Kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika?


Acha kupotosha watu na kuharibu Neno la Mungu kwa kuchomoachomoa vifungu na kuvipatia maana unayoitaka wewe, kama vile imeandikwa leo au juzi biblia sio gazeti kwamba unaamka tu na kujipatia tafsiri..

hiyo ufunuo wa yohane 22:18-19. Haina maana kama unavotaka kutiaminisha hapa. Kajifunze historia ya icho kitabu cha ufunuo, mazingira ya uandishi wa icho kitabu cha ufunuo, kwanini kiliandikwa, mazingira na maisha ya walengwa wa icho kitabu nk.

Kukusaidia tu ni ivi:

ufunuo 22:18-19 inayohusu agizo la biblia la "usiongeze wala usipunguze neno".

ni ivi ndugu kipindi ivo vitabu vya biblia vinaandikwa hakukuwa na technologia ya uchapishaji au "copy and paste" kama ilivo leo. kumbe ili kupata copy ya kitabu (gombo) wao walichokuwa wanafanya ni ku-nakili kwa mkono, mikono yao ndio iliokuwa iki-nakili neno hadi neno, herufi hadi herufi mpaka kitabu kizima kinakamilika.

kazi hiyo ya kunakili ilikuwa inafanywa na watu maalumu waliojulikana kama "waandishi au waalimu wa sheria kwa jina lingine" (wanaitwa waandishi kwa sababu ya kazi hiyo ya ku-nakili maandiko ila kimsingi ndio hao walimu wa sheria).

kumbe basi baada ya kumaliza kunakili kitabu husika ilikujua kama kazi "nakala" HAIJACHAKACHULIWA, HAIJAONGEZWA WALA KUPUNGUZWA, HAINA MAKOSA(kama kukosea neno, kuruka au kusahau neno/herufi, nyongeza au upungufu wa maneno nk) walitafuta idadi ya maneno kwa kuhesabu neno hadi neno kisha walioanisha na idadi ya maneno kwenye gombo husika kama yana lingana au la. yakilingana basi iyo nakala inakuwa ni sahihi, idadi ikitofautiana hata kidogo basi iyo nakala inakuwa na mapungufu "au imeongezwa au imepunguzwa au ujumbe/maana imeharibiwa"

baada ya maelezo hayo hapo juu utagundua kuwa ufunuo 22:18-19. hazina maana ya mantiki unayotaka kutuonesha hapo juu. ila waandishi wanataka kulinda na kutunza jumbe/unabii wa vitabu vyao usiharibiwe "usiongezwe wala usipunguzwe". huku kwetu leo tunaita hati miliki "copyright".

Zaidi kajisomee pia torati 4:2
 
Sio Kweli hata kidogo Mkuu!
Moja ya Hoja ya Council of naecea ni kutafuta Jina la Hiyo siku Na Majira yake..
Na Pasaka haikuwahi kuitwa Easter ilikuwa ikiitwa Pasaka Means Pass over..
Pass over ni ukumbusho wa wana wa israeli kutoka misri utumwani. Sisi ni wakristo tuliokombolewa toka katika utumwa wa dhambi na kristo mwenyewe kwa kifo chake msalabani na ufufuko wake, hiyo ndio passover yetu kama wakristo (na sio wayahudi). Hata mtume paulo mwenyewe anasema hayo yote yalikuwa ni kivuli cha yale yajayo yaani kristo.

wewe unataka uendelee kufanya pass-over kwa kukumbuka ni nini ?
 
Hiyo ni pasaka ya wayahudi (pass over), wakifanya kumbukumbu ya kutolewa utumwani misri.

Swali, wewe kama mkristo unataka ufanye passover, pasaka ya kiyahudi kwa kumbukumbu ipi, kwa kukumbuka nini ?.
 
Ikabodi ni neno jumuishi kama jibu la aya uliyoiandika hapa.
 
Hiyo ni pasaka ya wayahudi (pass over), wakifanya kumbukumbu ya kutolewa utumwani misri.

Swali, wewe kama mkristo unataka ufanye passover, pasaka ya kiyahudi kwa kumbukumbu ipi, kwa kukumbuka nini ?.
Yesu alifanya karamu ile siku ya Pasaka ya Wayahudi kwa kukumbuka nini?
 
