Pre GE2025 Kwanini TBC hawarushi Live Mkutano Mkuu wa CHADEMA? Je, hiki ni chombo cha CCM au Watanzania wote?

Pre GE2025 Kwanini TBC hawarushi Live Mkutano Mkuu wa CHADEMA? Je, hiki ni chombo cha CCM au Watanzania wote?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa issue muhimu kama hii yenye maslahi kwa umma na chombo hiki kinajinasibu kuwa chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi kinaona kipindi cha Lulu za kiswahili ni muhimu kuliko mkutano huu! Ingekuwa ITV hapo sawa, maana ni chombo binafsi, ila TBC ni chombo cha umma!
 
Hahaha Team Lisu mnatafuta cha kuongea.

Wakirusha mnasema Mbowe kawaagiza.

Twendeni hivyo hivyo na simu zetu za Tochi.
 
Je chama kimelipia kurusha matangazo? Au walienda kuomba mkutano urushwe wakakataa? Hivi unajua gharama ya kurusha matangazo MUBASHARA kwa siku ni bei gani? Taasisi ninayofanyia kazi mwaka jana tulikuwa na mkutano mkuu mwaka tulifanyia Arusha, tuliwapa hao TBC milioni 7 kwa siku moja ili kurusha matangazo na hapo lazima kufanya booking may be siku 3 kabla, sasa je CDM waliomba kurushwa matangazo TBC wakakataliwa? Au unadhani ni bure
Ila uchaguzi wa CHADEMA umefatiliwa na watanzania wengi na kwasababu hiyo ungetakiwa kuoneshwa mbashara. Msema kweli ni taarifa ya habari ya usiku ambayo mara nyingi hutakiwa kuwa habarisha wananchi kuhusu matukio muhimu ya siku
 
Back
Top Bottom