Kwanini Tanzania na sio Cameroon: Imperialism and Barbaric actions against patriotism

Kwanini Tanzania na sio Cameroon: Imperialism and Barbaric actions against patriotism

Madictator sikuzote huaminisha watu wao kuwa kuna maadui wa nje hawawatakii mema na pia kuna watu ndani ya nchi wanatumiwa na maadui wa nje.Kwa kuaminisha watu hivyo huendelea kukaa madarakani na kujustfy matendo yao.
Kwani hawezi pigana hiyo vita ya kiuchumi bila kuingilia mikutano ya kisiasa, kusweka ndani wanasiasa, wanasiasa kupotea, kupigwa risasi, kubadili sheria za takwimu nk?
Pia Uganda au Rwanda wakiharibu na kutoambiwa haamaanishi na wewe ukikosea usiambiwe. Kuna wengine hawaambiwi sababu wanaonekana wameshakuwa doomed, hawarekebishiki. Mtu akikushauri ujirekebishe ujue ameona una uwezo wa kufanya makubwa.

Endeleeni na Rafiki wa dhati kutoka China, Siku wakishika uchumi wote ndiyo muanze kulialia.
Huitaj kuambiwa kuwa mtu mweupe ni adui wa ngozi nyeusi aliyejificha kwenye mwamvuli wa MISAADA mara kutetea democracy. Hao walioko ndani wako kisheria, nilifikir ungekuja na vifungu vya sheria kuonesha hawajatendewa haki kuweko huko ndani.Kuwa kiongoz wa siasa sio kinga ya kuishi utakavyo nje ya sheria. Kila nchi inataratibu zake ktk kufikia malengo. Haiwez ikawa nchi kama kila siku watu wanaamua kuandamana ovyo na bila sababu za mcng. Umeambiwa fanya siasa ktk jambo lako lkn hutaki unataka ukafanye siasa kwenye jimbo la mwenzio. Kwamba unataka kugundua nini huko?Mattz ya wananchi wako yameisha kiasi uone ni mda wa kwenda kwenye jimbo la mwenzangu?Rais kafuta sherehe za uhuru na hela kaagiza zijenge hospital, we unapinga oooh bunge halijapitisha so tuandamane na wakati unajua fika hilo swala hata lingeletwa huko bungeni lingepita. Hizi sio siasa uchwara?
 
Ngoja Jiwe lipondwe kwanza ndio tutakujibu
Wasting their time. It is high time now we stand firm with our beloved leader against them. This time we have won.
The more they see us moving towards being independent, the more they make noises. After all we have all the choices....watusubiri muda utawaambia.

Africa wanaopendwa ni kama hao kina Paul Biya au marehemu Omar Bongo
 
Sawa, hivyo vita ndio vinafanya mkulu achezee box la kura kwa faida ya ccm? Ule wizi wa mabox ya kura ili ccm itangazwe washindi ni sehemu ya hiyo vita ya propaganda mfu? Ule ukatili anaoagiza mkulu kwenye box la kura kwa faida ya ccm una ulazima wowote kisa hiki Cameroon, Uganda nk wanafanya hivyo hivyo? Ajirekebishe aheshimu box la kura ili wananchi wote tuwe kitu kimoja dhidi ya hao wazungu. Sio kuongoza kwa itikadi kisha mtarajie tuwe pamoja. Dhuluma haimuachi salama.

Mkuu

Umemsikia huyo kilaza alieleta uzi,eti mbona Cameroon anafanya makosa sana Jiwe kafanya machache anaadhibiwa?

Hayo hayo machache ni makosa,anatumia makosa ya wengine kufuta makosa yake!

Wamebanwa pabaya sana!

Hii dunia tenda haki na utaheshimiwa milele....

Heshima ya Mandela na Mussolini hapa duniani ni kama tembo na sisimizi!
 
Sawa, hivyo vita ndio vinafanya mkulu achezee box la kura kwa faida ya ccm? Ule wizi wa mabox ya kura ili ccm itangazwe washindi ni sehemu ya hiyo vita ya propaganda mfu? Ule ukatili anaoagiza mkulu kwenye box la kura kwa faida ya ccm una ulazima wowote kisa hiki Cameroon, Uganda nk wanafanya hivyo hivyo? Ajirekebishe aheshimu box la kura ili wananchi wote tuwe kitu kimoja dhidi ya hao wazungu. Sio kuongoza kwa itikadi kisha mtarajie tuwe pamoja. Dhuluma haimuachi salama.
Mkuu hizo ni siasa za Africa. Swala ni kwanini hao wazungu wanaiona Tanzania tu?Na history inaonesha kiongoz yyt aliyekinyume na maslai ya mzungu lzm apigwe vita ila aliyesawa naye hata kama hakuna democracy lazima wamuunge mkono. Huoni kuna la zaidi nje ya wanachoita HAKI ZA BINADAMU?
 