Kwani Easter maana yake ni nini?
The exact origins of the word "Easter" are unclear, but it may derive from Eostre, a pagan goddess of spring and fertility, whose festival was celebrated around the same time as the Christian observance of Easter. Over time, Christian traditions blended with pagan customs, leading to the modern celebration of Easter.
 
HIyo Pasaka ya kwanza Iliwekwa na Mungu mwenyewe Na kutangaza Tarehe, hiyo paskaa ya Pili aliiweka Nani?
Na unajia Chimbuko Lake??
Pasaka ya pili iliwekwa na kristu mwenyewe kwa kifo na ufufuko wake akafuta pasaka ya kiyahudi na kutipatia pasaka mpya kama ukumbusho wa sisi kutoka katika utumwa dhambi kureplace pasaka ya kiyahudi ya kumbukumbu toka utumwani misri.
 
HIyo Pasaka ya kwanza Iliwekwa na Mungu mwenyewe Na kutangaza Tarehe, hiyo paskaa ya Pili aliiweka Nani?
Na unajia Chimbuko Lake??
Pasaka ya pili iliwekwa na kristu mwenyewe kwa kifo na ufufuko wake akafuta pasaka ya kiyahudi na kutipatia pasaka mpya kama ukumbusho wa sisi kutoka katika utumwa dhambi kureplace pasaka ya kiyahudi ya kumbukumbu toka utumwani misri.
 
Tarehe 14 ya mwezi upi wa kalenda ya sasa ?.

Lete ushahidi kuhusu council ya Naecea kubadili hiyo tarehe ya pasaka.
Tarehe 14 ya mwezi wa Nissani Mkuu kalenda ya kiyahudi..

Ushahidi kuhusu Council of Naecea Tafuta Decree zote za Council of Naecea soma Decree ya Pili..


 
Hivi ni kweli wayahudi hawaamini kuhusu Yesu hadi leo? Wanaamini nini kuhusu dini na Wana mitume gani kama hawaani Yesu?
Je wanaamini nini kuhusu mtume Muhammad?
 
Pasaka ya pili iliwekwa na kristu mwenyewe kwa kifo na ufufuko wake akafuta pasaka ya kiyahudi na kutipatia pasaka mpya kama ukumbusho wa sisi kutoka katika utumwa dhambi kureplace pasaka ya kiyahudi ya kumbukumbu toka utumwani misri.
Naomba uthibitisho mkuu!
 
Mkuu, hapo ukisoma hakuna maelezo kuwa watu washerehekee eid. Ukisoma mitandaoni kupata origin ya sherehe ya eid el fitr wanaeleza kuwa ni Mtume SAW alikuwa akisherehekea ushindi wa vita ya Badr.

Kwa hiyo unakuta haihusiani chochote na mwezi wa Ramadhan (kufunga) ingawa vita hiyo ilipigwa kipindi cha mwezi wa Ramadhan

Ni sherehe ya kidesturi tu lakini sio ya kidini (kwa maana ya agizo)
 
Yesu alifanya karamu ile siku ya Pasaka ya Wayahudi kwa kukumbuka nini?
Kasome vizuri huo mstari, kuna mahali kumeandikwa "kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi", Yesu kama myahudi ulitaka aishi kinyume na taratibu zao alizozikuta ?.

Wakati wa hiyo pass-over ya kiyahudi Yeye mwenyewe alisema "Fanyeni ivi kwa ukumbusho wangu" unaelewa hata maana ya maneno hayo ?. Hakusema fanyeni ivi kwa ukumbusho wa toka utumwani misri. Ni "fanyeni ivi kwa ukumbusho wangu." Na baadae paulo mwenyewe anasiaitizi hayo yote pasaover, na desturi zingine zote za kiyahudi zinazoonekana kwenye agano la kale zilikuwa ni kivuli cha yale yajayo (kristo).

onesha hapa kuwa yeye au wafuasi wake wanafunzi waliendelea kufanya iyo pasaka ya kiyahudi baada ya kifo na ufufuko wake (yaani kutukomboa toka katika utumwa wa dhambi). Na kama hakuemdelea kuifanya hiyo pasaover ya kiyahudi ni kwanini ?
 
mwandamo wa mwezi unahusika kwa mahesabu ya Kikatoliki.Wakatoliki ndo wamiliki wa Biblia na sikukuu zote za Yesu.
 
Sasa mie naeauliza mwakani pasaka itakuwa tarehe ngapi na mwezi ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…