Kwanini traffic akikusimamisha huomba leseni, kadi ya gari n.k?

Kwanini traffic akikusimamisha huomba leseni, kadi ya gari n.k?

muhogomtamu

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
412
Reaction score
69
Ndugu wanajamvi,

Binafsi nakerwa sana na ninaposimamishwa na traffic kisha kuombwa leseni, kadi ya gari na wakienda sana ni fire extinguisher na triangle! vitu hivi ni muhimu kuwa navyo na hasa ni kwa usalama wa mmiliki wa gari.

Hainiingii akilini kama mimi mtu mzima natoka na gari yangu umbali mrefu naingia barabarani mwenyewe halafu sijithamini usalama wangu! nikishamuonesha kadi ya gari, ama leseni, yeye kikazi inamsaidia nini?!

Fire extinguisher siku hizi lazima ulipie kupitia re-licensing, sasa kwa nini watu hawa huulizia hii kitu, utakuwa mwendawazimu kiasi gani ulipie fire extinguisher kisha uishie kutokuwa nayo?

Napata maswali mengi sana juu ya taaluma hii, ndivyo maelekezo ya kazi yao au WANAPASWA KUELIMISHA JUU YA USALAMA BARABARANI?!

Wanajamvi naomba anayefahamu sana mambo haya anielimishe, I am tired, karibu napaki gari zangu, nianze kutembea kwa baskeli. asanteni.
 
Mkuu ulitaka ukisimamishwa barabarani uulizwe cheti cha ndoa au?
Wakati ukijifunza udereva hukuambiwa kwanini askari wa usalama barabarani wanastahili kuuliza particulars za gari lako?
Hebu weka picha basi ya unazoita gari zako isije kuwa

800px-Bush_taxi_station_wagon_type.jpg
 
Mkuu ulitaka ukisimamishwa barabarani uulizwe cheti cha ndoa au?
Wakati ukijifunza udereva hukuambiwa kwanini askari wa usalama barabarani wanastahili kuuliza particulars za gari lako?
Hebu weka picha basi ya unazoita gari zako isije kuwa

800px-Bush_taxi_station_wagon_type.jpg
Sio kwamba waniulize cheti cha ndoa kama unavyosema, ila napata shida kulink kuwa na kadi ya gari na leseni wakati naendesha gari na jukumu lao la usalama barabarani. Kwa mfano, kadi ya gari inanisaidia nini katika kuendesha gari langu?! mimi nilitegemea anishauri kwa mfano, kunikumbusha walau matairi yangu yameisha na hivyo ni hatari kwa usalama wangu, na sio kusema "huna kadi ya gari" faini sh..... nini hiii?!?!?!?!?!?!? binafsi napata shida sana, hawana mambo mengine ya kukagua barabarani? over speed nakubaliana nayo, ila vitu vidogo vidogo kama kadi, NO au eti abiria wako hajafunga mkanda, faini elf 30!!!! is it logical?.
 
Sio kwamba waniulize cheti cha ndoa kama unavyosema, ila napata shida kulink kuwa na kadi ya gari na leseni wakati naendesha gari na jukumu lao la usalama barabarani. Kwa mfano, kadi ya gari inanisaidia nini katika kuendesha gari langu?! mimi nilitegemea anishauri kwa mfano, kunikumbusha walau matairi yangu yameisha na hivyo ni hatari kwa usalama wangu, na sio kusema "huna kadi ya gari" faini sh..... nini hiii?!?!?!?!?!?!? binafsi napata shida sana, hawana mambo mengine ya kukagua barabarani? over speed nakubaliana nayo, ila vitu vidogo vidogo kama kadi, NO au eti abiria wako hajafunga mkanda, faini elf 30!!!! is it logical?.

What if gari linamilikiwa isivyo halali, nenda mwenge Majembe pale Magari kibao ya maana yaliyokuwa na usajili wa piki piki kukwepa ushuru, wengine magari ya wizi so Plate no na kadi ni mguu wa kushoto na wa kulia ... let em do their work! Usilalamike labda iwe kuna kitu unaficha!
 
kwani mkuu hata hofisini kunakuwaga na sheria...!! hizo ni kati ya sheria hambazo mmiliki wa
gari anatakiwa kuwa nazo...

