Kwanini TIGOPESA wananilazimisha nitoe pesa kwenye akaunti yangu?

Kwanini TIGOPESA wananilazimisha nitoe pesa kwenye akaunti yangu?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Tangu tozo mpya zilipoanza nimesusa kutoa pesa kwenye akaunti yangu, chakushangaza Tigo wamekuwa wakinitumia ujumbe nitoe pesa vinginevyo wataifunga! Wakiifunga inamaana wao watakomba pesa yote ndani ya akaunti yangu?

Na kwanini wakombe wakati mimi niko hai kwani namba yangu ya Tigo ninaitumia kila siku, na mimi nasema LIWALO NA LIWE, ila tozo ng'o.
 
Ata picha ya vocher ya tigo kusindikiza thread hamna
 
Uongo hauna maana watakulazimoshaje kutoa pesa .?
 
Tunaomba hata reference.

NB: Tigo wanakuhurumia huenda kunaongezeko jingine la tozo
 
Je, hiyo laini unatumia kila siku kwa mawasiliano? If yes wewe komaa tuu na wakiifunga waburuze kwa pilato.
 
Mbona mimi sijatoa pesa tigopesa muda na sijawahi kutumiwa hiyo text
 
Back
Top Bottom