Kuna Tatizo gani mtu kutoka jimbo jingine kwenda kufanya mkutano jimbo jingine?

Unavyosema kwenda kufanya siasa ni kama vile siasa ni jambo baya na la vurugu. Unajua maana ya siasa? Ni hivi, Siasa ni mchakato wa kufanya maamuzi jinsi nchi itavyoendeshwa na chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu wenye mawazo yanayofanana ya jinsi ya kuendesha nchi.

Ukiyajua hayo utajua kuwa kuna faida zaidi siasa ikifanyika kotekote nchini kuliko hasara.

Unasema wanaokamatwa na kunyimwa dhamana ni kwasababu wamevunja sheria za nchi!!!?
 
Mnafiki,kiherehere,hujitambui,unawaza Kwa kutumia masaburi na una njaa ndio unajikomba na kujipendekeza kwa Jiwe.
great! nakuhaidi nitaongeza juhudi kulinda title ulizonipa.
Naanza kwa kujipendekeza:Magufuli oyeee
Kumbuka kujibu swali ambalo haujaulizwa ni kiherehere pia, ahsante kwa kuungana na mimi kwenye kiherehere.
 
IMPERIALISM AND PATRIOTISM

Nimekuwa najiuliza kwanini Tanzania na sio Cameroon na kwanini Magufuli regime na sio incumbent Paul Biya regime.

Cameroon chini ya Rais Paul Biya aliyedumu madarakani kwa takribani miaka 36 na Cameroon iliyo na matatizo lukuki ya ndani tumeshuhudia jeshi ikiwapiga wafuasi wa upinzani na kuua watu kinyama barabarani mwezi octoba mauaji ya kutisha yalifanyika lakini hakuna measures zinazochukuliwa kwa Paul Biya na serikali yake.Juzi tarehe 5-dec US imepeleka msaada wa dollar Bilioni 27 Cameroon licha ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu na kutokuwepo na political change Rais Biya yupo madarakani kwa miaka 36.

Tumeona namna Tanzania ikipigiwa kelele na mataifa makubwa ya Magharibi na matamko yakitolewa huku na kule na vitisho juu.

Mnamo mwezi Novemba 2016 Bunge liliishauri serikali isijiunge na mkataba wa EPA na serikali ilikataa kujiunga na EPA, lakini jumuiya ya EU ikaja juu na kutoa vitisho mbali mbali lakini serikali ilisimamia msimamo wake baadae EU wakawaomba Museveni na Uhuru wamshauri Magufuli asaini mkataba kandamizi wa EPA na Museveni alimshawishi Magufuli ila mpaka sasa Magufuli hajasaini.Mkataba wa EPA ni mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi za EU na EAC lakini kwasisi tutabaki kuwa importers tu kuwanufaisha na viwanda vyetu vitakufa na hata ndoto ya viwanda itakufa.

Rais magufuli na Kagame walipiga marufuku uingizaji wa nguo za mitumba tukaona USA ikaja juu na kutishia kuiwekea vikwazo Tanzania baadae serikali ya Tanzania ikalegeza.

Suala la Acasia likivyokuwa handled na Rais wa Tanzania kiukweli hii imewagusa imperialists kwa kiasi kikubwa ukizingatia dhahabu ni moja ya resource muhimu kwa US na Nchi za ulaya na kutetereka kwa kampuni kubwa ya madini ya hawa wakubwa lazima wawatetee wafanya biashara wao.

Je Hawa mabwana wapo concerned kweli na haki za binaadamu zinazodaiwa kuvunjwa Tanzania ndio maana nikatolea mfano nchi kama Cameroon chini ya rais Biya mbona hashambuliwi kama rais wa Tanzania.

Lets stop this Imperialism and Barbaric actions from Imperialists and the best way to counter this horror and Barbarism is to be patriotic to our mother land no body will liberate our economy ila ni sisi wenyewe tu kama vile babu zetu walivyopigania uhuru wa nchi hakuna imperialist aliyekuja kufanya liberation Africa ila patriotism na nationalism ya wazee wetu ndio iliyotuletea uhuru.