1- Mkanda
mkanda hata kama mtakuwa kumi ndani ya gari wote mwatakiwa kufunga mikanda kwaajili ya usalama.
2- Fire
sawa walipia kwenye road license, lakini kuna fire hambayo hutumia kuzimia gari watakiwa kuwa nayo...
usiwachoke kwani wapoa kwaajili ya usalama wetu.
 
muhogomtamu,
Mkuu, ukifuzu kuendesha gari unapewa leseni kama uthibitisho kwamba wewe ni dereva na sheria inakutaka kuwa na leseni hiyo kila wakati unapoendesha gari. Kadhalika ukinunua gari na kulisajili unapewa kadi kama uthibitisho wa uhalali wa gari lako na sheria inakutaka kuwa na kadi hiyo kwenye gari lako muda wote.Trafiki anatakiwa kuhakikisha unafuata sheria za barabarani zikiwepo hizo hapo juu ndio maana huwa wanauliza.
 
Kama ni usumbufu kuulizwa hivyo vitu basi endesha baiskeli au panda usafiri wa umma
 
Ndugu wanajamvi, binafsi nakerwa sana na ninaposimamishwa na traffic kisha kuombwa leseni, kadi ya gari na wakienda sana ni fire extinguisher na triangle! vitu hivi ni muhimu kuwa navyo na hasa ni kwa usalama wa mmiliki wa gari. Hainiingii akilini kama mimi mtu mzima natoka na gari yangu umbali mrefu naingia barabarani mwenyewe halafu sijithamini usalama wangu! nikishamuonesha kadi ya gari, ama leseni, yeye kikazi inamsaidia nini?! fire extinguisher siku hizi lazima ulipie kupitia re-licensing, sasa kwa nini watu hawa huulizia hii kitu, utakuwa mwendawazimu kiasi gani ulipie fire extinguisher kisha uishie kutokuwa nayo? Napata maswali mengi sana juu ya taaluma hii, ndivyo maelekezo ya kazi yao au WANAPASWA KUELIMISHA JUU YA USALAMA BARABARANI?! Wanajamvi naomba anaefahamu sana mambo haya anielimishe, I am tired, karibu napaki gari zangu, nianze kutembea kwa baskeli. asanteni.

Umesahau kuwa vilevile huuliza First aid kit
 
kwa siku hizi sababu pekee ya kudai kadi ni kuangalia 'uzito' wa jina lako na la mwenye gari, kabla hajaanza kukuzingua!
 
Usiwe mbishi hivyo vitu ni muhimu kuonesha kwa polisi. Sheria inataka wafanye hivyo. Magari kila siku yanaibwa. Unataka yasikaguliwe ili wezi wapate mteremko? Au na wewe ndio ...... ?!!!!
 
Ndugu wana jamvi,

Binafsi, sina tatizo na wao kuangalia au kukagua leseni, kadi ya gari, etc etc..... Tatizo langu ni pale wanapong'ang'ania hivyo vitu wanapokosa cha kusema. Atalizunguka gari lako mara tano kama anasindikiza harusi, ameshikilia leseni yako na kadi... baadaye akikuona hubabaiki anakukabidhi na safiri salama.

Jambo lingine ni kujiuliza wanafanya nini na hivyo vitu. Kama wangeunganishwa na mtandao wa kuweza kuuliza uhakika wa hivyo vitu ningeona sababu ya kufanya hivyo. Lakini kwa sasa hata ungekuwa na kadi feki, leseni feki, etc etc hawawezi kujua. Kwa nini usumbue madereva???
 
Polisi wa usalama barabaran anapokusimamisha kwanza inatakiwa akague kifaa (gar, pkpiki au bajaj) akishamaliza ndo aje kwa dereva kumuuliza pariculars za gar pamoja na wewe mwenyewe dereva lakin polis weng wanakimbilia lesen na kad ya gar lakin kwa utaratib wa kaz hausem hivo. Kuna siku niluikuwa na pikpik nikasimamishwa na trafic police cha kwanza kukimbilia ilikuwa funguo ya pikpik akaizima na kutaka kuichukua kwa kwel kitendo kile nilikereka sana. Na mimi nilimchukulia kama mwizi kwan wazi najua kwamba sheria inamzuia kufanya hivo.
 
kwa siku hizi sababu pekee ya kudai kadi ni kuangalia 'uzito' wa jina lako na la mwenye gari, kabla hajaanza kukuzingua!

Hii ndio haswa sababu. Jina la kadi likifanana na leseni anajua anaongea na mwenye gari, kwa hiyo dau linapanda
 
Pale ccp moshi tulifundishwa kwamba ili ku secure mtuhumiwa. kumbuka kila unaposimamishwa na polisi wewe ni mtuhumiwa. anachukua kadi na lesen kabla ya fiziko examination. Hakuna trafiki anaechukua rushwa hii ni dhana ya urongo na potofu. kama umeshawahi kutoa rushwa lete ushahidi
 
Back
Top Bottom