Kwanini timu zinazomilikiwa na majeshi hazidumu kwenye ligi na zina matokeo mabovu?

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,705
Reaction score
4,217
Kwanini hizi team uwa hazidumu kwenye ligi na zinaongoza kwa matokeo mabaya??Na sio Bongo pekee ni E.Africa ndo tuna ili pepo la team za majeshi ligi zilizoendelea kiafrica kama S.Africa na Egypt,Morocco,Algeria amna team za majeshi.Huko duniani EPL hata tusifike kabisa..

Pia zinaongoza kwa kucheza vibaya(Rafu) mfano msimu wa 2021/2022 team nyingine zililamika sana na pia mashabiki walilalamika unakuta game ni viatu(Rafu) mwanzo mwisho hakuna fair play..JE!! Ni kwakuwa wachezaji wa team izo wanaamini katika UBABE UBABE kutokana na mazoezi ya kijeshi wanayopitia?

MFANO:
TZ
~Polisi Tanzania(iko mkiani)
~JKT Tanzania(Ilishuka daraja)
~Ruvu shooting(inapumulia gesi mkiani)
~Tanzania prisons(Angalau ila Inashika nafasi ya 10)

Pia Uganda
~UPDF(iko hatarini kushuka)
~Black powers(inashika mkia)

Kenya
~Kenya police(Nafasi ya 5)
~Ulinzi stars(ya 8)

USHAURI:
'Nashauri hizi timu za majeshi ziwekeze kwenye michezo mingine kama Ndondi(Boxing).Wanaweza kuingia mkataba na Azam TV.. kwenye Boxing wanafanya vizuri sana sana.
~Selemani Kidunda
~Rashid mfaume
Na wajeda wengine tunaowaona Azam TV kwenye VITASA wanafanya vizuri sana wawekeze huko labda kuna siku watatoa mwanamasumbwi atakaeipeperusha bendera kama ISRAEL ADESANYA alivyoipeperusha bendera ya wanigeria.

WAKO MTIIFU,KENGE
NAWASILISHA
.
 
Mishahara ya wachezaji hasa raia mpaka wakatane wao( Maafande) ndio upewe tarehe 38.
Inakubidi ukapige ndondo then kesho game lazima kuharibu na kuchoka ligi ikiwa mbichi km sio injuries.

Matumizi makubwa ya nguvu na hisia kuliko akili.

Mazoezi ya mpira lazima yahusishe mpira ila wao hayahusish wanakomaa na endurance na physical fitness.
Tech n Tactics weupe.

Wachezaji wakiwa masoja jua imeisha hiyo.
Ajisumbue ili iweje na kashakula namba ya ajira.

Kuna Majungu na makundi Kama kawaida.

Nidhamu ya wachezaji kwenda kwa Walimu huwaga ni ndogo hasa mwalimu akiwa raia.

Kutunza na kuongeza kwa kile Wanachopewa Huwa hawana hy kariba.
Angalia Quality Yao itakuinesha kuwa hata training session zao si bora.

Kuna wauwa ndoto wengi ambao walishatupwa mkono na game still anakomaa kikosini na wengi ndio wale mnawaita wakongwe Hawa ni Virusi na wajuvi balaa.

#Acha niishie hapa.
 
Umemaliza kila kitu hasa kwenye (Mazoezi na mshahara)

Kazi ipo
 
Mtoa mada unaijua, Association sportive des Forces armées royales a.k.a Far Rabat

Misri kuna timu za majeshi El Entag El Harby Sporting Club, Botswana kuna Botswana Defence Force, Russia, Gambia mpaka Spain zipo.

Issue ni perfomance ya timu za Bongo ila siyo kitu kibaya majeshi kuwa na timu. Mfano Rwanda APR inamchango mkubwa sana kwenye mpira wao.
 
Sio mbaya ila zina kariba ya kufanana mfano zinacheza rafu sana

Umesema na spain zipo??em taja hata moja inayocheza laliga
 
Sio mpira tu, hata shule zao tazama matokeo. Hasa hapa kwetu.
 
Falasafa yao ya usajili sio ya ushindani,ni ya michezo ya ridhaa huko wangefanikiwa.
 
Sio mpira tu, hata shule zao tazama matokeo. Hasa hapa kwetu.
Kishule angalau kwani Jite inamatokeo mabaya?? Ila kuna chuo cha Afya Lugalo sio mbaya sana
 
Falasafa yao ya usajili sio ya ushindani,ni ya michezo ya ridhaa huko wangefanikiwa.
Labda kunawapigaji sana kama pesa zinatoka serkalini na kama team inajiendesha basi kuna Umaskini mkubwa sana
 
Hizo timu zinaendeshwa na michango makato ya mshahara toka kwa askari husika so wanazipiga vita chini chini
 
Uendeshaji wa timu ni gharama sana sio mchezo hasa ukitaka kupata wachezaji wenye viwango
Kweli aisee pia kuongeza wafanyakazi mfano team kubwa Simba,Yanga,Azam zinawatu maalum wa Analysis & Statistics na kuchambua kila game.ila team za Apache Alolo na majeshi amna watu hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…