Hivyo basi hakuna yeyote atakayekuja kufanya liberation ya uchumi Africa isipokuwa patriotic na nationalists kama Rais Magufuli na wengineo.Imperialists siku zote wanapenda Africa na Latin America iwe ni dump ya bidhaa zao na kunyonya maliasili za nchi za bara hizi kwa kuwarubuni viongozi kwa mikataba mibovu na later kuja kutoa pesa kwa mgongo wa msaada.

Ukiukwaji wa haki za binaadamu kama US na EU wanavyosema mbona Egpt hakuna haki za LGTB na ni kosa la jinai kufanya ushoga na sheria zao ni kandamizi maisha jela mbona hatusikii wakitolewa kauli na wakilaaniwa kwa kuminya haki za binaadamu na kila mwaka US hupeleka pesa Egypt kuchangia bajeti..Why Tanzania na sio Egypt obvious utajua ni tough stance ya rais Magufuli ya kufanya liberation ya uchumi na kutetetea exploitation ya resources na kustand against capitalist Barbarism.

Ipo siku Tanzania na Africa itakuwa Economic independent hata Mao alivyofanya mapinduzi China alikumbana na misukosuko na Vita kutoka kwa Imperialists lakini mwisho wa siku China imesimama na kuwa Nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi,kiteknolojia na viwanda.Kwenye kila mapinduzi lazima changamoto na kupigwa vita kuwepo kwa njia na mbinu mbalimbali hata kulazimisha regime change kwa kumeddle siasa za nchi.

Revolution is not a bed of roses.A revolution is a struggle between the future and the past.

-Fidel Castro
Uchambuzi mzuri lakini ni lazima tuwe ma DICTATOR ndiyo tulete mapinduzi ktk maendeleo ya uchumi ktk taifa ?!. Ushoga na usagaji mbaya ktk jamii yetu, lakini halikuwa tatizo la taifa kwa kiasi hicho . Mpaka pale mtoto mpendwa alipooanza kuwatishia amani. Tukubali approach ya Makonda sometimes ni tatizo kwa mstakbali ya nchi. Na ushahidi ni hapa.

Tatizo la utawala huu ni u dictator wa kudhani fikra za kiongozi ni sheria za kufuatwa na kila mtu. Hii si sawa kwa nchi ya ki democracy. Unyanyasaji unaofanyika kwa watu wenye mawazo tofauti na kiongozi ni mkubwa, na hili wafuasi wa huu utawala mnaliona kama jambo dogo. Haya hayakustahili kusubiria hao mabeberu wslisemee. Hili hata vikao vya ndani vya ccm vingeweza kulirekebisha. Lakini wapi ?!!!!.
Je na hili la kupitisha sheria kandamizi kwa lengo la kudhibiti wapinzani na watoa takwimu, mpaka tuwasubiri wazungu watusemee ?!

TUJIKOSOE NA KUJISAHIHISHA KABLA YA KUWALAUMU HAO MABEBERU.
 
Huitaj kuambiwa kuwa mtu mweupe ni adui wa ngozi nyeusi aliyejificha kwenye mwamvuli wa MISAADA mara kutetea democracy. Hao walioko ndani wako kisheria, nilifikir ungekuja na vifungu vya sheria kuonesha hawajatendewa haki kuweko huko ndani.Kuwa kiongoz wa siasa sio kinga ya kuishi utakavyo nje ya sheria. Kila nchi inataratibu zake ktk kufikia malengo. Haiwez ikawa nchi kama kila siku watu wanaamua kuandamana ovyo na bila sababu za mcng. Umeambiwa fanya siasa ktk jambo lako lkn hutaki unataka ukafanye siasa kwenye jimbo la mwenzio. Kwamba unataka kugundua nini huko?Mattz ya wananchi wako yameisha kiasi uone ni mda wa kwenda kwenye jimbo la mwenzangu?Rais kafuta sherehe za uhuru na hela kaagiza zijenge hospital, we unapinga oooh bunge halijapitisha so tuandamane na wakati unajua fika hilo swala hata lingeletwa huko bungeni lingepita. Hizi sio siasa uchwara?
Kawaambie EU sasa huku hamna msaada😂😂😂😂😂
 
