Kwanini Tanzania tuko kwenye orodha ya nchi zisizo na furaha? Je, ni kweli hatuna furaha?

Umeshatembea nchi ngapi mwenzetu?
 
Yaani Somalia iwe na furaha kuliko Tanzania ! Au Kenya wawe na furaha kiko Tz wakati raia wa kawaida wa kenya hata kipande cha ardhi cha nusu eka hana. Hayo tunalishwa matango pori wala hakuna ukweli wowote. Huo utafiti wao umesukumwa na hasira ya kukosa rasilmali zetu
 
Tunayo furaha tena sana tu
 
Hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kuwaajiri wahitimu wote wa vyuo vikuu. Never ever
 
Hajui kwamba hata marekani kuna Bush junior na Bush senior wote walikuwa maraisi wa marekani ! Anatafuta usawa duniani ataupata wapi ! Hata huko mbinguni hatutakuwa sawa
 
Hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kuwaajiri wahitimu wote wa vyuo vikuu. Never ever
Sawa serikali haiajiri ila sekta binafsi inakuwa na uwanda mpana wa kuajiri huku serikali ikifanya monitoring ya hio sector ili kuondosha unyonyaji. Pia serikali inawahudumia fully wananchi wasio secure kazi kwa kuwapa chakula toka government reserves ama stipends za mwezi kwa ajili ya kufinance kodi.

Serikali iko fully responsible kupitia asasi zake. Inakusanya kodi ila kodi zinafanyiwa evenly distribution. Kwanini wenzetu inawezekana kwao sie kwetu ishindikane? Kuna shida mahali yani.

Imagine mwananchi anatakiwa a file tax individually kila mwaka. Kazi zipo japo si zote ni za maofisini zingine ni maviwandani ila wame standardize malipo ya kima cha chini. Huwezi kutumia masaa 12 ya mtu ukamlipa sh.5000 huo upuuzi uko Tanzania tu.

Unachomlipa mtu lazima uhakikishe kinaenda na standards za maisha, kinaweza kumlipia rent na bill za mwezi na kumuachia chenji kwa ajili ya kujiletea maendeleo binafsi.

Sasa upuuzi wa huku kwetu muhindi anaingiza billions in a year na kukwepa kodi ila mishahara anayolipa watu ni ya kinyonyaji kiasi kwamba mtu akidunduliza kulipa kodi tu na nauli hela imeisha anakuwa anafanya kazi ya kukusanya hela na kulipa kwa landlord akiumwa tu ni madeni sababu hana saving. Furaha itatoka wapi?

Vijana wamefikia umri wa kuoa ila kazi hakuna. Utaoa mke ukamlishe nini? Una hamu ya kuwa na familia yako uitunze ila huna jinsi furaha itatoka wapi?

Haya yanafanyika serikali ikiwa macho tu. Kama vile watu hawajatembea wakaona. Ubinafsi uliokithiri sababu wao wana allowances na kulipwa mishahara minono wanahisi kila mtu yuko kwenye same ride.
 
Ukusanyaji mapato lazima uzingatie welfare ya wananchi pia.

Kumkamua mzalishaji au kampuni zinazoendesha shughuli zake kwa kukomoa haisaidii. Unaweka targets ambazo haziendani na uhalisia ni kuua sector binafsi. People have to feel proud of paying the government taxes sababu zina positive impacts kwao.

Furaha itakuja endapo basic needs zinakuwa ascertained na sambamba na maendeleo.

Natamani serikali yetu ya wanyonge ione umuhimu wa muda wa wananchi. Tu adopt mfumo wa kulipana kwa masaa rasmi.

Haiwezekani ukifanya mradi wa mzungu aweze kukulipa kati ya elfu 50 mpaka laki 2 kwa masaa 8 ila mtanzania mwezio akulipe 5000 kwa masaa 12! Huu ni unyonyaji na kutoheshimu fani za watu.

Serikali iangalie gharama za maisha za sasa na ku standardize mishahara iendane na hali halisi. Sio unalipwa laki 4 ila cost za maisha ni laki 6 kwa mwezi. Una accomodate vipi? Furaha itatoka wapi?

Unasema watu wajiajiri ila masoko yatakayotokana na uzalishaji wao yako katika mikono ya madalali walafi. Ukahenyeke kulima huko uje ugawane hela na dalali?
 
Umeshatembea nchi ngapi mwenzetu?
kitendo cha kuuliza huu upumbavu inaonekana kiasi gani umekua affected na kukaa vijiweni na low self esteem ndo maana rahisi kupelekwapelekwa...nshazunguka schengen countries na baadhi ya east african countries,...ila hainizuii kuchambua na kujua lipi sawa lipi unyumbu
 
Well said
 
Sisi wafanyakazi tunakatwa direct tax kwenye PAYE na Kodi nyingine indirectly, mbaya zaidi mtu na chuki zake anakuja kusema eti atatunyima miundombinu kwasababu eti hatukuchagua chama chake
 
Akili za chadema ni za kijinga sana. Unasema huwezi semea watanzania halafu hapo hapo unasema, njiani hawana furaha, familia yako hawana furaha, kwenye daladala hawana furaha, mwendokasi hawana furaha, daaaaaah. Kwa hiyo hao uliowasemea ni mbuzi?
 
Schengen States??? Ulienda via VPN servers
 
Akili za chadema ni za kijinga sana. Unasema huwezi semea watanzania halafu hapo hapo unasema, njiani hawana furaha, familia yako hawana furaha, kwenye daladala hawana furaha, mwendokasi hawana furaha, daaaaaah. Kwa hiyo hao uliowasemea ni mbuzi?
Sasa hizo ndio akili za CHADEMA? Je CHADEMA ndio walifanya utafiti na kugundua kuwa Tanzanians are not happy? Basi na nyie leteni utafiti wenu unaoonesha ni kwanini Watanzania wana furaha na muandae orodha yenu ya nchi zote duniani
 
Sisi wafanyakazi tunakatwa direct tax kwenye PAYE na Kodi nyingine indirectly, mbaya zaidi mtu na chuki zake anakuja kusema eti atatunyima miundombinu kwasababu eti hatukuchagua chama chake
Unapataje furaha sasa
 
Wakati DR Congo haipo huu ni uchochezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…