utajiri mkubwa na mapesa yasiyo na kazi kama Qatar, United Arab Emirates, etc
Kuwa na shirika la ndege kuna faida nyingi wewe kwa sababu hufahamu unataka kutuaminisha wote kwamba ndege hazina faida. Hakuna biashara ya ndege isiyo na faida ndio sababu nchi zote zinakuwa na mikataba ya reciprocity. Ndege zingekuwa hazina faida kusingekuwa na mashirika mengi ya ndege. Ni sawa na vyama vya Siasa kama kusingekuwa na faida Mlevi wa konyagi asingeweza kukaa miaka yote hiyo kwenye chama na kujitajirisha binafsi na familia yake.
 
..faida au hasara haitokani na idadi ya raia.

..uwezo wetu wa ku-invest ili tuweze kushindana ni mdogo.

..pia hakuna idadi ya abiria wa kutosha kuweza kutengeneza "hub," na ku-justify manunuzi ya ndege za kutosha.

..bila kuwa na "hub" huwezi kupata faida ktk biashara ya shirika la ndege.
You are not serious, what is a ''hub'' in air industry?
 
Back
Top Bottom