Umetolewa mifano ya nchi zinaziminya democracy lkn hutaki unalazimisha kuvaa miwani ya mbao. Huko Uganda au Rwanda kuna democracy?Yaani umeshindwa hata kurudi Zimbabwe kilichomtesa Mugabe ni nini?Mtu mweupe kamwe hawezi kuwa na huruma na ngozi nyeusi.Oooh wanatupigania democracy, Mzungu akupiganie wewe?Yalikuwepo mabomu ya Arusha, kuteswa kwa kibanda, Ulimboka, kuuawa kwa Mwangosi na kupigwa vita kila siku kwa mikutano ya siasa. Je uliona matamko tuka huko Ulaya?Jibu ni Hapana na hoja ilikua ni UONGOZI uliokuwepo uliwawezesha KULA WATAKAVYO. Democracy haijaanza kuvunjwa leo,So hizi ni HASIRA za kubanwa tu.Najua vita ni ngumu lkn jpm kathubutu
Kikwete aliwahi kusema mtaishia jela? Uongozi unahitaji kauli makini sana anaweza kuwa na lengo zuri magufuli lakini kauli zinamponza unafikir wale hawana wadukua taarifa huku? Wakiwa ikulu anawaita wanaume wakisepa anawaita mabeberu watakufurahia? Lazima watafute namna ya kukuchomoa hii michezo huwa inachezwa kwa akili sana sio wazi wazi kama anavyofanya bwana mkubwa
 
Uchambuzi mzuri sana.
Uzuri wa vita hii Jemedari wetu Mkuu mhe.John anamjua adui na mbinu zake zote.
Watashindana lakini hawatashinda maana hata yule aliyeijenga misingi ya ulimwengu yuko upande wetu.
Kikubwa ni Watanzania kuwa wazalendo atakayeleta usaliti afanywe kama Kashogi-yes kwa faida ya taifa.
Mpuuzi
 
Simpendi jiwe ila kwa hili nipo pamoja na mleta mada

Wazungu sio watu wazuri hta kidogo

Ona walichomfanyia lumumba, kumefanya mpaka leo kongo haikaliki
Vipi kuhusu kwame nkurumah.ghadafi na wengine wengi waliofanyiwa hujuma,na,wazungu ili wakombe rasilimali zetu!!!

Narudia tena mzungu sio mtu mzuri
 
Huitaj kuambiwa kuwa mtu mweupe ni adui wa ngozi nyeusi aliyejificha kwenye mwamvuli wa MISAADA mara kutetea democracy. Hao walioko ndani wako kisheria, nilifikir ungekuja na vifungu vya sheria kuonesha hawajatendewa haki kuweko huko ndani.Kuwa kiongoz wa siasa sio kinga ya kuishi utakavyo nje ya sheria. Kila nchi inataratibu zake ktk kufikia malengo. Haiwez ikawa nchi kama kila siku watu wanaamua kuandamana ovyo na bila sababu za mcng. Umeambiwa fanya siasa ktk jambo lako lkn hutaki unataka ukafanye siasa kwenye jimbo la mwenzio. Kwamba unataka kugundua nini huko?Mattz ya wananchi wako yameisha kiasi uone ni mda wa kwenda kwenye jimbo la mwenzangu?Rais kafuta sherehe za uhuru na hela kaagiza zijenge hospital, we unapinga oooh bunge halijapitisha so tuandamane na wakati unajua fika hilo swala hata lingeletwa huko bungeni lingepita. Hizi sio siasa uchwara?
Polisi anampiga akwelina kisha kesi anapewa mbowe hivi uko timamu wewe? Hapo ndipo tunashindwa kwenda sawa ili mzungu afungiwe vioo kwa post za kipuuzi kama hizi mnakaribisha maadui bila kujijua kuwa na akili timamu mambosasa alikiri polisi kupiga mtu risasi mwisho akabadilika baada ya kuona mambo yatawaendea vibaya hamna vipofu shwaini wewe.
 
Simpendi jiwe ila kwa hili nipo pamoja na mleta mada

Wazungu sio watu wazuri hta kidogo

Ona walichomfanyia lumumba, kumefanya mpaka leo kongo haikaliki
Vipi kuhusu kwame nkurumah.ghadafi na wengine wengi waliofanyiwa hujuma,na,wazungu ili wakombe rasilimali zetu!!!

