Kwanini traffic akikusimamisha huomba leseni, kadi ya gari n.k?

Sasa wewe unakereka na nini au ulitaka akuombe cheti cha ndoa?
 
Hamna wako kzn..kama kazi zingine..anakuuliza lesen ili umpe ..next anakutafutla kosa.
Ukishindwa kumtoa na buku 2..anangangania leseni..mi huwa cwapi walishapoteza lesen yangu mikese 1997..csahau.waliingangania nikawa cna pesa.kurudi baada ya wki kulipa fain lesen haionekani..nikaanza kutafuta dublicate..
 

ndugu,mimi sio trafic ila kwa kukuliza hayo maswali kama kadi ya gar na lesen kama n vya wizi wanaweza kuvibain kwa wasiwasi utakaokuwa nao
 
hizi leseni za kutafutiwa na Anko ....
 
ndoo sheria kaka soo inakubidi uvumilie tuu na kuzoea,
 
Mkuu hujui kuna watu wanaendesha magari bila leseni? Ndo maana wanauliza

Fire extingusher ni muhimu na sio kuwa nayo tu inabidi iwe nzima moto unaweza tokea muda wowote hata kama sio kwako kwa dereva mwenzako. Kuna wengine wana makopo tu ila ndani hamna kitu.

Upande wa kadi ya gari hapo ndo kuna utata
 
Kama unakosa hivyo vitu ni kosa na kama unakosa unategemea nini kama si kuchukuliwa hatua? Kama unaona unaonewa usilipe hiyo fine waambie tu kua unataka kesi yako iende mahakamani ili mkagaragazane huko weeeee hadi haki ipatikane.
 
Labda atakua anamiliki gari ya wizi huyu ndiyo maana ana wasiwasi km gaidi
 
Saa ingine unakuta mtu hajafunga akichukuliwa hatua analialia, anaendesha pikipiki bila kofia ngumu napo akichukuliwa hatua anakua mkali. Hivi ukipata ajali majeraha atayapata traffic au kichwa cha traffic ndiyo kitapasuka ukianguka na hiyo pikipiki? Uoni traffic anapokuchukulia hatua ili ufate sheria mfaidika ni wewe na wala siyo yeye? Alafu ukipata madhara kwa uzembe wako unaanza oh hawa traffic hawafanyi lolote wamesimama barabarani km nguzo za umeme tu.
 
Ni kawaida trafic kuomba hivyo vitu,, ni sawa na wew ukitongoza mwanamke unavyoomba ,,kujua jina lake,, kabila lake,, mahali anapoishi,, na namba yake ya simu nk.
 
kwa siku hizi sababu pekee ya kudai kadi ni kuangalia 'uzito' wa jina lako na la mwenye gari, kabla hajaanza kukuzingua!
Mkuu nakubaliana na ww kabisa trafiki akijua kadi ya gari ina jina la mzito wa serikalini huwa wanakuwa na adabu sana
 

We hamnazo kabisa. Tena siku hizi hamuombi, manataka rushwa kwa lazima. tena usinikumbushie machungu wewe.
 
Kwa mataifa yalioendelea /mfano Kny Askari anakagua stika ya inspection /bima/windscreen kama iko Safi tairi /kama uko vizuri hata license hakuulizi, lkn akiona kosa Mojawapo atakuitisha leseni, for Tanzania bado sana kufika huko
 
Wewe ushawahi kutoa Rushwa?
Tena kwa lazima la sivyo inakula kwako, nipo na haraka nawahi airport, nataka kuwahi taa nikachelewa nikajikuta nimesimama mbele ya msitari wa stop. wakadai faini sh 30000 papo kwa hapo, au lete mwekundu usepe. ukiangalia saa mbaya, gari umepaki kando alafu wenyewe wala hawana haraka. Shikamoo kaka trafik.
 
Kwahiyo ulikuwa na kosa na haukutaka kufata utaratibu wa kawaida wa kulipa faini..

Sheria ya Rushwa inasema anaetoa na kupokea wote wanamakosa

Kwani ungemwambia niandikie faini alafu ukaondoka angekulazimisha au ulitaka mteremko ndugu?
 
Nadhani tusome kwanza sheria ndio tuanze mjadala wa suala hilo. Sheria ya polisi inasema pia kwamba askari aweza kukagua chombo cha usafiri wakati wowote ule. Lakini hiyo ya kaunzia kwenye leseni na kadi sina ufahamu nalo. Lakini kwa trafki wengi wa tz ni wala rushwa na wala tusifiche. Vitu hivyo vinakuwa kama ATM kadi ya chain zao. Na hata kama wakikukuta huna kosa watakuambia MZEE hata ya Maji huachi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…