Problem tuliyonayo watu wengi wamekuwa mateka wa propaganda za upinzani.
Ukiuliza kosa la Maghufuli,
-watakwambia dikteta! Sijui dikteta wanamjua? Na anayeongoza kuwaaminisha hivyo anatawala chama chake kidikteta! Anang'ang'ania madaraka kwa kujenga ufalme badala ya utaasisi.
-Watakwambia anaminya uhuru wa habari, alafu kila siku hapa JF wanamtukana matusi yasiyo na idadi!
Ukweli ni kwamba Maghufuli anapendwa na watu wa chini ambao ndiyo wengi sababu anatekeleza ahadi kwa kasi ya ajabu. Wapinzani baada ya kugundua kwa njia ya kura hawawezi kushinda, wakabuni njia ya kumchafua hasa kwa mataifa ya nje. Yaani wanatanguliza ulafi wao wa kushika madaraka kwa kuhatarisha maendeleo na usalama kwa watu wote.
Sijawahi kuliwaza hili, lakini Sasa hivi nimeanza kuelewa kwa nini states huwa zina wapoteza wasaliti kwa njia mbalimbali!