Narudia tena mzungu sio mtu mzuri
Ngozi nyeupe yoyote haijawahi kuwa rafiki kwa mweusi hapo zambia tu nchi inaporwa na mchina

Tatizo kauli zake zinamponza na kutesa wenzie bila sababu mwisho wa siku unatengeneza genge la maadui toka ndani kwako hadi nje

Raisi anasema mtaishia gerezani tena mbele ya hadhara unafikir hamna watu waliotafsir ile hotuba?

Wazungu wakija ikulu anawaita wanaume wakienda kwao anawaita mabeberu tena hadharani hizi kauli zinamadhara makubwa sana kikwete alipiga sana wapinzani lakini alikuwa smat kwa kauli zake aliejuu yupo juu tu
 
Mkuu hizo ni siasa za Africa. Swala ni kwanini hao wazungu wanaiona Tanzania tu?Na history inaonesha kiongoz yyt aliyekinyume na maslai ya mzungu lzm apigwe vita ila aliyesawa naye hata kama hakuna democracy lazima wamuunge mkono. Huoni kuna la zaidi nje ya wanachoita HAKI ZA BINADAMU?

Uko sahihi, sasa ni kipi kinafanya kiongozi wetu kama ana nia njema awafanyizie uhayawani wasiokubaliana naye? Ni kipi kinafanya afanye makosa ambayo hao wazungu watatumia kama kigezo cha kumuadhibu? Kama anadhani kuongoza nchi ni kuitetea ccm basi acha wazungu wamfanyizie na sisi tunaona hao wazungu wako sawa.
 
Kikwete aliwahi kusema mtaishia jela? Uongozi unahitaji kauli makini sana anaweza kuwa na lengo zuri magufuli lakini kauli zinamponza unafikir wale hawana wadukua taarifa huku? Wakiwa ikulu anawaita wanaume wakisepa anawaita mabeberu watakufurahia? Lazima watafute namna ya kukuchomoa hii michezo huwa inachezwa kwa akili sana sio wazi wazi kama anavyofanya bwana mkubwa
Kwani wewe unafiki wasiotii sheria wataishia wapi?Lipumba alipigwa kipindi cha nani?Hivi ulishwah angalia clip ya vurugu za Arusha?Au unajiropokea tu kuhusu jk?
 
Polisi anampiga akwelina kisha kesi anapewa mbowe hivi uko timamu wewe? Hapo ndipo tunashindwa kwenda sawa ili mzungu afungiwe vioo kwa post za kipuuzi kama hizi mnakaribisha maadui bila kujijua kuwa na akili timamu mambosasa alikiri polisi kupiga mtu risasi mwisho akabadilika baada ya kuona mambo yatawaendea vibaya hamna vipofu shwaini wewe.
Nafikiri wewe ndio hauko timamu. Mbowe anamshtaka mangapi huko mahakaman?Hujui kuandamana bila kutoa taarifa polisi ni kosa kisheria?Mbowe alitoa wapi taarifa ya kuandamana zaid ya saa 12 jioni?Huoni hapa tu kuna kosa hata wakisema wamfutie makosa mengine?Unaruhusiwa kudai HAKI na ni HAKI yako ya msingi lkn kuna taratibu zake ktk kudai HAKI. Je ukikiuka hizo taratibu sio kosa kisheria?
 
Uko sahihi, sasa ni kipi kinafanya kiongozi wetu kama ana nia njema awafanyizie uhayawani wasiokubaliana naye? Ni kipi kinafanya afanye makosa ambayo hao wazungu watatumia kama kigezo cha kumuadhibu? Kama anadhani kuongoza nchi ni kuitetea ccm basi acha wazungu wamfanyizie na sisi tunaona hao wazungu wako sawa.
Kawafanyia nini?
 
Kwani wewe unafiki wasiotii sheria wataishia wapi?Lipumba alipigwa kipindi cha nani?Hivi ulishwah angalia clip ya vurugu za Arusha?Au unajiropokea tu kuhusu jk?
Narudia tena ulimuona akisema mtaishia gerezani? Uliwahi kumsikia anajiapiza kwenye utawala wangu hili halifanyiki? Uliwahi kusikia anawaita mabeberu?

Wale jamaa wanatune taratibu tu mtu alambe matapishi yake ulimi uliponza kichwa kwani anagekuwa na misheni zake za kufunga wakina mbowe nani angajua kwa nini alopoke hadharani? Ujue anawatia hadi majaji kweye wakat mgumu pengine kesi inaweza kuwa mpinzani anakosa lakin kishasikia mtaishia gerezani unafikir nani ataikubali hukumu? Amka wewe pompi
 
Back
Top Bottom